1.Yohana alimwona Yesu akiwa katikati ya vile vinara saba vya taa ya dhahabu akiwa na nguvu na uweza mkuu na enzi,hivyo vinara vya taa saba ni hayo makanisa saba(Ufunuo1:2)
2.Vazi lililofika miguuni ,vazi lililovaliwa na kuhani mkuu ambapo huonyesha ukuhani na utakatifu wa Yesu kristo(Ufunuo1:13,Daniel7:13,Ezekieli1:26)
3.Kufungwa mshipi wa Dhahabu matitini,huonyesha kuwa yeye ni Mfalme na ni utayari wa kutenda,(Ufunuo1:13)
4.Nywele zake kama sufu nyeupe na kama theluji,huonyesha utukufu wake(Ufunuo1:14)
5.Macho yake kama miali ya moto,huonyesha kuwa yeye ana uwezo wa kuona kila kitu na ana uwezo wa kutambua makusudio ya moyo wa Mtu,hakuna kilichojificha mbele yake,(Ufunuo1:14,Ebrania4:12)
6.Miguu yake kama shaba iliyosuguliwa sana,hii huonyesha kuwa yeye ni hakimu anayehukumu kwa haki kwa mataifa yote,(Ufunuo1:15,19:15)
7.Sauti yake kama maji mengi,huonyesha nguvu zake katika kutoa hukumu kupitia neno lake,(Ufunuo1:15)
8.Nyota saba mkononi mwake,huonyesha malaika saba wa makanisa ambao ni watumishi wa hayo makanisa (Ufunuo1:16,20)
9.Vinara saba vya dhahabu,huonyesha hayo makanisa saba,(Ufunuo1:20)
10.Upanga mkali ukatao kuwili mkononi mwake,huonyesha neno lenye nguvu na uwezo linalotoka kinywani mwake(Ufunuo1:16)
11.Uso wake kama jua liking'aa kwa nguvu zake,huonyesha utukufu wa hali ya juu alionao kristo na ataonekana hivyo katika umilele wake.
12.Andiko hili la Ufunuo1:18 linadhihirisha kuwa Yesu anamnyang'anya shetani mamlaka yote.1 Yohana3:8,1Korintho15:20-26,Luka 10:7-19
Mawasiliano
+255784570700
+255622573146
+255675691700
NDUGU MSOMAJI WANGU NIKUKUMBUSHE TU KUWA KUMCHA MUNGU NI CHANZO CHA MAARIFA,MTAFUTE SANA MUNGU ILI UWE NA AMANI.
YOU ARE READING
SIFA 12 ZA YESU KRISTO KATIKA UFUNUO WA YOHANA
SpiritualHapa utaweza kuelewa kile ambacho Yohana alifunuliwa kwa Habari ya MWONEKANO WA YESU KRISTO