A.KUKUA KIROHO
Kukua kiroho ni pamoja na kuongezeka katika usafi au utakatifu,Ishara ya kukua kiroho ni (Tunda la Roho),Galatia5:22-23,Pia kukua kiroho ni kukua kimafundisho,kulijua Neno la Mungu na kuwa na uwezo wa kupambanua roho na kutochukuliwa na kila Elimu au maarifa ya Ulimwengu huu.
>>Kanisa likikua kiroho itaweza kupambanua roho 1Yohana4:1-2,halitaamini kila roho.
B.KUKUA KIIDADI
Kanisa la Kristo ni lile amabalo kila siku watu wanaongezeka,Matendo2:47,Hii ni kwa sababu kuna uhai wa kimungu na Nguvu za Mungu zinazotembea ndani yake.C.UMOJA
Sifa nyingine Muhimu sana ya kanisa la Kristo ni umoja,Yohana17:11,21,Yesu alijenga kanisa lenye Umoja.>>Kusiwe na mafarakano kati ya mwamini na mwamini,mtumishi na Mtumishi mwingine,na kati ya usharika mmoja na mwingine.
Dalili ya kuwepo kwa shetani katika Kanisa lolote ni mafarakano na Ugomvi,tena ni dalili ya watu wa mwilini,1Korintho1:10
D.NGUVU ZA ROHO MTAKATIFU
Sifa nyingine ya kanisa la Kristo ni kujaa nguvu za Roho mtakatifu,Roho mtakatifu ndiye nguvu ya kanisa la kwelila Yesu kristo.Matendo1:8,Luka24:49.
YOU ARE READING
KANISA LA KRISTO NA MTAZAMO WAKE
SpiritualKUJUA ASILI YA KANISA PAMOJA NA MTAZAMO WA WATU JUU YA KANISA