hamisi
1 story
USHAURI KATIKA MAISHA by Mababiyoo68
Mababiyoo68
  • WpView
    Reads 12
  • WpVote
    Votes 0
  • WpPart
    Parts 1
*USHAURI KUHUSU MAMBO MBALIMBALI KATIKA MAISHA* *1. Huwezi kubadili namna watu walivyokutendea mpaka ubadili namna unavyowatendea.​* Matayo 7:12; "Basi yote myatakayo mtendewe na watu, nanyi watendeeni vivyo hivyo; maana hiyo ndiyo Torati na Manabii." *​2. Huwezi kubadili tabia mpaka ubadili marafiki.​* 1Wakorintho 15:33 "Msidanganyike; Mazungumzo mabaya huharibu tabia njema." *​3. Huwezi kubadili ulichovuna mpaka ubadili ulichokipanda.​* Wagalatia 6:7; "Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi; kwa kuwa chochote apandacho mtu, ndicho atakachovuna." *​4. Huwezi kubadili mwelekeo wa maisha yako mpaka ubadili dereva.​* Kutoka 23:1-3; "Msivumishe habari za uongo; usishirikiane na mwovu kwa kuwa shahidi wa uongo. Usiwafuate walio wengi katika kutenda uovu; wala usitie ushahidi wako katika neno lolote kwa kugeukia kando na kuandamana na mkutano ili kupotosha hukumu; wala usimpendelee mtu mnyonge katika neno lake". Maisha yako yaweza ongozwa na mkumbo wa watu au ​MSIMAMO​ wako ​BINAFSI​ kwa ​UNACHOKIAMINI.​ *​5. Huwezi kubadili hali yako ya kifedha mpaka ubadili tabia yako ya kifedha.​* Mithali 21:17; Mtu apendaye anasa atakuwa maskini; yeyote apendaye mvinyo, kula na manukato hatakuwa tajiri." ​Mtindo wa maisha ya ufukara ndiyo busara kwa wengi.​ *​6. Huwezi kunibadili mpaka ujibadili mwenyewe.​* Matayo 7:3-5. "Basi, mbona wakitazama kibanzi kilicho ndani ya jicho la ndugu yako, na boriti iliyo ndani ya jicho lako mwenyewe huioni? Au utamwambiaje nduguyo, Niache nikitoe kibanzi katika jicho lako; na kumbe! Mna boriti ndani ya jicho lako mwenyewe? Mnafiki wewe, itoe kwanza ile boriti katika jicho lako mwenyewe; ndipo utakapoona vema kukitoa kile kibanzi katika jicho la ndugu