Mababiyoo68
*USHAURI KUHUSU MAMBO MBALIMBALI KATIKA MAISHA*
*1. Huwezi kubadili namna watu walivyokutendea mpaka ubadili namna unavyowatendea.*
Matayo 7:12;
"Basi yote myatakayo mtendewe na watu, nanyi watendeeni vivyo hivyo; maana hiyo ndiyo Torati na Manabii."
*2. Huwezi kubadili tabia mpaka ubadili marafiki.*
1Wakorintho 15:33
"Msidanganyike; Mazungumzo mabaya huharibu tabia njema."
*3. Huwezi kubadili ulichovuna mpaka ubadili ulichokipanda.*
Wagalatia 6:7;
"Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi; kwa kuwa chochote apandacho mtu, ndicho atakachovuna."
*4. Huwezi kubadili mwelekeo wa maisha yako mpaka ubadili dereva.*
Kutoka 23:1-3;
"Msivumishe habari za uongo; usishirikiane na mwovu kwa kuwa shahidi wa uongo.
Usiwafuate walio wengi katika kutenda uovu; wala usitie ushahidi wako katika neno lolote kwa kugeukia kando na kuandamana na mkutano ili kupotosha hukumu; wala usimpendelee mtu mnyonge katika neno lake".
Maisha yako yaweza ongozwa na mkumbo wa watu au MSIMAMO wako BINAFSI kwa UNACHOKIAMINI.
*5. Huwezi kubadili hali yako ya kifedha mpaka ubadili tabia yako ya kifedha.*
Mithali 21:17;
Mtu apendaye anasa atakuwa maskini; yeyote apendaye mvinyo, kula na manukato hatakuwa tajiri."
Mtindo wa maisha ya ufukara ndiyo busara kwa wengi.
*6. Huwezi kunibadili mpaka ujibadili mwenyewe.*
Matayo 7:3-5.
"Basi, mbona wakitazama kibanzi kilicho ndani ya jicho la ndugu yako, na boriti iliyo ndani ya jicho lako mwenyewe huioni? Au utamwambiaje nduguyo, Niache nikitoe kibanzi katika jicho lako; na kumbe! Mna boriti ndani ya jicho lako mwenyewe? Mnafiki wewe, itoe kwanza ile boriti katika jicho lako mwenyewe; ndipo utakapoona vema kukitoa kile kibanzi katika jicho la ndugu