Hiki ni kitabu cha unabii katika Agano jipya,na kitabu cha 66 katika biblia ya kawaida inayotumiwa na protestanti,
•Protestanti ni makanisa yaliasi au kutoka katika imani potofu ya kikatoliki.Jina la kitabu linatokana na ujumbe uliomo ndani yake ambao alipewa yohana katika mateso ya kanisa chini ya utawala wa Rumi.(Roman Empire).
Neno UFUNUO Kwa kilatini linaitwa "Revalatio",Likiwa na maana Tegua kitendawili.
Kwa kigiriki linaitwa "Apokalipsi"(Ondoa shela) kwa kiswahili.
Mwandishi wa kitabu na Tarehe ya kuandikwa
•Mwandishi wa kitabu ni Yohana mtume wa Yesu .Ambaye alihusika katika uandishi wa
-Injili ya yohana mtakatifu
-Nyaraka 3 za injili ya yohana
-Ufunuo wa yohanaKuna Yohana wa Aina 2 hapa ambao wanachanganya watu sasa watofautishe hivi,
Yohana mbatizaji
•Baba yake ni Zakaria kuhani
•Mama yake ni ElisabetiYohana wa Ufunuo
•Baba yake ni zebedayo
•Mama yake ni Salome
Ambapo familia yao ilikuwa ni ya wavuvi.Yohana wa zebedayo aliandika vitabu vitano kama tulivyoainisha hapo juu,
NA
Yohana mbatizaji aliandika kitabu kimoja tu.Kitabu hiki cha ufunuo wa Yohana kiliandikwa kati ya Ya Mwaka 95-96BK (Baada ya Kristo)
Kitabu hiki ndicho kilichoonyesha ushindi wa Yesu katika Dunia na hukumu ya shetani katika Biblia kuliko vitabu vingine vyote.
Key verse ya kitabu hiki ni
Ufunuo1:19
"Basi uyaandike mambo hayo uliyoyaona ,nayo yaliyopo na yale yatakayokuwa baada ya hayo".(Makundi ya Tafasiri ya kitabu cha Ufunuo).
•Kitabu cha Ufunuo
•Kitabu cha Historia
•Kitabu cha Unabiikitabu hiki kiliandikwa chini ya Utawala wa Mfalme wa NERO wa Rumi,ambaye alikuwa Mfalme katili sana.
swali:>>Kwanini Rumi inatajwa??
Wakati huo Rumi ilikuwa inatawala na hata Yesu anazaliwa bado Israeli ilikuwa iko inatawaliwa na "DOLA YA RUMI".Kitabu hiki kina sura 22
Kina mistari 404
Kina maneno 12,000• Yohana aliandika kitabu hiki akiwa katika Kisiwa cha (PATMO)Kilichoko Mashariki ya Kati ,Eneo linaloitwa Asia Ndogo ambayo sasa hivi ni Uturuki.