wakati mti unakua kuelekea juu ndivyo unavyokua kuelekea chini, na kukua huku kwa jina lingine tunaweza kuita kukomaa kwa mizizi. Taabu inayowapata wafanyakazi ya kung'oa mti ni kuhakikisha hawabakishi kisiki chini ya ardhi inamaana kuondoa mzizi wote. Miaka kumi ya ndoa si jambo rahisi kuifikia. Na ndoa iliyofika umri huu hapana shaka kuwa imekomaa na imekwepa mishale mingi. Maumivu na furaha yote ni mambo ya kawaida kwenye ndoa hii, hakuna jipya. Kuisambaratisha ndoa ya namna hii, nafananisha zoezi hili sawa na kung'oa mti ulikuwa na kukomaa miaka kumi. Lakini inaweza kazi hii ikawa nyepesi kama kuchuma mchicha shambani.. Naam inaweza kuwa nyepesiAll Rights Reserved
1 part