1 part Ongoing Hatupotezi watu ghafla kama taa inapozima wakati umeme unapa katika, inafanyika kwa wakati na awamu. Japo mara nyingu huja kuyaona matokeo na si mlolongo ulio pelekea matokeo.
Ile hofu wa kumuona baba amerudi mikono mitupu bila kamfuko chenye nguo za skukuu na kesho ndio skukuu yenyewe,ama ule uoga wa kutazama kulia na kushoto bila kumuona mama na upo kati kati ya umati wa watu sokoni hivi ni vitu ambavyo mtoto vina mstua moyo kama jinsi ambavyo mtu mzima anapo soma habari ya maafa ya tetemeko la Ardhi kwenye eneo la analo ishi mtu amoendae na sim inaita hapokei.. .
Sononi ya kuagana na rafiki zako ulio kua nao pale unapo hama mtaa, sononi ya kutazama matokeo ya mwisho na uone umefeli, sononi ya kujua kua mpenzi wako ame kusaliti, sononi ya kumuona mtu unae mpenda akiwa na mtu mwingine, sononi ya kutofikia ndoto zako iko so real
Kila mmoja ana yakwake anayo pitia hataka si yote basi moja amesha pitia ila mengi tubapitia na pengine wengine wana pitia kwa sababu yetu
Huwezi kufahamu ni maumivu ama furaha kiasi gani unasababisha kwa mtu kwa sababu mara zote tume kua tuki chagu yalio bora kwetu na si bora kwa ulimwengu,, na hii ndio tafsiri ninayo dhani mahusiano ya ki binadamu hufafanuliwa na walio wengi kua tunahitaji kilicho bora kwetu na si kutoa kiricho bora.
Lile kumbato unalo toa ukiwa hauhisi chochote inawezekana unae mkumbatia kumbato hilo hilo likaka a kwa zaidi ya miaka 30, lile neno la kawaida kwako ulilo mwambia mtu kama utani ama kwa kuto kutilia maanani pengine ni neno la kuvunja kabisa moyo wake au kustawisha mbegu ambayo inaenda kumtesa.
Siku zote hufanyika pole pole...
Umbali unao tembe na mtu unapimwa na vituo mlivyo simama kati ya safari sababu hata mkitaka hatua zenu hazita lingana na hii ndio hata askari hutembea sawa kwenye gwaride na hupishana wanapo tekeleza walicho fundishwa kwenye gwaride..