NGUZO NNE ZA MOYO WA MWANAUME
I WAFALME 2:1-4
UTANGULIZI
Katika mwaka 1555, Hugh Latimer na Nicholas Ridley walitoka gerezani kwa mara ya mwisho. Walihukumiwa mauti kwa kuchomwa moto kwa sababu walikataa kumkana Yesu Kristo na kukataa Imani yao katika Kristo. Walipokaribia motoni, Latimer alimwambia Ridley “Furahini, Ridley simama kiume. Leo tutahakisha taa hakuna mtu atakaye zima, kwa neema ya Mungu”. Latimer alikuwa amesoma hayo kutoka kwa mfalme Daudi (V.2).
Leo tujifunze juu ya jukumu nne za mwanaume. Hapo mwanzo Mungu alimuumba (Mwanzo 2:7). Mungu alimpa Adamu jukumu (v.15) kulima na kutunza. “zaeni mkaongezeke, mkaijaze nchi na kutiisha, mkatawale” (Dominion) (Mwanzo 1:28). Onyo (Mwanzo 2:17) Adamu aliangusha mwanadamu, hivyo mwanaume amekuwa katika kuangaika tangu siku hio.Tutazame nguzo nne za moyo wa mwanaume:-
I. KIONGOZI WA JAMII– KIONGOZI (Leader)
Mungu alimuumba mwanaume kuwa kiongozi na mwenye kutuza nyumba yake (leader,provider)
Kuwa kiongozi ni kuona mbali. Tumeitwa kuwa kiongozi wa nafsi, jamii, uma na dunia.
Kwanza– Jiongoze mwenyewe.
Mfalme Daudi alikuwa kiongozi wa wengi, lakini siku moja alirudi nyumbani kukuta adui amefanya shambulizi (I samweli 30)
Samweli 30:6- “Daudi alijitia nguvu katika Bwana Mungu wake”
Daudi alirudi ndani yake mwenyewe, kukutana na Mungu, kujidhibiti mwenyewe.
Serikali iliyekubwa zaidi nikujiongoza, yaani jishide-ushinde.
Yesu Kristo kiongozi mwema alikuwa na wakati wa utulivu, kuomba na kufunga saumu.
Kila mwanaume mkristo lazima kujiuliza;
i)Je, kuna dhambi ya kuungama katika maisha yangu?
ii)Je, kuna watu wa kuwasamehe, hau kuwaomba msamaha etc.
Tumeitwa kuongoza jamii zetu.
Tumeitwa kutoshelesha jamii zetu, chakula, mavazi, hisia na roho.
Wanaume wawili katika Biblia walikuwa viongozi wa watu lakini wakashidwa na jamii.
Daudi– mfalme, jemedari, mwandishi, msherati, muuaji– lakini Daudi alishindwa na jamii yake ( I Wafalme 1:5-6)
Eli- (I Sam.2:22-25) Alipoteza usemi juu ya wanaye.
Lakini Joshua Jemedari alikuwa kiongozi mwema (Yoshua 24:14-15)
II. SHUJAA WA VITA (Warrior)
Katika kila mwanaume kuna mtu shujaa wa vita.
Lazima kupigania jamii yako kutoka kwa adui.
Abrahamu alikuwa shujaa wa vita, alikuwa na jeshi la watu 318 (Mwanzo 14:1-6)
Daudi aliua Goliathi, simba na dubu. (I Sam.34:17-51)
Yoshua alizunguka Yeriko (Yoshua 6)
Kalebu akiwa na miaka 85 alipigana na wana wa Anaki (Yoshua 14:6-14)
Nehemiah alijenga kuta za yerusalemu, mkono moja kijiko, mkono wa pili upanga (Nehe.4:16-18)
Stephano alimhubiri Kristo katikati ya watu waliokuwa adui wa msalaba– akauliwa kwa mawe, akamuona Kristo amesimama (Matendo 6:8, 7:60)
Wanaume– tumeitwa kusimama vitani (I petro 5:8-9)
Heshima yako, jamii, ndoa, watoto na Kanisa zimo katika hatari (2 Wakorintho 10:3-5)
Tumeitwa kuwapenda wake wetu (Waefeso 5:25, Zab 112:1-2)
III. MWALIMU- (Mentor)
Mwalimu wa kufundisha wengine maisha.
Paulo alikuwa na Timotheo (2 Tim.2:2)
Sulemani naye aliandika (Mithali 3:1-4)
Wanaume wanahitaji kuelewa na mambo.
Kuna mama wanao simamia nyumba zao bila mme, hawa watoto wanahitaji waalimu.
IV. RAFIKI MWEMA (Friend) Mwanzo 2:18
Mungu alituumba tukatosheleze, kupigania, kufundisha na kuunganisha watu katika urafiki mwema.
Tunahitaji kuungana na wanaume wengine katika urafiki wa kiroho.
Wanaume wengi hawana marafiki wa karibu– hivyo upweke upo.
Wanaume ni watu wa siri– Lakini tunapofungua mioyo– tunakuta hatupo peke yetu. Hofu, kukosa usalama– Jonathan na Daudi walikuwa marafiki.
Panapo urafiki pako na hakikisho, upendo na kuhesabika (Mithali 17:17, warumi 15:7, Mithali 18:24)
Mamlaka– Authority- (Mithali 27:5-6) Mhubiri 4:10.
Yesu Kristo ndiye kiongozi, shujaa wa vita, mwalimu na rafiki wetu.
MWISHO
Kuwa mwanaume:
Yashike mausia ya Bwana (Observe)
Uende katika njia za Bwana (Walk)
Ushike sheria zake, amri zake, hukumu zake na shuhuda zake (Keep)
Hivyo ndivyo utapata ahadi za Mungu.
Kiongozi mwenye upendo, shujaa mwenye hekima, mwalimu anayebandilisha wengine vyema na rafiki mwaminifu– Mwanaume.
Mawasiliano
+255784570700
+255622573146
+255675691700
Mtume Mwl Amos Ngosha
DU LIEST GERADE
NGUZO MUHIMU ZA MOYO WA MWANAUME
SpirituellesZITAMBUE TABIA ZILIZOJAA KATIKA MOYO WA MWANAUME