Kijana Ngeleja katika dimbwi la madhila mazito , moyo wake umejaa matundu kwa pigo la kuwapoteza wazazi wake wawili , kunajisiwa kwa mdogo wake aitwaye " Nyanjige ". Kwa mwenendo huu wa dunia , anauvua unyoofu wa moyo na kugeuka na kujiingiza kwenye uhalifu pale Mkoani Mwanza . Hana tone la huruma , anatumia mkono wake wa kushoto vizuri kuwapumzisha watu ambao wanakaidi huruma ya dunia kwa kujichunia mali , kupitia kauli yake ya 'Do or DIE' , yaani aidha ufanye au ufe . Mwili wake umejaa makovu ya visu na siafu yote hayajali , anachojali ni kuipendezesha na kuifurahisha nafsi yake . Hakuna marefu yasiyo na ncha anauvua utu huu mbaya , anafanya biashara na anajenga familia , anamuoa Bi. Hajra na wanapata mtoto wa kiume aitwaye Hamza kwa jina la kumbukizi la rafiki yake kipenzi , ambae anafariki katika umri wa miaka 11 , anapata jeraha moyoni mwake. Jeraha ili linajaribu kupozwa baada ya mkewe Bi. Hajra kupata uzao wa mtoto wa kike aitwaye Harshan ............................. Ili kupata udambu zaidi wa simulizi hii ya kusisimua , fuatilia mkasa huu .
More details