Daraja bila Faraja.

0 0 0
                                    

Leo ni siku ya ijumaa. Siku hii pia ni ya furaha na shangwe katika uwanja wa JKIA. Vigelegele, nderemo na vifijo vya kila Aina vimejaza hewa mle uwanjani, kwani ni kipi linalotukia?,Leo ni siku ya furaha na Bashasha kwani ndege imewasili na kutua humo. Imewasili huku imembeba mwana wao mpendwa.
Mpendwa wao anafahamika kama Saida, Leo ametua kutoka nchi ya nje. Mamake Bi Pauline amejawa na machozi ya furaha anapomtazama akishuka kutoka kwenye ndege. Umekuwa ni muda mwingi Sana tangu kuonanana ana kwa ana. Saida alikuwa amefika na begi mmoja ilikuwa mabegani make. Hatimaye ana lakiwa kwa shangwe na nderemo huku ikifuatiwa na nyimbo za kitamaduni. Saida aliliabiri Gari moja Aina ya taxi pamoja na mamake mzazi na kuelekea moja kwa moja Hadi nyumbani kwao, baada ya kuwasili atapata kupumzika na kupumzisha nafsi kwani amechoka, sio kuchoka sababu ya safari, amechoshwa na Maisha huko katika nchi ya nje,amechoka na dhiki na taabu, Amechoka na mateso, mateso yaliyomsbabishia kurudi na majeraha mwilini mwake. Ilikuwa muda wa miaka Mitano tangu kutoka nyumbani na kuelekea ughaibuni, madhumuni Yake ni ilikuwa ni kutafuta Maisha mazuri mapya, sababu ya kusaka Maisha mazuri ilikuwa ni kuwa nyumbani palikuwa hapakaliki na aliona vyema kuwa Ajira ya nje ingepata kumsaidia pakubwa lakini hata hivyo alipataje kusafiri Hadi ughaibuni?,Saida alikuwa ni msichana ambaye hakubahatika kumaliza kidato cha tatu sababu ya Karo, Hali ya nyumbani na hata pia matokeo yake katika mtihani shuleni.
Mzee Walter bake Saida aliipiga dunia sababu ya ugonjwa wa saratani. Mzee Walter alijulikana kwa kuwa mkakamavu Sana kwani yeye ndiye aliyekuwa akihakikisha kuwa Karo ya shule ya Saida imelipwa. Maisha ilianza kuwa na Panda shuka nyingi tangu Mzee huyo huenda jongomeo, Hilo ilimlazimu Bi Pauline kujaribu juhudi zake zote za kihalali ili kukidhi mahitaji yake pamoja na ya mwanawe lakini alifaulu kweli?
Saida pia hakuachwa nyuma kwa kazi, alilazimika pia kutumia ujuzi aliokuwa nao aliofunzwa na mamake kwa kuvipika na kuviuza vitumbua na matobosha Barbara I angalau kujiruzuku. Yote haya yalifanyika kwa muda Hadi nyakati ambapo Maisha Yao yalikuja kubadilika na kuuchukua mkondo mpya.
Yangebadilika sababu Mzee mmoja alikuja kwa madhumuni ya kuishinao, alifahamika kama Mzee Wema Fadhili alikuwa ndiye rafiki wa karibu na mwandani wa familia ya Marehemu Mzee huyo, yeye ndiye aliyehusika vikubwa katika kusimamia mazishi ya mwandani wake aliyejuana Nate kwa muda mrefu. Mzee Fadhili hakuja kama mgeni,alikuja kama Bake Saida. Kwanini hivyo? alikuja kama Babake Saida. Kwanini hivyo?
Ilikuwa ni purukushani na Jambo lililoleta makunjubo nyumbani humo lakini ilikuwa njia ya pekee kwani Mzee wama alimuarifu mamake Saida mambo yaliyomtisha. "Hero uje kuoleka kwangu sababu usipo, sitakuwa na budi ila kupiga ripoti na kuarifu idara ya polisi kuwa unawauzia watu vileo na kupika pombe haramu, kwa hivyo chaguo ni lako", alisema. Jambo hili lilimtia kiwewe na kumkosesha usingizi kwa siku kadhaa, Mzee Fadhili alikuwa kampa wakati wa kufikiria Jambo ya muda ilikuwa umeanza kudidimia na alitaka majibu. Mzee huyo alikuwa tayari kuenda kupiga ripoti sababu alijua kuwa Bi Pauline angekataa tena, kwa Mata ya pili. Uamuzi wake mamake Saida ukafanyika na akabaki kuishi siku zote kwa kujuta na kudondokwa na machozi kila usiku, ilimbidi yeye kunywa mringa ili kujituliza nafsi yake kila uchao huku akishikilia picha ya Marehemu Mzee Walter.
Mzee Fadhili aliposhika usukani kuwa mwenye kiti wa nyumba hiyo hofu ilianza kutanda nyumbani humo, mamake Saida alianza kupata majeraha ambayo hakuwepo nazo kabla ya mazishi kwani alikuwa akipokea vichapo kila wakati Mzee Wema alipokuwa akiwasili nyumbani na chupa ya kileo alichopenda kunywa. Ilikuwa ni Hali ya mazoea kila wakati ambapo Sheria zake alizoweka mwenyewe hazikuwa zinatiliwa maanani. Hali hii ilizidi kuwa mbaya kwa Saida lakini licha ya hayo hakuweza kufanya lolote hata kuita usaidizi wa karibu kutoka kwa majirani sababu alijua vyema angejaribu hivyo angekuwa akipigania Maisha yake katika katika Hospitali ya kitaifa.
Saida hakujua la kufanya wala pa kuenda, lakini pa kuenda palikuja kupatikana. Uamuzi haukuwa wake wa kuolewa Bali ulikuwa wa lazima sababu "Babake" aliyafanya Maisha yake nyumbani kwao kuwa magumu kwa Sheria ambazo hata yeye hakuweza kuzifuata na pia alikubali kwa shingo upande. Hapo mamake Saida pia alimuunga mkondo Mzee Fadhili sababu kupinga kulikuwa mambo mengine ambayo hayawezi kuelezwa.
Saida hatimaye aliozwa kwa Mzee aliyetambulika kama Mzee William. Mzee huyo alijulikana kwa kuwa mkwasi. Ilikuwa ni siku ya huzuni wakati Bi Pauline alipomuachilia mwanawe kuenda kuishi na mtu aliyemzidi umri kwa umbali Sana. Ilikuwa vigumu kwake kuhimili lakini hamna lolote ambalo angeweza kufanya ila Tu kumuombea kwa Jalali. Saida alikuwa akiishi Maisha ya kitajiri. "Hapa ndio kwetu, karibu nyumbani!". Hakuhisi kuwa amekaribishwa, alihisi kuwa ni mwanzo wa utumwa kamili lakini Mzee huyo alimhakikishia kuwa hangejutia kuishi humo. Ni kweli kuwa Maisha humo yalikuwa ya kuridhisha kwani hata hewa ndani humo ilikuwa yenye harufu ya kitajiri.
Hofu yake ilipungua alipohisi ukarimu alipohisi ukarimu wake Mzee huyo lakini hakuhisi utulivu nafsini mwake, alikuwa bado nazo fikra za kurejea ili kumjulia mamake Hali asije akafia mikononi mwa "jambazi" huyo kama alivyomtwika Hilo jina. Alikuwa sasa akihofia usalama wa mvyele wake badala ya wake binafsi. Ukosefu wa utulivu ulizidi kumpanda na kuongezeka nyakati ambapo hakuruhusiwa kutoka nje ya jumba Hilo baada ya siku chache ya kuuona jumba Hilo kwa nje ulivyokuwa wa kuvutia.
Aliwekwa ndani na kufungiwa kana kwamba alikuwa mfungwa. Mzee huyo alikuwa akimfungia kila siku nyakati za asubuhi akielekea kazini na kufungulia jumba lake nyakati za machweo hata ingawa hakufahamu ni kazi gani aliokuwa akishughulika nao haswa.
Alianza kutoaminiana Sana naye na alitamani Sana kutafuta mbinu jinsi atakavyokwepa mahalo hapo. Alijaribu njia zote lakini juhudi zake hazikufua dafu. Wakati mmoja alipokuwa alijaribu kutafuta namna ya kulifungua lango la nje, aliduwaa Sana kwa kumpata kijana mmoja ambaye alikuwa na mtazamo wa kumfahamu,hakumbuki aliwahi kumuona wapi maishani lakini alikuwa na uhakika kuwa aliwahi kumuona, ndipo yalimfika Mambo na kutaamali jinsi yalivyokuwa baada ya kufikiri Sana. Sura hiyo aliwahi kuiona akiwa katika shule ya upili, hakuyakumbuka mambo mengi lakini anakumbuka kuwa utangamano wao haukuwa mzuri naye wakati walipokuwa shuleni. Kila wakati Josee alikuwa na matatizo Sana yaliyosababishwa na Saida, anakumbuka vyema shuleni kuwa yeye ndiye aliyekuwa kiranja na viranja shuleni walikuwepo na mamlaka ya kuwaadhibu wanafunzi haswa wale waliokuwa katika kidato cha Kwanza, alikuwa anawapa adhabu Kali Sana wanafunzi shuleni kuliko walivyoweza kuhimili, hili liliwafanya wanafunzi kuwaogopa Saida na wenzake na hata kulazimu wengine kuhamia shuleni zingine.
Jose pia alikuwa akitaamuli kuila adhabu zake wakati huo akiwa katika kidato cha Kwanza, alipata adhabu ya viboko kutoka kwa waalimu na Saida kumwaamuru kuusafisha uwanja wa gwaride kwa mwezi mmoja mfululizo, hakuyakumbuka aliyoyafanya lakini kila wakati ilikuwa yeye kuusafisha uwanja huo pekee yake kila asubuhi kabla ya masomo kuanza na jioni baada ya masomo kukamilika, alikuwa akirejea nyumbani akiwa mchovu kama aliyekuwa ametoka kuliwahi jengo zima yenye majumba mengi na yote haya aliyafanya kwa kukosa Sare Rasmi ya shuleni, alitamani kusema sababu lakini hamna aliyemsikiza.
Saida hakutaka kusubiri kuyaona madhumuni Yake Jose yalikuwa yepi, alianza kuvifunganya virago vyake na kupanga mikakati ya kutoroka humo,ombi lake likiwa asipate kumwona jicho kwa jicho wakati wa kutoroka lakini hivi angekwepa aje na kila lango hapo lilikuwa limefungwa? Aliwaza Sana na kuwazua. Wakati mmoja nyakati Mzee William alipokuwa akirejea kutoka kazini, ndipo aliposhuhudia mshtuko na kuduwaa kwani pindi Tu alipofungua lango kuu la nyumba, aligutuka karibu kuangushwa Chini kwani alikwenda kwa mwendo wa Kasi ungedhani alikuwa mwanariadha.
"Mshike huyo!!" Alisema Mzee huyo kwa sauti ya juu,"Asijaribu kutoroka huyo!"lakini wakati alipomaliza kuyasema maneno hayo alikuwa tayari amesha chana mbuga na kukwepa humo na kutafuta njia ya kuelekea mahalo pa bustani ya magari na kuliabiri Gari moja ndogo akiwa tayari kuelekea aliokuwa anaishi rafikiye Christine. Safari ilikuwa ndefu lakini hatimaye aliwasili nyumbani kwake inshalaah. "Christine, mwandani wangu wa zamani,muda mrefu sana tangu kuonana kwetu!!"alisema Saida huku akikimbia kumkumbatia,"Nami pia nimetamani Sana kuiona Sura hii yako kama ya tausi,"alimjibu huku akimtania. Saida alijawa na furaha na pia alihisi mzigo wa Makazi umeshushwa angalau angepata mahala pa kupumzisha mtima wake wakati huo. Walirejelea nyakati zilizopita na panda shuka zao za kiamaisha, baina ya hao wawili Saida ndiye aliyeonekana kuwa na shuka nyingi kuliko panda. Wawili hao waliweza pia kurejelea nyakati ambazo zingekuja kujiri na vitu ambavyo wangedhamiria kufanya hapo siku za usoni na hapo ndipo Christine alipozua hoja moja ambalo alikuwa nao Kwa muda. Hoja ambalo Saida alitega sikio kwa makini sana,ni hoja ambalo lingeweza kubadili Maisha yake mile,hoja ambalo angeishi kuwaambia watoto,wajukuu na vitukuu wake.
"Dadangu kuna kazi ambayo inasemekana kupatikana katika taifa la nje la ughaibuni", alisema Christine,"Alaa!eti wasemaje?"aliuliza Saida kwa mshangao na mshtuko yote kwa pamoja. "Mbona wabung'aa namna hiyo?"aliulizwa,"Naam ndio nafasi ya kazi ipo!"alisema kwa sauti ya kumhakikishia. Fikirini mwake Saida aliona ahueni mbeleni pindi Tu angepata fursa ya kazi hiyo lakini mlikuwa na swali ambalo kuuliza kulikuwa ni kwa lazima.
"Hivi ni kazi ipo ambayo tunakwenda kushughulika humo?"aliuliza Saida. "Ni kazi kidogo Tu za nyumbani zenye majumba makubwa yanayomilikiwa na mabwanyenye!" alimjibu Christine.Hoja la kazi kwenye majumba makubwa hayakumtisha badala yake ilimjaza na hamu ya kutaka kuwa kazi Aina hiyo. Bila ya kusita wala kujawa na mawazo chungu nzima alikubali wazo Hilo la Christine ingawa hakujua ni nchi ipi atakakojipata akifanya kazi lakini alikuwa na matumaini kuwa Maisha yake yangebadilika si haba,aliona Jambo hili kuwa kama ahueni angalau kujikwamua kutoka Maisha hayo yaliyokuwa kama kifuu. Iliwalazimu Kwanza kuwajibika mambo kadhaa kabla ya kusafiri, mambo kama vile kufunzwa njia tofauti ya kufanya kazi na jinsi ya kutangamana na watu wa nchi za ughaibuni.
Baada ya hayo Saida alijua ametokota na kuiva katika sehemu isiyo karibu na nyumbani kwao,muda mfupi baadaye, baada ya kujipanga na kujiweka vilivyo alikuwa na mwandani mwenzio kwenye ndege tayari kuelekea Hadi alikostahili kuwahi shughuli. Safari yake pamoja na ya mwenzio haikuwa ya kufana wala yenye Raha sababu ilimbidi yeye kustahimili Hali ya safari Kwa njaa sababu ya ukosefu wa uwezo kifedha kukidhi mahitaji ya chakula, aliwahi wakati mmoja kumuuliza wakala wake jinsi Hali hiyo ingeshughulikiwa lakini wakala huyo alimhadaa kuwa angegharamiwa kila kitu kwenye safari hiyo kwenye ndege. Mstahamilivu hula mbivu ndio maneno yaliyokuwa yakizunguka akilini mwake. Alipowasili alihisi kana kuwa amefika mbinguni kutoka kwenye mateso ya Ulimwenguni. Saa chache baadaye alipata kuelekezwa mpaka mahala pale pa kazi. Aliona yote aliyojitoloea yalikuwa ya afadhali, kwani alijitahidi sana kuyauza matobosha na bhajia barabarani ili kupata fedha ya kumwezesha kukata tikiti ya ndege na pia mchango kutoka kwa familia ambaye ilikuwa ni mama mzazi ili kufaulu. Mzigo wake mmoja begani na mwingine kwenye mkono wake na kuelekea mahala ambapo alipata ufadhili tokea kwenye uwanja wa ndege Hadi ambapo alipata kufika kuonana na muajiri wake katika afisi za ubalozi wa nchi yake alikotoka. Wakala waliokuwa wakihudumu katika afisi hizo walimpa maneno ya kumhakikishia usalama,ubora na kuimarika atakakoelekea. Saida alimpungia mkono wa buriani Christine kwani rafikiye alikuwa akielekea kwingine kujiruzuku lakini waliahidiana kuwa na mawasiliano pindi Tu walipoachana. Hatimaye alipata kuwasili alikostahili kufanya kilichohitajika. Shida zake zingekuja kufika kikomo, hivyo ndivyo alivyofahamu, aliweza kuhudumu katika jumba Hilo huku akiwa na hofu kwani kungekuwa na vikwazo sababu yeye hakuwa wa asilia ya nchi hiyo lakini yote yalikuja kuwa tofauti na dhana zake, watu humo walimpa Amani Sana lakini fauka ya hayo Amani hiyo ilikuja kudumu kwa takriban miezi miwili hivi tangu kuanza kwa kazi yake humo na hapo ndipo alipoanza kuyashuhudia mambo kubadilika.
Mambo ambayo hakuyaona katika muda huo mdogo aliokuwa akiishi hapo. Nyakati zilipozidi kusonga ndipo kazi za kuwahi zilizidi kuongezeka mithili ya kuwa mizigo mizito. Maswali na kuwaza ndivyo ilivyokuwa desturi yake kuhusu mambo yalivyokwenda kwani hayakuwa kama alivyoyabashiri kwani alikuwa akijihimu alfajiri na mapema na kushtaki usingizi usiku wa manane, alikuwa akifanya kazi humo Hadi ukafika wakati ambapo mgongo wake ulikuwa ulikuwa ukihisi maumivu makali na miguu yake kufura, fikra zilimjia jinsi angepata tiba lakini lo! angepata wapi?
Wakati mwingine alikuwa akistahimili Hali bila kushyaki njaa na kujawa na utaksiri wa kupata chakula, muajiri wake alimtaka kufanya kazi kwa wingi na kwa utahabibu mithili ya panga kutikiswa, alifedheheshwa sana na Hali hii, hakuwa na budi ila yeye kumwendea muajiri wake na kumuarifu kuhusu misukosuko na mahangaiko yake na hata pia kumuarifu kuhusu matakwa yake, alidhani amepitia mengi nyumbani humo kumbe safari bado kwani badala ya kushughulikiwa na muajiri wake mwili wake ulianza kuvimba na kufura zaidi kwa vile vichapo alivyokuwa akivipokea kutoka kutoka kwa muajiri wake, anataamuli wakati aliposhambuliwa na muajiri wake na kuanza kumpiga pasipo na kosa. Hali hii iliendelea kuwa ya kudhoofisha kwani hata kutoroka haikuwa ni Jambo la kufikiria kwani kila wakati alipojaribu Hilo alifungiwa nafasi ya milango yote na kumlazimu kusalia humo. "Kwanini barabara hii?"alijiuliza fikirini,"kwanini kivuko hili yaonekana kuwa na ajali nyingi Sana kwangu?!". Hakujua la kufanya wala wa kumuendea wala pa kuegemea sababu mwandani hakuwepo karibu, zaidi ambalo angeweza kulifanya ni kuzungumza naye bila ya kuonekana na muajiri au angekuwa akihesabu muda wake Ulimwenguni. Mshahara wake nao haukuwa wa kuongea kwani ulikuwa umepungua Bali na ule wa makubaliano. Yote yake aliyaona kama yamekwisha kwani muajiri wake aliamuru kuyafanya ambayo Saida hakuwahi kuya fikiria wala kudhamiria. Wakati mmoja ulipokuwa umetimia mida ya saa sita usiku, alimketi Chini,"Leo safari yako inakomea humu, nataka nikumalize leo!" ndiyo maneno aliyoyasikia kutoka kwake, hakuwa na Budi ila kuyakubali Ila aliomba fursa ya kuweza kuwasiliana na mamake mzazi na kumuarifu kuwa iwapo angeipiga Dunia teke mikononi mwake, masazo yake yasafirishwe Hadi nyumbani kwao na hapo ndipo alipoyafumba macho yake na kuyasema maombi yake ya mwisho. Ghafla kilochoonekana kuwa la dharura lilitokea katika rununu ya muajiri na kuliweka bastola yake Kando, aliyafumbua yake macho na kuduwaa ikiwa bado angali hai au anawasalimu Malika Jibril na waliokuwa wakimzunguka, alichukua fursa hiyo na kukimbia kwenye chumba chake cha kulala na kukifungia kwa ndani pasipo na yeyote ambaye angeweza kuingia humo. Alibung'aa kuamkia kwa habari kuwa afunganye virago vyake asijue anakoelekea. "Nimechoshwa na uhai wako humu hebu jiweke tayari nikupeleke kwa familia yako mpya", alisema muajiri. "Familia mpya?" ndio maneno yaliyomjia fikirini, hakuwa na la kusema wala la kufanya Ila kutii amri kwani alijua familia hii mpya ingemkubali kwa uzuri. Kufikiri kuwa kutoka kwa muajiri wa Kwanza na kuelekea kwa wa pili eti mambo yangekuwa ni ya heri ilikuwa ni kujidanganya, yalikuwa ni kama kutoka kwenye karai yenye koto Hadi kwenye Moto wenyewe akiwa kumo alikumbana na visivyotajika kwani muajiri wake alijaribu kumnajisi kila alipopata fursa lakini alifeli kulikuwa na vita ambavyo Saida alikataa katakata kwa lazima kutumika visivyo, hata hivyo akistahamili kuwa na majeraha kila tendo Hilo lilipotukia, isitoshe malipo yake yalikuwa finyu Sana kulinganisha na ule ujira wa muajiri wa Kwanza.
"Siwezi tena, nimejaribu kulivuka daraja hili na linaonekana kuwa na mamba wengi ambazo Wana Nia ya kunila Mimi", alisema wakati mmoja alipokuwa akiwaza. Alichoshwa na Hali hii ya taabu hata ikiwa aliwacha stakabadhi zake kwake muajiri wake wa Kwanza, aliamuru liwalo na liwe, aliamua kutoroka nyumbani humo pindi Tu alipopata nafasi, lakini angefanyeje na milango yote yalikuwa yamefungiwa yeye kutoroka, hapo ndipo aliona kutekeleza hoja moja lililokuwa fikirini mwake, aliufunga dawari na kushuka Chini tokea kwenye roshani ya jumba Hilo kubwa na kisha baadaye kutua Chini na kuchana mbuga yeye na virago vyake vidogo alivyokuwa navyo. Ilikuwa ni sharti yeye kutoroka nusura muajiri wake kumuona au ungekuwa ni kujitosa kwenye tundu la Simba,alikimbilia kwenye bustani ya polisi sababu alikuwa ametebwereka na Maisha hayo ya utumwa, akikimbia ili kujinusuru na kuweza kumuomba polisi mmoja fursa ya kuvutia waya ambapo angepata usaidizi kwa haraka. Hali ya wasiwasi ilimjia kwani alijaribu kumpigia Christine lakini hakupata jibu, aliwaza ikiwa kuna Jambo lililomtokea mwenzio ya kumfanya kuogopa. Alijaribu tena kumpigia wakala wake katika ubalozi na kile alichopata ni kutukanwa na kuambiwa kuwa ni mwiba wake wa kujichoma, msaada wa mwisho pa kujitwaa ulikuwa ni Kwa mamake mpendwa, kulikuwepo na mshikamano wa mawasiliano lakini mwishowe alipata kuisikia sauti yake mama."Mama wee!mamangu Leo nimefurahi tena sana kuisikia sauti yako tepetepe ya kumfariji mtu"alisema.
"Naam asante Sana mwanangu kwa Hilo, umekuwa ni muda tangu tulipowasiliana kawani kuna kipi kimetukia?"aliuliza Mama. "Enhe mama ninaomba usaidizi wako maanake hamna yeyote ambaye angeweza kunipiga jeki Ila wewe Tu ", alisema mwanao huku akijikaza asije kuusikika akijiliza akizungumza na mvyele wake. "Wanitia hofu hebu nieleze ni kipi kilchokufila?"aliuliza tena mama mtu,alimueleza yaliyomfika nakumuomba usaidizi kwa jinsi angeweza kurudi nyumbani nchini kwao sababu huko alikokuwa kila pumzi aliokuwa akiuvuta alikuwa akinusa kifo mbeleni. Mamake upande mwingine alipoyasikia maneno ya mwanao alishindwa la kufanya sababu hata kujinusuru yeye ilikuwa ni Kwa kudra za Ilahi. Aliwaza huku akitoka dukani alikotumwa na Mzee janadume mwenye nyumba, na ilimbidi yeye kuharakisha asije kushuhudia ukali wake Simba.
Aliendelea kuwaza pindi Tu siku zilipozidi kusonga huku akizidiwa na hofu ya kumpoteza mwanao, huku kwingine baada ya mawasiliano hakuwa na Budi Ila kusalia gerezani sababu ya kukosa namna ya kuishi. Ilikuwa ni kun faya kun kukumbatia Maisha hayo na kuishi kama mfungwa huku akiweka matumaini kuwa jibu ingemjia kutoka nyumbani mwao.
Masaa yalipozidi kusonga ndipo matumaini yake yalipozidi kufifia kuhusu kupata suluhu ,masaa yakageuka kuwa siku, siku nazo zikabadili na kuwa muda mwingi. Swali jingine likamtokezea akilini ikiwa angewahi kurejea nyumbani na hapo ndipo alipoteza hamu ya kusubiri na kuendelea kuyazoea na kuyafahamu Maisha ya ya ufungwa Hadi siku ambayo angepata ahueni na kuenda akhera. Maskini hakujua la kufanya.
Ilikuwa sasa ni kufuata ratiba ya jela Kwa kujihimu nyakati za mafungulia Ng'ombe na kuchapa kazi mfululizo na kusubiri chajio mwisho wa siku na baadaye kushtaki usingizi. Desturi ilikuwa vivyo hivyo Hadi ule wakati mmoja alipokuwa akijiweka tayari Kwa shughuli za siku ndipo mmoja wa Askari katika katika jela hizo kamsimamisha,alianza kuwa na dhana kuwa ameongezewa miaka yake ya kifungo au kusafirishwa Hadi kwenye jela nyingine sababu siku kabla ya hiyo alikumbuka akilumbana na mmoja wa Askari jela kuhusu Jambo Fulani.
"Msichana hebu kanifuate!"alisema Askari hiyo, hakujua ni kipi kingetukia Kwa wakati huo,masaa chache baadaye alishuhudia Kwa mara yake ya Kwanza kuachiliwa huru na kuelekezwa katika uwanja wa ndege mojawapo za huko ughaibuni na baadaye safari ya kurejea kwao nyumbani iliwadia. Lakini ilikuwaje namna hii?
Sababu mamake akikumbuka vizuri hakuwa na chochote wala lolote la kumsaidia naye pia Tu kuishi Kwa Imani au pengine alikuwa ni marehemu babake au pengine ni Mzee Fadhili aliubadili mtima wake na kufanya kama jina lake? hata hivyo alijawa na furaha nyakati ndege ilipotua Uwanja wa JKIA na kuwasili nyakati za usiku. "Karibu nyumbani!"alisikia sauti hiyo katika uwanja. Hapo alipowasili usiku alifahamu ule msemo wa siku njema huonekana...
Aliwasili na kulakiwa na Mamake,na kijana aliyefahamika kama Jose. Machozi ya furaha iliwajia Saida na mamake walipokutana tena,alitanabahi na pia kuliwaza kwanini kijana huyo amejitwika jukumu la kuuonyesha uso wake humo, baada ya masaa machache aliliabiri gari lililomfikisha Hadi nyumbani na hapo ndipo alipopata habari kamili kutoka kwake Mama,alipata kusikia kwamba ni Jose ndiye aliyehusika na ufadhili wake kutoka kwenye jela za ughaibuni Hadi nyumbani na isitoshe alimuarifu jinsi Jose alivyokuja kugundua kuhusu jinsi Hali ilivyokuwa kwani alipomuona mamake dukani akimvutia mwanao waya,alikuwepo dukani na kupata kuyasikiza kile walichokuwa wakinong'onezana Kwa sauti ya juu na pia alikuwa amemfahamu mamake Saida tokea siku za jadi alipokuwa akija shuleni kumuona mwanawe. Aliweza kumfumbulia habari zake Mzee mwenye nyumba na jinsi yeye mama Saida alivyotoroka na kukwepa bonge Hilo la janga humo na kupata usaidizi katika mojawapo ya nyumba za kukodi kama usaidizi kutoka kwake Josee ,wangeishi humo Hadi wakati ule ambapo wangepata nafuu kwani iliwalazimu hao kujiradi na kutafuta Maisha upya tena kwani hawakuwa na pa kukimbilia isipokuwa hapo walipokuwa. Saida hata hivyo ilikuwa ni Ombi lake kutopatikana na lile Janadume aliloozeshwa ili asije kumuongezea shida juu ya matatizo alipokuwa nazo na fauka ya hayo alianza kuwaza ikiwa mwandani mwenzio alifariki mikononi mwa muajiri wake au Kwa kudra za mwenyezi yupo hai.
Siku chache baadaye alipokuwa akifurahi kuila izu Kwa utaratibu, alisikia habari kwenye redio iliyoku karibu na kitanda chake kuwa kulikuwepo na mshukiwa ambaye amekamatwa Kwa Madai kuwa mlanguzi wa watu pamoja na madawa ya kulevya, aligutuka aliposikia kuwa ni lile Janadume Mzee William na Christine alikuwa mshukiwa mwenza kwenye kesi hiyo. Karibu chozi limtoke lakini akakumbuka kuwa hayupo jahanamu tena. Wazo kuu kwake Kwa wakati huo ulikuwa ni kutafuta Maisha mapya sababu mamba walikuwa wengi wa kuzuia njia yake ya kupata ufanisi wa kuvuka, alikuwa na jukumu tena ya kulitafuta mbinu jingine ya jinsi angelivuka daraja.

You've reached the end of published parts.

⏰ Last updated: Jun 05, 2023 ⏰

Add this story to your Library to get notified about new parts!

Daraja bila Faraja Where stories live. Discover now