We've updated our Content Guidelines.
Review the latest guidelines to keep sharing stories safely.

Hadithi Stories

Refine by tag:
hadithi
hadithi

7 Stories

  • MOYO ULIYO KATAA MAPENZI  by mwana2026
    mwana2026
    • WpView
      Reads 18
    • WpPart
      Parts 1
    Amina alikuwa msichana ambaye moyo wake haujawahi kuguswa na mapenzi. Uzuri wake uliwatesa wanaume wengi kijijini, lakini hakuna hata mmoja aliyewahi kuvunja ukuta wa moyo wake. Alikataa wachumba matajiri. Alikataa waliotoka mjini. Alikataa wote. Aliamini mapenzi si yake. Mpaka siku moja... Akiwa mtoni, alikutana na kijana mgeni mwenye majeraha mwilini na macho yaliyojaa hofu. Kijana anayesema anafuatiliwa. Kijana ambaye hakuwa na jina, wala historia. Na kwa mara ya kwanza... moyo wa Amina ulianza kupiga kwa sababu ya mwanaume. Lakini kumsaidia kunamaanisha kuleta hatari nyumbani kwao. Watu wasiojulikana wanaanza kumtafuta kijijini. Siri zinaanza kufunuka. Na mapenzi yanaanza kuota katikati ya hofu. Je, Amina ataweza kulinda familia yake? Je, atavunja ahadi yake ya kutojitoa kwa mwanaume? Na huyo kijana ni nani hasa - mwathirika... au mwanzo wa matatizo makubwa? Huu ni upendo wa polepole unaozaliwa kwenye kivuli cha hatari. Na wakati mwingine, moyo unaochagua kupenda huchagua pia kuumia. 🏷️ HASHTAGS #Mapenzi #SwahiliStory #Romance #Mystery #Drama #LoveAndDanger #HadithiYaKijijini
  • Jirani Yangu Tajiri by wandezmogire
    wandezmogire
    • WpView
      Reads 47
    • WpPart
      Parts 2
    Kitabu cha nyimbo na mashairi
  • simulizi za kusisimua  by dadasimulizi-
    dadasimulizi-
    • WpView
      Reads 63
    • WpPart
      Parts 2
    Ni usiku wa saa sita... simu ya ajabu inapigwa kwa namba isiyojulikana. Dada mmoja anapokea akidhani ni rafiki, kumbe ni mwanzo wa safari ya siri, hofu na mapenzi yasiyoelezeka. Kila ukurasa unafichua jambo jipya, na kila sura inakuacha na swali jipya: Je, utakuwa na ujasiri wa kuendelea kusoma hadi mwisho?
  • THE TARGET by hancyabdon
    hancyabdon
    • WpView
      Reads 27
    • WpPart
      Parts 2
    Ni mwaka wa uchaguzi wa rais, wananchi wanampenda rais wao mpaka vyama pinzani lakini viongozi wenzake baadhi wanakutana kwa ajili ya kupanga kumuua ndipo wanapokubaliana kumtumia mtu hatari aliyefungwa gereza lililopo kisiwani,wanapanga mpango wa kumtorosha ili aje afanye hiyo kazi huku wakikubaliana kuwa hakimaliza wamuue na yeye ndipo wanapomtumia binti mmoja ambaye ni miss tanzania kwa wakati huo kwa ajili ya kufanya kazi hiyo lakini mambo yanabadirika unajua kinatokea nini.......... fuatilia kisa hiki sitokuanguashaa katika kazi hii..😋😋😋
  • Siri ya Bega la Kushoto by stanjwm
    stanjwm
    • WpView
      Reads 180
    • WpPart
      Parts 7
    Kuzaliwa kwake kulisimamisha sherehe na kuleta ukimya mzito kijijini Nyarongo. Kwenye bega lake la kushoto, alama ya ajabu ya mistari mitatu iliyopinda nyekundu imechorwa, alama ya kipekee ya urithi ambayo haijaonekana tangu enzi za babu mkuu wa ukoo, Mzee Mwamba. Matosi, kijana anayekua akibeba siri hii nzito asiyoielewa, anajikuta katikati ya mfululizo wa matukio ya kimiujiza, uwezo asiouelewa, na hatari zinazomwandama bila yeye kujua sababu. Kuanzia udongo wa kijiji chake hadi kwenye harakati za kutafuta maisha katika ulimwengu mpya wa 'Jiji la Faraja', Matosi anagundua kuwa hawezi kuikimbia damu yake. Lazima afumbue fumbo la alama yake kabla nguvu zisizoonekana zinazoisaka siri hiyo hazijamfikia. Je, kovu hili la urithi ni laana inayomwangamiza, au ni ukombozi wa maisha yake? "Siri ya Bega la Kushoto" ni riwaya ya kusisimua iliyojaa taharuki, inayochanganya uhalisia wa mapambano ya maisha, saikolojia, na siri nzito zilizofichwa. (Sura mpya zinaongezwa kila wiki!)
  • KIU YA MILELE(Mpenzi wa Giza) by Deelove1
    Deelove1
    • WpView
      Reads 66
    • WpPart
      Parts 2
    Kwa karne nyingi, Mfalme Iryad mwenye macho ya damu ameishi katika gereza la giza na upweke, akiamini moyo wake ulikufa siku Jihan, malkia wa dhahabu, alipopotea katika dimbwi la kifo. ​Lakini giza halidumu milele. ​Katikati ya utupu huo, anatokea Laila; binti mwenye macho ya zambarau anayekuja kama nuru mpya, akianza kuponya vidonda vya kale na kufanya moyo wa mfalme huyu mnyama udunde tena. ​Hata hivyo, wakati Iryad akijaribu kumpenda Laila, kivuli cha zamani kinafufuka. Jihan anarudi kutoka kuzimu! Malkia wa dhahabu anakuja kudai kiti chake cha enzi na moyo wa Iryad. ​Je, Iryad atachagua nini? Nuru ya Laila inayompa amani sasa, au Moto wa Jihan uliompa utukufu zamani? ​Hii ni vita ya mioyo, nguvu za giza, na kiu ambayo haitatulia mpaka damu imwagike.