SIKU 10 ZA KINABII (WAFALME10)

0 0 0
                                    

Kitabu cha ufunuo ile sura ya 2:8-11,inazungumzia mambo magumu sana ambayo watu wengi wameshindwa kuyatatua au kuyaelezea,

Lakini leo nataka tufanye uchambuzi kidogo juu ya Eneo hili.

Kitabu hiki cha Ufunuo wa Yohana kinakisiwa kuandikwa kati ya Mwaka 95/96BK na YOHANA MTUME,Chini ya utawala wa Mfalme Nero ambaye alikuwa ni mtawala kwa kipindi hiko na Alihusika sana katika mauaji ya watu wengi waliokuwa Wakitangaza Neno la Mungu.

Na miongoni mwa watu hao alikuwepo YOHANA MTUME ambaye anasadikiwa kuwa mdogo kiumri kati ya mitume wote wa BWANA YESU,na Kifo chake lilitokea katika mwaka ule wa 100BK(Baada ya Kristo).

Kitabu hii kiliandikwa na yohana akiwa ndani ya kisiwa cha Patmo ambacho kilikuwa Ni kisiwa maarufu kwa kuwakomesha wafungwa sugu kwani ni eneo ambalo lilikua na baridi kali sana pamoja na wanyama wakali na kazi nzito.

Hivyo kwa ufupi wa hali hii ni kuwa Yohana alipelekwa kule kwasababu alionekana akiendelea kutangaza habari za YESU KRISTO.

Sasa Akiwa yupo PATMO ,YOHANA aliomba apewe siku kwaajili ya kumwomba Mungu wake na kwa hali hilo alipata kibali na Akapewa ruhusa na inakisiwa siku hiyo ilikua ni jumamosi kwa kalenda yetu ya sasa,

Na akiwa kule alipewa mambo Mengi ikiwamo na hii ya kuwa katika dhiki Muda wa siku 10,sasa naomba unifatilie kwa makini hapa

Hapa kiluchokuwa kinazungumziwa si kwamba kanisa litahangaika kwa siku 10 HAPANA,Bali ni unabii uliokuwa unawapa jinsi kanisa litakavyopita kwa mateso ndani ya tawala kumi zitakazo tawala Dunia kwa kipindi cha kuanzia kanisa la SMIRNA.

ANGALIA ORODHA HII YA WAFALME 10 WALIOTESA KANISA,

1.Kaisari Domitiani mwaka wa 96BK Alimtupa yohana katika kisiwa cha patmo

2.Kaisari Trrajan mwaka 98-117BK Aliendeleza mateso ya kanisa,hapa alikuwepo kiongozi au Askofu wa kanisa la Smirna aliyeitwa polikapu,huyu aliteswa chini ya utawala huu.

3.Kaisari Hadrian mwaka117-138BK Mateso kwa kanisa yanaendelea tu kwa utawala wake

4.Kaisari Antonius pius mwaka138-161BK  huyu alimwua Askofu Polikapu amabaye alikuwa mwanafunzi wa Yohana Kule Efeso.

5.Kaisari Marcus aurelius mwaka 161-180BK Aliendeleza mateso kwa kanisa la smirna

6.Kaisari Sevenus mwaka 193-211BK Aliendeleza mateso kwa kanisa,

7.Kaisari Maximini mwaka 211-238BK Aliendeleza  mateso kwa kanisa.

8.Kaisari Decius mwaka 249-251BK Aliendeleza mateso kwa kanisa.

9.Kaisari Valerian 251-260BK Aliendeleza mateso ya kanisa

10.Kaisari Diocletian mwaka 284-305BK Huyu ndie kaisari wa mwisho anaekamilisha siku 10 za Mateso  ya kanisa mpaka Tangazo la Amani kati ya Serikali ya RUMI NA KANISA iliyofanyika mnamo mwaka310BK.

Kwahiyo hiyo ndio chambuzi ya sura hiyo na mistari yake,hivyo ni Muhimu kujua matukio ndani ya Biblia ili mtu asikudanganye kabisa kwa upotovu na ukajikuta umepotea njia.MUNGU AKUBARIKI

•Imeandaliwa na Mtume Mwl Amos Ngosha
Mawasiliano
+255784570700
+255622573146
+255675691700

Kamu telah mencapai bab terakhir yang dipublikasikan.

⏰ Terakhir diperbarui: Nov 23, 2023 ⏰

Tambahkan cerita ini ke Perpustakaan untuk mendapatkan notifikasi saat ada bab baru!

UFUNUO SURA YA 2:8-11Tempat cerita menjadi hidup. Temukan sekarang