stanjwm
Kuzaliwa kwake kulisimamisha sherehe na kuleta ukimya mzito kijijini Nyarongo. Kwenye bega lake la kushoto, alama ya ajabu ya mistari mitatu iliyopinda nyekundu imechorwa, alama ya kipekee ya urithi ambayo haijaonekana tangu enzi za babu mkuu wa ukoo, Mzee Mwamba.
Matosi, kijana anayekua akibeba siri hii nzito asiyoielewa, anajikuta katikati ya mfululizo wa matukio ya kimiujiza, uwezo asiouelewa, na hatari zinazomwandama bila yeye kujua sababu. Kuanzia udongo wa kijiji chake hadi kwenye harakati za kutafuta maisha katika ulimwengu mpya wa 'Jiji la Faraja', Matosi anagundua kuwa hawezi kuikimbia damu yake. Lazima afumbue fumbo la alama yake kabla nguvu zisizoonekana zinazoisaka siri hiyo hazijamfikia.
Je, kovu hili la urithi ni laana inayomwangamiza, au ni ukombozi wa maisha yake?
"Siri ya Bega la Kushoto" ni riwaya ya kusisimua iliyojaa taharuki, inayochanganya uhalisia wa mapambano ya maisha, saikolojia, na siri nzito zilizofichwa.
(Sura mpya zinaongezwa kila wiki!)