3 parts Ongoing "........mama kusema kweli hata mimi sijijui ni nani na wala sikujui wewe ni nani, ila nahisi Kama vile mtu mnae dai kuwa ni mimi namfahamu........."
Moyo mpya ni simulizi inayohusu tukio la ajabu ama tuseme sililoelezeka baada ya tetemeko kubwa la ardhi kutokea. Wanafunzi Hans na Kamala wakawa ni miongoni mwa wahanga wa janga hilo, Kamala ni kijana wa wazazi matajiri na anakipaji cha kucheza mpira lakini anatabia za ugomvi, dharau japo pia anasumbuliwa na tatizo la moyo na anahitaji kubadilishiwa moyo, na Hans ni kijana wa wazazi wenye uwezo wa kawaida kifedha kiasi kwamba sio kila kitu wanaweza kumtimizia kijana wao lakini Hans anakipaji kizuri cha uchoraji na ni kijana mpole na mstaarabu ila kwenye tetemeko kwa bahati mbaya Hans alifariki lakini Kamala alibahatika kubaki hai licha ya tatizo lake la ugonjwa wa moyo kuzidi kuwa mbaya na mpaka madaktari wakapendekeza abadilishiwe moyo, swala lililowahusisha wazazi wa Hans kuombwa kumtumia mwanao kuokoa maisha ya wengne wanaopigania maisha.
Kamala anapata bahati ya kufanyiwa upasuaji wa moyo na kubadilishiwa kuwekewa wa Hans, lakini baada ya upasuaji Kamala anabadilika kuanzia matendo mpaka tabia kiasi cha kushangaza kila mtu aliyekua anamjua.
Swali ni je, Kamala alibaki kua Kamala, ama ndani ya Kamala kulikua na nafsi ya mtu mwingine?. Sababu ya Kamala kubadilika ni nini na ilikuaje akabadilika ghafla kiasi kile?.