JUMAPILI (Kamala)

49 7 3
                                    

Jina langu ni Kamala, sijui nina shida gani, sielewi kama ni tatizo la kiroho, au la kuhitaji daktari, au ni mimi mwenyewe ndio najichangaya na ujinga wangu, ila sijielewi kabisa, najihisi niko kwenye mwili tofauti, hakuna anae weza kunielewa nikimuelezea hali hii, leo nimejaribu kumuambia mama na matokeo yake kampigia baba na sasa hivi nipo hospitali kukutana na Dr. Masasi japo mama hajaridhia.

Saivi ni Jumapili usiku majira ya saa tano kasoro, mvua za manyunyu zimetawala na hali ya hewa sio nzuri kabisa, nikisema hali ya hewa simaanishi maswala ya upepo wala joto ila namaanisha hali ya nafsi za watu, kwanza ukimya umetawala utazani hakuna dalili za uhai humu ndani, au wenda ndivyo namna watu wanavyokuwa wakiwa hospitalini?, mmmmmh sijui!, kwenye ghorofa tuliyopo, tupo sisi peke yetu na Kila mmoja anamgogoro wake na hakuna anaetaka kuongea kitu, ila unajua ni nini mimi ninachowaza?, ninahisi ukimya wote huu na migogoro ya nafsi ndani ya watu hawa, yote ni Kwa sababu yangu mimi, kiasi kwamba natetemeka ndani Kwa ndani, naogopa lakini nimeyaacha macho yangu yazungumze, namuona kabisa mama amejaa hasira japo hataki kuongea ila anazunguka tu ndani kwenda na kurudi hataki kukaa, baba hajui cha kufanya amekaa kwenye sofa huku anagonganisha magoti lakini mawazo hayamuishi hasa akimuona mama anavyotembea nenda rudi, kaka yangu Joel ndio kabisaaaaaaaaa amekaa tuli kama hayupo, sijui ndivyo ilivyo siku zote watu wakiona kama Kuna jambo linataka kulipuka?.

Alafu Kuna mimi ambaye ndio natembea kwenda chumba jirani nilipoelekezwa kumuona daktari, ni mwendo mfupi tu kama hatua saba au nane lakini macho ya hawa watu jamani ntadondoka kwa kweli, wanavyonitazama nauona mwendo mrefu Kama hatua mia ivi, moyo unadunda maana najua kabisa ninakoenda, naenda kuhojiwa vitu nisivyojua majibu yake na pengine nayajua ila sijui nitajibuje nieleweke.
Huuuuuuuuuuuh hatimaye nimefika mlangoni ila mbona kama kitasa chenyewe kigumu hiki au ndio kibovu?, heeeeee hatimaye umefunguka, Ndani namuona Dr. Masasi ambaye peke yake ndiye anayeonekana mwenye utulivu, alafu anaonekana mkarimu au tuseme ndio kazi yake, kaniomba niketi na niwe huru ila natamani angemalizia nijiskie niko nyumabani, kiukweli chumba chenyewe kinashawishi hali ya utulivu maana kidogo nimeanza kuuhisi uhuru kweli, au wenda nahisi kuna uhuru Kwa sababu najisikia kulala maana nimechoka balaa mtu asikuambie!.
Dr. Masasi naona ananitazama tu, utazani ananijua au kama vile anataka kunisoma akili ya ninachowaza saivi, na mimi macho yangu kwenye meza, nimetulia nasubiri kuambiwa cha kufanya tu. Alafu nimesahau kumsalimia na yeye kaniwahi

"Kamala hujambo?"
"Sijambo"

"Mambo yanaendaje lakini?"
"Kawaida tu"

"Kamala mi naomba uirudie kauli uliyomwambia mama yako na mi niisikie kama hutojali"
"Mi nilimuambia mama kiukweli hata mimi sijijui ni nani na wala simjui yeye ni nani japo mtu wanae niita kua ni mimi nahisi namjua na yupo kwenye kumbukumbu zangu"

"Kwa nini ulihisi umjibu hivyo mama yako?"
""Mama alikua anaongea Kwa hisia na nikaona kama anataka tuongee uhalisia ndio akawa ananiambia amenimisi sana, na hata ukorofi wangu pengine ulikuwa unamkera lakini hajaniona nikiwa hivyo kama vile nimebadilika mno, Kwa hiyo na mimi nikajaribu kumjibu tu uhalisia wa vile nilivyokua najisikia ila sio Kwa nia mbaya na wala yeye hakuichukulia vibaya"

"Lakini si unaelewa Kwa nini baba yako kakuleta apa, na wala sisi hatuna Nia mbaya si ndio?"
"Yah naelewa"

"Bas Kamala kama unaelewa Kwa nini upo hapa muda huu na Kwa..........

Muda huo daktari ananisemesha mimi nahisi kama kuna kinachoendelea nje ya mlango wa chumba cha daktari, namsikia mama kama anafoka na Kwa mbali ,sauti ya Joel naisikia Kama anamsemesha mama. Kumbe mama alikuwa alikua anasubiri niingie ndani Kwa daktari alafu yeye ndio akiwashe kule, muda wote mimi nipo na daktari mama alikuwa na hasira na baba Kwa sababu baba ndiye aliyenileta huku.

Mama Kamala (Sophia) ;
"Hivi Msangi kwani hujui Kama mtoto ametoka kwenye operation wikimbili zilizopita?, na hata kama unahisi mtoto anashida na anapaswa kumuona daktari kwani akisubiri kesho asubuhi au mchana muda mzuri amesha pumzika amekula akili inawaza vizuri Kwani atakufa?"

MOYO MPYAWhere stories live. Discover now