WANANGU

7 0 0
                                    

Jimba ni Kijiji kilichoko kasikasini mwa watamu ward county ya kilifi. Ni Kijiji ambacho  ni mahame kwa mtazamo. Kijjini humu hakuna mmea Wala mnyama anaeishi hapa maana eneo Zima limefunikwa kwa jabali ama mwamba wa jiwe kubwa kama wakazi wanavyoita jiwe hilo. Shughuli katika eneo hili ni uchimbaji mawe ya kujengea. Uchimbaji huo umegawanyika katika viwango vya kitabaka kwani wenye njenje wanatumia mashine na mitambo kupasua jabali Hilo ilhali Wala hoi wanao Saka tonge kwenye zana hiyo ya uchumi wanatumia misuli Yao kugonga jiwe hilo zito kama nanga kwa kutumia vibuyu na nyundo. Hapa wake kwa waume humiminika katika machimbo haya na kuchoma misuli Yao huku jasho likiwavuja milini kama maji ya moto. Usemi wa angalia pochi ndo hutumika huku kwani wachimbaji hao hutupilia mbali uchafu wa magwanda Yao na kutaka usafi wa pochi zilizo Nona mabunda ya pesa kuwapamba.
Masaa ya saa tisa unusu hivi kama kumbukumbu za mamangu zinavyosimulia wakati  mwadhini katika mskiti ulioko karibu na machimbo hayo alikuwa akipiga swala lake takatifu,basi mamangu alijupumzisha kwa kutwaa kulicho nonesha tumbo lake kwa kipindi Cha miezi tisa na kunizaa Mimi nkiwa kijusi Cha mtu ndani ya kibanda chetu Cha msonge. Wakunga walinikungua .na kuniosha kisha vitambaa vikuukuu vilivyo pangwa kwa shughuli iyo nilifungwa na tayari nkatolewa kutazamwa na wanakijiji waliokuwa na bashasha ya ajabu.

Eti kua uyaone. Miaka kumi na miwili ilinipata kama mwenye siha sihaba. Ungo refu na wembamba wa kitanashati vilinikamilisha kuwa Stephen imara. Tulicheza na marafiki wa hirimu huko huko machimboni. Mchezo yenyewe hakutofautiana na shughuli za uko machimboni. Tulibeba vipande vya mawe,tukagonga ardini kwa vijiti,tulijenga vijumba na vitu vingi vinginevyo. Machweo ilitupata tulio choka hoi bin tiki. Chakula Cha kuzuia matumbo kilivutia usingizi uliotuacha hoi . Asubuhi tungeamka na kuelekea kwa kazi zetu za kawaida ungedhani mwisho wa mwezi ni donge nono ndo tungejibebea pochini.

Waliosema siku hazigandi hawakikosea. Gafla tu,nilikuwa barobaro. Kuko huko machimboni nilipatana na Binti nilie amini tutaendeleza maisha pamoja. Nilimpenda na kimuenzi kama pumzi ya uhai wangu. 
Ndoa na maandilizi ya harusi vyote vilikamilishwa kwa muda ufaao. Nyama na Michele ya kuchemsha vililia matumboni. Soda na majuisi zikamiminwa vinywani huku wengine wakapiga mabiu na kiteuka kama mbuzi. Lo mbona usiite siku iyo kama ile ya ndovu kumla mwanawe?

Sherehe zilitia nanga. Wakushafiri wakapanda mabasi makuukuu na kusafiri makwao. Haya kazi kwangu Sasa. Mpira umebaki kwangu. Nkaanza heka heka za kutafuta mabao. Mwezi ulipomaliza hesabu zake,wangwana wakaanza kunipa heko kwa ustadi wangu wa kutikisa mpira wavuni. Bibi yangu anamimba. Tumbo ilo. Likaanza kufura kama kitumbua Cha hamira lala.
Mwezi wa tisa ulifika mbio kama umeme. Nkaanza kuhesabu masiku angalau niitwe baba. Taari nilikuwa nikiwaza na kuwazua jinsi tapokea kijusi wangu. Fikra za uzazi zikanitawala. Nkawa mwenye kujilinganisha na wazazi wengine.

Siku ya masiku ikafika. Make wangu akawa mwenye kushikitisha. Vilio vya kite na simanzi vilinibubujisha machozi.nkajihisi mnyonge .doh ,kuko huko milango ya hospitali, nilikuwa nmekaa kitako nje ya wadi ya kina mama. Moyoni nkiomba jalali awaongezee ujuzi manesi na wakunga angalau mke wangu azae salama.
Gafla kimya kilitanda hospitali mzima. Dokta aliye kuja mbele yangu alikuwa mwenye huzuni. Aliinamisha kichwa kama alikosa usemi. Aliponiangalia maneno aliyotoa ni pole shujaa. Doh nilihisi kunyong'onyea. Bila kuuliza lolote mlango ulifunguliwa na nikaashiriwa kuingia ndani. Kumbe naenda kuomboleza. WANANGU mapacha. Vijusi viwili. Wote wamelala maiti. Bahati mamayao alinusurika mauti. Tuliomboleza na kusahau yaliopita

You've reached the end of published parts.

⏰ Last updated: Jun 27, 2022 ⏰

Add this story to your Library to get notified about new parts!

WANANGUWhere stories live. Discover now