Sehemu ya 2

2 1 0
                                    

Baada ya miaka 6, tulibahatika kupata watoto wawili mimi pamoja na Agness. mtoto wa kwanza tulimuita Theonest. wa pili Linda na wa tatu Aron. Urafiki kati ya mke wangu na mke wa Richard ulikua umekua sana.

"Babe, leo ntaenda kwa Martha.. kaomba niende hajiskii vizuri.." Agness alinambia akiwa amekaa kitandani

"Saa ngapi unaenda?" Nilimjibu huku nikijiandaa kutoka kwenda kazini

"Jioni baada ya kumfata Theonest shule.." Alinijibu

"Utamsalimia asee, mwambie asidhani nimemsusa.. ntaenda kumuona.." Nilisema

"Sawa baba.." alitabasamu

"Aya bye kipenzi, naenda.." Nilimkumbatia na kuanza kuondoka

"Uwe na siku njema.." Alinibariki

........

"Agness..nina mawazo sana rafiki yangu.." Martha alinambia akiwa na huzuni sana

"Nini tatizo?" Nilikua na shahuku ya kujua

"Mume wangu ananipenda na ananipa kila kitu ninachotaka ila nimeshindwa kitu kimoja tu.. sijamzalia mtoto.." Alisema kwa huzuni sana

"Usijali mama, kila kitu anapanga Mungu, usiache kusali.. utapata mtoto tena watoto wengu. Usijali" Nilimtia moyo

"I hope so, I really hope so..!" Alijibu

Ghafla, simu ya Martha ikaita.. "Hubby" ilisoma

"Hello hubby.." alijibu kwa madaha

"Naendelea vizuri, nipo na Agness hapa ananipa company.." Alijibu.. sikuweza kusikia yaliyokua yakiongelewa upande wa pili

"Hahaha sana, ni zaidi ya ndugu sasa hivi.." Aliendelea

"Woooooh.. kama unanidanganya sitokusamehe milele.." Alijibu kwa furaha kubwa

"Aya nakungoja.." alikata simu

"Mume wangu anarudi leo.. I'm so happy" Alinikumbatia

Hatukukaa muda mrefu gari ya Mr. Richard iliingia. Agness hakuweza kuzuia furaha yake alitoka nje mbio kumkimbilia mume wake, nilisimama kwenda kuchungulia dirishani. Alimrukia wakakumbatiana muda mrefu, mara Agness akaanza kulia huku mme wake anambembeleza. Walipendeza kwakweli

Mara geti likafunguka tena, ikaingia gari nyingine nyeusi nzuri sana.

"Surpriseeee!" Nilimsikia Richard akisema

"Wooooh.." Agness aliruka ruka huku akizunguka kulikagua lile gari akamkumbtia tena mume wake.. kwakweli walipendeza nilifurahi kuwatazama, nilitamani namimi siku moja mume wangu anifanyie hivo

Baada ya hapo, ilibidi niondoke maana niliona kama nawabana

"Agness mbona unaondoka mapema hivi?" Martha aliuliza

"No dear, I just want you guys to be free.." Nilitabasamu kuonesha kwamba sio kwa nia mbaya

"Ntawakaribisha hivi karibuni tufurahi pamoja.." Mr. Richard alisema

"Ahsante.." Nilijibu na kuondoka

Nilifika nyumbani salama, nikaanza kuandaa chakula. Mawazo ya namna Richard na mke wake walikua wakikumbatiana kwa furaha yalinitawala hadi nikajikata kidole.

Muda wote huo sikujua kama mume wangu amesharudi na yupo nyuma yangu ananiangalia.

"Nini tatizo mke wangu.." Nilishtuka nusu nizimie

"Umrnishtua jamani.. sikujua kama upo" Nilijibu kwa hofu

"Unawaza nini kipenzi?" Alisogea karibu na kushika mkono wangu nilipojikata

THE STAINED ALTARWhere stories live. Discover now