7 parts Complete Hii ni riwaya inayomhusu Mzee Moja ambaye anajinyima starehe,tangu miaka yake ya ubaroro,na kulimbikiza mbegu anayoipanda katika biashara za kujianika juani.
Anapomaliza shule ya msingi,anajiingiza katika biashara ya rejareja,kuuza bidhaa katika kituo cha daladala mjini.
Anajinyima, wakati mwingi hata chakula, na hatimaye kumudu,kwa bidii zake za mchwa,na kundura za Mola,kujenga himaya kubwa ya kibiashara.
Himaya inayotamabaza mizizi katika nyanja mbalimbali za kiuchumi.
Mzee Moja anapata jina lake kwa kusisistizia watu kuwa;mja anahitaji mlo mmoja tu!kwa siku,ili kuishi na kuwa na afya.
Ni hadithi ya kuchochea na kuwatia shime waliozaliwa katika mazingira duni,au kukumbana na majanga maishani,kuwa "Haba na haba hujaza kibaba"
Kuwa penye nia,na njia ipapo hapo!
ONYO
Majina yanayotumika katika riwaya hii ni ya kimajazi na ya kubuni,wala hayawakilishi watu maalum katika maisha.
Naomba radhi iwapo kutatokea sadfa ya mfanano.