Jumanne (Hospitali)

16 1 0
                                    

Baada ya Jumatatu nzito ambapo Dr. Masasi, mzee Msangi na mchungaji kujitahidi kutafuta ni wapi pa kuanzia kumsaidia kijana wao Kamala, basi waliongozana tena na kuelewana wakutane hospitali ya Arusha Lutheran hospital ili kukutana na daktari aliyehusika na matibabu ya Kamala. Yote haya ni Kwa ajili ya kujua chanzo cha Kamala kupoteza kumbukumbu na namna ya kumsaidia ama kama sio tatizo la kuhitaji daktari ijulikane njia nyingine itakayokua nzuri kumsaidia.
Jumanne iliyochangamka basi imechangamka na wahusika wake baada ya mzee Msangi, Dr. Masasi na mchungaji kukutana hospitali kama walivyoelezana awali, moja Kwa moja ikawa ni kumtafuta Dr. Benjamin ambaye ndiye daktari aliyehusika na matibabu ya Kamala kabla ya Kamala kupelekwa kufanya upandikizaji ya moyo.

Dr. Masasi: "Dr. Benjamin eeeeee?"

Dr. Benjamin: "Naam ndio mimi, karibuni ofisini mnaweza mkaketi......(mzee Msangi, mchungaji na Dr. Masasi wakaketi)........kwanza poleni Kwa yote yanayoendelea."

Wote: "Asante"

Mzee Msangi: "Dr. Benjamin, (Dr. Benjamin anatikisa kichwa kuitikia) mimi nina mwanangu anaitwa Kamala na kama wiki mbili zilizopita mwanangu alikuwa hapa kipindi cha tetemeko la ardhi kutokea, na sasa hivi anapata nafuu baada ya upandikizaji wa moyo lakini ni kumbukumbu tu ndio zimekua mtihani Kwa mwanangu, daktari wake wa transplant alisema mambo kama hayo hutokea hivyo tuwe wavumilivu kwenye hali yake ila mimi nipo hapa leo ili kupata mwanga kidogo nini kiliendelea siku hio mwanangu alipofikishwa hapa."

Dr. Benjamin: "bwana Msangi bana ni kweli mwanao aliletwa hapa..........

******sauti ya Dr. Benjamin*******

......siku ya Jumapili jion, ilikua sasa ni baada ya tetemeko la ardhi kutokea, kusema kweli mvurugano na kurupushani zilikuwa nyingi hapa hospitali lakini wagonjwa mahututi walikuwa wachache akiwemo Kamala, Kamala alikuwa kwenye hali mbaya sana na asingewahishwa pengine tusinge kuwa tunaongea haya sasa hivi, shida kubwa iliyokuwa imemkuta kijana wetu  ni 'heart valve disorder' ambapo vali za moyo zilikuwa na hitirafu kubwa kiasi kwamba zilikuwa zinaharibu mtiririko mzima wa damu zinazoingia na kutoka kwenye moyo, na Kwa sababu hospitali yetu haina wabobezi kwenye kupandikiza moyo hivyo tuliamua kumfanyia ukarabati wa vali za moyo na kumpa dawa za kutuliza presha ya damu kwenye moyo, wakati huo huo Kuna mgonjwa pia aliletwa kutoka shule ya Mt. Constantine na Kwa bahati mbaya kijana huyo ubongo wake haukua hai japo moyo ulikuwa bado mzima, jambo hili likikuwa la kusikitisha sana, lakini ni Kwa upande mwingine ilikuwa ni bahati kijana kamala aliyekuwa akihitaji donor wa moyo, Kwa taratibu zetu tukaona ni vyema tukimsaidia Kamala kupata moyo wa upandikizaji kabla hajapelekwa Dar es salaam hospitali ya Muhimbili kufanyiwa upandikizaji, wazazi wa kijana yule ambaye taarifa zake haziwezi kuanikwa Kwa wengine, waliitwa pembeni na mkuu wa idara ya wagonjwa mahututi baada ya taarifa ya kufariki Kwa mwanao na mkuu wa idara ya wagonjwa mahututi alifanya kuwaomba wazazi wale kama wataridhia kumtumia mwanao kuokoa mwaisha ya vijana wengine wanaopigania uhai wao Kwa kusubiri upandikizaji wa viungo, haikuwa rahisi kusema kweli, na hii ni Kwa yeyote ambaye angekua kwenye nafasi ile, mkuu wa idara ya wagonjwa mahututi alijitahidi mno kuwashawishi na mwisho wa siku wazazi wale waliridhia Kwa moyo mmoja na hapo ndipo tulipata uhakika wa Kamala kwenda Dar es salaam hospitali ya Muhimbili kufanyiwa upandikizaji wa moyo maana 'donor' wake alikuwa amesha patikana, maandalizi ya usafirishaji na mapokezi ya mgonjwa na 'donor' wake yalifanyika kikamilifu lakini nakumbuka kabla hata ya kumpeleka Kamala kwenda kupanda ndege Kamala alipewa taarifa za kupata 'donor' atakae mchangia moyo, Kamala alifurahi na alishukuru mno japo ilikuwa Kwa uchungu maana alihisi maumivu ya kupoteza mtu ili yeye alishi, alilia sana na aliomba akatoe heshima zake za mwisho Kwa kijana yule aliyemchangia moyo, Mungu alivyo wa ajabu Kamala alikuta mtu yule aliyetokezwa kumchangia moyo ni kijana wa darasani kwao, muda huo Kamala alilia sana na aliomba na kusisitiza tumpishe, Kuna vitu vinatia uchungu sana, Kuna muda ndio unagundua ni kweli maisha hatuyapangi sisi Wandamu, pamoja na kulia sana Kamala alipata muda wake wa kutosha kama dakika ishirini hivi, na baada ya hapo alibebwa kwenye machela Kwa ajili ya kumsafirisha kwenda Kwa ajiri ya upandikizaji, wazazi wa kijana aliyemchangia moyo Kamala waliomba kumuona pia angalau kwa mbali hata kama hawatopata nafasi ya kuwasiliana nae, na walimuona Kamala akiwa kwenye machela anapelekwa kwenye ndege kuwahishwa Kwa ajili ya upandikizaji wa moyo, hii ilikuwa ni jumapili ya masononeko makubwa sana, kila aliyeshuhudia kipande hiki lazima alitokwa na machozi, vijana wawili wanapigania maisha yao lakini mwisho wa siku mmoja ndio anabaki hai Kwa sababu ya mwenzake kumsaidia kiungo muhimu. Muda wote hata kwenye ndege nilikuwa na Kamala na tulifika nae Dar es salaam vizuri tu na tukamuwahisha hospitali ya Muhimbili, maandalizi na taratibu zote zilisimamiwa na kufanywa ipasavyo na upandikizaji ulifanikiwa baada ya masaa sita, kijana wetu Kamala alibaki kwenye hali ya kutojitambua Kwa masaa lakini Mungu alikuwa ni mwema na baada ya masaa ishirini na nne alirejea kwenye fahamu zake japo alikuwa na hali ya kumbukumbu zake kutokuwa sawa na hii imechangiwa sana na athari alizozipata wakati wa tetemeko la ardhi, japo kuwa ni tatizo la muda tu na ndani muda kadhaa kijana atarejesha kumbukumbu zake.

Mzee Msangi: "na vipi kama mwanangu anajifananisha kuwa yule kijana aliyemchangia moyo?"

Mchungaji: "eeeeee hapo ndo swali kuu maana tunataka kufahamu kama mambo kama hayo hutokea"

Dr. Benjamin: "oooooooh hilo tatizo litaka kufanana na ugonjwa unaitwa 'dissociative amnesia' Yan amnesia ya kujitenga........"

Dr. Masasi: "Dr. Benjamin apo ndipo nilitaka kuhakiki kama ni dissociative amnesia, ila kwani huu ugonjwa unaweza kumkuta kijana wa umri mdogo kama yule?"

Dr. Benjamin: "eeeeee inawezekana, sana sana hutokea kulingana na ajali anayopata mtu, majanga ya asili kama kuanguka kwenye tetemeko la ardhi nakadhalika, Kwa hiyo kijana wetu anaweza akawa kwenye kipindi cha ugonjwa huu au ndio unaanza Kwa hio matibabu sahihi na malezi chanya kulingana na anachotaka ndio yatamjengea na kumsaidia kupona, lakini atahitaji dawa hasa za kutuliza wasiwasi yan 'anxiety' pia kumsimulia habari zake na ikiwezekana kumsimulia pia kuhusu upande wa pili ambao ni wakijana aliyefariki ili aone tofauti, pia atahitaji familia na marafiki ambao watampa ushirikiano asikae kinyonge ambapo mnaweza kufanya nae vitu alivyokuwa anapenda kama mpira nakadhalika"

Mzee Msangi: "Dr. Benjamin hapo uliposemea kuhusu kumpa simulizi za upande wa pili, Kwangu mimi daktari naomba utusaidie tukutane pia ata na familia ya waliotusaidia mpaka tumeokoa maisha ya kijana wetu, nazani itasaidia vyema kumfanya ata Kamala mwenyewe kuona tofauti na kujua yeye ni nani"

Dr. Benjamin: "nimekuelewa mzee mwenzangu, nimekuelewa sana, ila muda mwingine tunafata tu taratibu zilizowekwa kua hakuna kudhihirisha taarifa za 'donors' wetu. Hapo Kwa kunisaidia labda ni utaandika barua ya kuwashukuru kupitia hospitali yetu na sisi tutawafikishia"

Dr. Masasi: "hio iko sawa, tupe anuani ya hapa na sisi tutawaandikia barua ya shukrani ili muwafikishie"

Mchungaji: "nazani ni vyema ukaiandika sasa hivi, na ata mahali pa kukutana nazani tufanye kwenye sehemu inayojulikana, pia itapendeza tukiwataarifu Kamala na mama yake kuwepo badala ya sisi kuzunguka wenyewe wakati mgonjwa tunaetaka kumsaidia hayupo."

Dr. Benjamin: "basi mkitoka apa mtazame kulia kwenu Kwa mbele Kuna wadada wengi wakihudumia mapokezi ya wagonjwa, basi hapohapo mnaweza kuomba karatasi ya barua na anuani"

Wote: "asante"

Mzee Msangi na wenzake wakanyanyuka na kutoka ofisini Kwa Dr. Benjamin kwenda kufata karatasi ya barua vilevile wakaelewana kesho kukutana na familia ya akina Hans maeneo ya kanisa la parokia ya mt. Agustino. Barua ilipokamilika iliwasilishwa hapo mapokezi na mapokezi waliifikisha Kwa wahusika.

Du hast das Ende der veröffentlichten Teile erreicht.

⏰ Letzte Aktualisierung: Jun 07 ⏰

Füge diese Geschichte zu deiner Bibliothek hinzu, um über neue Kapitel informiert zu werden!

MOYO MPYAWo Geschichten leben. Entdecke jetzt