Peter ni binadamu ambaye alikuwa haelewi maisha yake aliumbwa kwa ajili gani na kwa nini alikuwa duniani.Kifo cha mpenzi wake wa siku nyingi siku ya harusi yao ndicho kilichokuwa kikimtia wazimu na kumfanya ajisikie upweke mkubwa katika maisha yake.Hakuruhusu moyo wake upende tena na hili liliwapa wakati mgumu sana kina dada kuingia katika mahusiano ya ki mapenzi na Peter.Baada ya miaka mingi sana Peter anagundua kifo cha mpenzi wake kilipangwa na watu asiowajua na kifo hichi kilimfungilia njia nyingi sana ambazo zilimsaidia kutafuta ukweli.Je ni nani aliyepanga kifo cha mpenzi wake? ni nini hatma ya Peter baada ya kujua hivyo?