1.USIKU

39 0 0
                                    


SAA MBILI USIKU,

Upepo ulivuma ukitokea baharini na Hawa alikimbilia mahala upepo ulipokuwa ukivuma na mwisho alijikuta yuko bandarini.Akili yake ilimwambia kuwa  "kama atasafiri usiku huo basis ataikimbia mikono ya Mustafa."

Hali ya hewa ya bandarini ilikuwa yenye upepo na baridi kali. Kwenye kingo za bahari Hawa aliona meli na boti zilizotia nanga huku abiria  wakiendelea kuingia ndani ya boti ,matingo nao wakibeba mizigo ya abiria na kuwaingizia ndani ya boti. Hawa alinyoosha moja kwa  moja mpaka kwenye kibanda cha simu aliingia ndani na kufunga mlango.Kibanda hicho kilikuwa mbali kidogo na mahala meli na boti zilipotia nanga.

Hawa alimbeba mtoto wake wa kike mgongoni  aliyekuwa na umri wa miaka minne.Mkononi mwake alishika fuko la nailoni na ndani ya fuko hilo alijaza nguo zale ; dela ,baibui nyeusi na nikabu .Pia ,alibeba nguo  za mwanae na bila kusahau alibeba kofia ya mumewe Mustafa .Uso wake ulikuwa na makovu ya majeraha kama vile alipigwa makofi au ngumi usoni.Nywele zake zilitibuka kama mwendawazimu na hakujali.Siku hiyo hakufikiria hata kuvaa nikabu au baibui badala yak .Miguu yake ilijaa vumbi na hata kandambili zake pia zilikuwa papa na nguru
.

Siku hiyo ,Hawa,alionekana tofauti kabisa .Majasho yakimwagika usoni na mengine kuteremka mpaka mashavuni .Pia,Hawa binti mwenye rangi ya maji kunde na nywele za kiarabu ; alikuwa akihema kwa nguvu na kila alipojitahidi kuzuia kuhema alishindwa .

Ndani ya mfuko wake a nailoni alitoa karatasi iliyokuwa na namba za simu.Baadaye alitoa sarafu ya mia mbili na kuidumbukiza kwenye mashine.Hawa alianza kusoma namba zile za kwenye karatasi na kuzinakili kwenye ile simu ya kibandani kwa kubofya .Baada ya kumaliza ,simu upande wa pili ilianza kuita.Simu ile haikupokelewa mpaka kukatika.

"Nini tena jamani ?.." alijisemea kwa ghadhabu.Macho yake yalitizama nje ya kibanda na kwa mbali aliona gari aliyokuwa akifahamu sana ikingia bandarini .Vinyweleo vilisimama na midadi ya kukimbia ilianza kumpanda.Hawa alijizuia na kuongeza juhudi kwa kuandika namba ile tena na tena ,haraka kwa haraka huku akitumia nguvu nyingi . Hatimaye simu iliita tena upande wa pili.

"Pokea simu..pokea simu..." aliomba huku macho yake yakiwa nje kutizama kama aliokuwa akiwakimbia wako njiani kumjia. Maombi yake yalisikika na simu upande wa pili ilipokelewa.

"Halo...halo....nani mwenzagu ?."sauti ya mvuto ya kike iliongea .
"Hawa .."
"Enhee niambie .Za huko kwema kweli ?."
"Kwema tu ."
"Aya niambie kulikoni na usiku wote huu kunipigia simu."
"Nakuja ."
"Wapi ..Dar au ?."
"Ndiyo,niko bandarini."
"Sasa utapajuaje huku ?.."
"Nipe ramani ."
"Kwani simu umepoteza ?."
"Sina simu ."
"Huna simu ?..mbona hiyo kazi sasa ."
"Sina muda wa kutosha Stela ,ebu niambie unapoishi mimi nitafika."
"Si una fedha za kutosha ?."
"Ndiyo."
"Sasa ukishuka chukua taksi ikulete mpaka Magomeni mapipa.Ukifika omba simu na unipigie nitakufuata au kumtuma mtu akufuate."
"Sawa." simu ilikatika na Hawa alinyanyua mfuko wake na kutoka nje ya kibanda.Nje kulikuwa na kundi la wasafiri waliokuwa wakielekea botini.Hawa alinamisha kichwa chake ,akatoa kofia mfukoni na kuivaa kisha kujichanganya na umati ule.Watu waliovalia suti nyeusi na miwani waliendelea kumfuata kwa nyuma ,Hawa alishashtukia.Hawa aliendelea kuakaza mwendo na mbele yake aliona boti ambayo alitakiwa kuipanda.

"Ndugu abiria wa boti ya Unguja M.V ,boti yetu itaondoka baada ya dakika kumi .Tunaomba muingie ndani ya boti .." Hawa alisikia tangazo hilo lilitolewa kwa kipaza sauti .Wale watu nyuma waliokuwa wakimfuatilia walishindwa kumtambua kutokana na umati uliokuwepo bandarini.Mwisho alifanikiwa kuingia ndani ya boti .Muda wote aliinamisha kichwa chini huku akihesabu vidole vya mkono wake mpaka sitini.Alijua kama atahesabu mara kumi basi mlango utafungwa na boti itaanza kuondoka .Mahesabu yake yalitimia baada ya mara saba ;mlango wa boti ulifungwa na ilianza kutembea.

Hawa alielekea kwenye chumba ambacho alitegemea kukiona kiti chake kilichokuwa kimeandikwa kutokana na tiketi.

"01Jk." alijikumbusha namba ya kiti .Pole pole alianza kukitafuta kiti chake.Hawa alipita kila mstari akitizama nyuma ya viti kulikoandikwa namba na herufi ya kiti husika.

"00Jk ...hiki hapa." Hawa alifika kwenye kiti chake.Ajabu ni kuwa alimkuta mtu ameketi kwenye kiti chake.Mtu huyo alikuwa mwanaume wa rika lake ;miaka thelathini .Kichwa cha mwanaume yule kiliegemea kiti na gazeti lilimfunika usoni.Hawa alifikiri yawezakana yule mwanaume alipitiwa na usingizi.

Pembeni ya mwanaume yule kulikuwa na mfuko aina ya brufkesi uliokuwa pembeni ya miguu yake.

"Yani tangu niingie hapa nimemkuta amelala tu . "Hawa aliambiwa na bibi kizee aliyekuwa ameketi karibu .
" Kaka samahani..hivi unanisikia ?..umekaa kwenye kiti changu."Hawa alimwambia .Mwamaume yule hakushtuka wala kunyanyuka alibakia vilevile.Hawa alihisi yawezekana zile zilikuwa dharau.Hasira ilimpanda na kujikuta amepayuka kwa nguvu ,

"We mkaka inamaana hunisikii au ?..nyie wanaume mbona mnadharau sana ..mbona mnaninyanyasa sana." Abiria wote waligeuka na kumtizama.Hakuna aliyemuelewa ila yapo mengi yaliyomsibu Hawa na hata kusema yote yale.

Hawa kwa hasira alimshika na kuanza kumtingisha.Ajabu no kuwa mikono ya mwanaume yule ilikuwa yenye ubaridi usio wa kawaida.Hawa alistaajabu na aliponyanyua mkono wa Julia wa mwanaume yule aliona ukiwa hauna nguvu .Na pale alipouachia ulianguka pasipo kujizuia .Hawa alichanganyikiwa na nadharia mbaya ilimjia kichwani.Hawa alitoa gazeti kwenye uso wa mwanaume yule na kupigwa na bumbuwazi tena.Kifua cha mwanaume yule haikuwa kikipanda na kushuka na pia hakuona mwanauem yule akivuta na kutoa hewa nje.Hawa alijikuta akisema kwa mshangao ..

"Amekufa au ?.."
"Nani amekufa ?..." sauti nyengine aliisikia ikimpinga.

You've reached the end of published parts.

⏰ Last updated: Mar 18, 2019 ⏰

Add this story to your Library to get notified about new parts!

MALAIKA WA MCHANA ,SHETANI WA USIKUWhere stories live. Discover now