Mtanzi ambaye ni Kiongozi wa Takia na mgombea kiti cha uongozi cha Takia anaonyeshwa kama kiongozi aliyejaa udhalimu, majivuno, kiburi, na ukatili. Harakati za kumng'atua uongozini zinaanza Lakini pia wale wanaopania kufanya vile haijulikani Hulka yao itakavyobadilika pindi watakavyopata kitu kile. Kutokana na hilo, Mariko Sipondi anazuumu kujitosa siasani asijue mengi mabaya atakayokumbana nayo. Licha ya ujasiri wake, wengi waliokuea na nia kama yake ni waoga sana wasioweza Kujitokeza waziwazi kwa kuogopa ghadhabu za Mtanzi.
Mariko, kinyume na ilivyoagizwa auawe, anapelekwa mafichoni na Mhazili, na hapo ndipo vita vya ukombozi vilipoanza.
Mhazili tu ndiye aliye na ujasiri tosha kwenda kinyume na Mtanzi. Ujasiri huu unafufua azma ya wanaharakati kama Karisa na wanapoaungana na kung'amua kuwa lazima wakomeshe uongozi ulio dhalimu, ndipo Takia inapata nuru gizani.
Kisa hiki kimejaa Uhondo wa kila aina anzia visanga, Mapenzi, usaliti, na ukarimu. Inafafanua kwa kina jinsi ujasiri unavyoweza kutuepua toka mikono ya viongozi madikteta.