Neema alikuwa chumbani anajiandaa atoke baada ya kumaliza hekaheka za harusi ya Bilal alitaka a force mazingira kwa namna yoyote ile ajue file ambalo amelisaka miaka yote hiyo lilikuwa wapi. Kabla hajatoka aliingia Ramadhani chumbani na kumshika mkono kisha akamkalisha kitandani, Neema akiwa anashangaa shangaa Rama alimkabidhi faili ambalo alikuwa akilitafuta miaka yote mikononi mwake. " Rama" aliita Neema akimshangaa " ndio ni mimi, naona isiwe kero, ulimwengu wa MAFIA ni mkubwa sana na mgumu mno ku deal nao, hili file si ndo file ambalo baba mkwe wako amekuwa akitafuta miaka yote si ndio?" Neema alishtuka baada ya kusoma ujumbe uliokuwa umechorwa juu ya file hilo. 'MAFIA SECRETS' ndio faili lenyewe ambalo miaka yote katika hiyo nyumba kalisaka katika chemba zote za nyumba lakini hakuwahi kulipata. Neema alitabasamu baada ya kulishika na ilibaki kidogo alifungue. " huna haki ya kufungua hilo file, mwenye haki nalo ni yule mtu aliekutuma hapa" Neema alijua wazi kwamba hakuna kitu ambacho Rama hakuwa anajua wakati huo. Rama alikuwa ameshajua kila kitu ndo maana alimkabidhi file, lakini kwa nini amkabidhi faaili ki rahisi hivyo? Neema aliinua uso wake kumtazama " najua unafahamu kila kuhusu mimi sasa Ramadhani Shabogi the Mafia Don. Lakini kwa nini umenikabidhi file kwa urahisi hivi, unapanga kufanya nini juu yangu?" Alihoji Neema akijiwa na wasiwasi " mhh hahaha! Hahaha aah! Nilidhani huna akili kumbe kweli huna, kama ningetaka kufanya jambo kwako si ningefanya tangh zamani, sina haja ya kufanya jambo lolote lile kwako mimi. Ndo maana nimekupatia file uondoke kwa amani umpelekee huyo Boss wako sijui baba mkwe wako alafu kitu kingine ni kwamba kaa mbali sana na mtoto wangu kwa sababu, sitaki ajihusishe kwa namna yoyote ile na haya mambo ya ki MAFIA " aliongea Rama Neema akatabasamu " Anha kumbe ndio maana unamlinda ki binadamu si ndio? Lakini yeye ni mtoto wa MAFIA damu ta MAFIA Don inatembea ndani yake unadhani atabaki msafi na mtakatifu milele ?"All Rights Reserved