Sehemu 1

13 1 0
                                    

Ni jumatatu asubuhi mida ya saa 11:30 alfajiri alarm ikaita. Ikasharia ni mda wa kuamka wa Maria ajiandae aende kazini kwa mara ya kwanza baada miaka miwili akiwa anatafuta kazi.
Aliamka kwa kujivuta kuelekea bafuni , akaoga na kupiga mswaki akajisafisha vizuri baadae akavaa nguo zake ambazo alizitenga tayari akajipaka na make up kidogo ili aweze kuvutia  alivyomaliza akajiangalia kweny kioo na kujihakikissha yupo sawa akatoka nje ya chumba akafunga akaondoka zake kuelekea kazini.
Maria alipata kazi katika kampuni ya Merio Electronics ambayo ni kubwa sana  ilikuwa  inashika nafasi ya 113 duniani katika mauzo yake ya mwaka uliopita.
Akiwa katika basi maria alikuwa anamawazo mengi sana aliwaza jinsi atakavyofanya kazi yake kwa ufanisi wa hali ya juu ili aweze kuajiriwa kwa muda mrefu na hata kuongezeka kwa kipato chake na kufikia ndoto zake za kuwa tajiri mkubwa duniani.
Alijisemea "nitafanikisha ,  nitafanikisha ndoto zangu"
basi lilifika katikati mwa jiji la salanda .jiji ambalo ni kubwa sana kama jiji la new york la marekani . Maria alishuka kutoka kweny basi na kuelekea kweny mjengo maridadi wa makao makuu  ya Merio electronics.
Alingia ndan ya mjengo na kuenda moja kwa  moja kwenye lift. Ndan ya jengo watu walikuwa wako bize mno  kila mtu alikuwa ana shughuli zake anafanya.
Lift ilipanda mpaka ghorofa ya 13 ambayo ofisi yake ilikuwepo . Alitoka nje ya lift na kuelekea moja kwa moja kweny ofisi yake ambayo alikuwa anashare na wafanyakaz wenzie watano na mkuu wao wa kitengo alikuwa anaofisi yake pembeni.
Aliingia ndani na kusalimiana na mfanyakazi mwenzie alimtangulia kufika. Alikuwa anaitwa Andre Jonas alikuwa Junior Accountant na ameajiriwa ndan ya Merio Miezi 8 iliyopita.
Wakat anafungua Kompyuta yake Andre akaja "maria karibu katika kitengo chetu"
"Hasante Mr jonas"
"Unajua kuwa hii ni kampuni kubwa sana na kitengo cha Accounting kinatakiwa kufanya maz kwa ufanisi wa hali ya juu"
"Ndio naelewa. Na ninaahidi nitafanya kazi kwa juhudi zangu zote ili kufikisha malengo ya kampuni"
"Ok maria acha tupige kazi"
Wakat anamalizia kuongea Juliana aliingia naye ni junior accountant ila ameajiriwa mwaka mmoja na nusu uliopita. Juliana alisalimia wafanya kaz wengine na kumkaribisha maria.
Mda wa saa 2 asubuhi wafanya kazi wote walikuwa washafika na boss wa kitengo Mrs Delmas alifika na kusema " habari zenu wapendwa"
"Salama mrs delmas"
"Natumaini mshamuona mfanyakazi wetu mpya Miss Maria Kermal atakuwa pamoja nasi kuanzia sasa, karibu miss maria"
Wafanya kazi wenzake wakapiga makofi kuashiria kumkaribisha.
Kazi zikaanza kazi yake ya kwanza ilikuwa ni kufanya forecast ya cost za project moja ambayo Mrs delmas alitaka iliawasilishe kweny mkutano wa bodi.
Mda ulisonga mpka mida ya saa 8 mchana wakat wafanya kazi wenzke walikuwa wamerudi kutoka lunch. Juliana akamuuliza maria "kazi inaonekana kubwa?" Huku akiijiegesha juu ya meza ya maria
"Ndio ni kubwa sana, Mrs delmas amesema anahitaji leo kwasababu kesho asubuhi inabidi awasilishe kweny mkutano wa bodi"
"Oh okay, fanya kwa ufanisi maana mtoto wa chairman hatak kusikia neno makosa"
"Mtoto wa chairman mhh ndo CEO wa Merio?"
"Yap ndio CEO baba ake alimwachia madaraka na kumpatia 75% ya share zake ndani ya Merio, alafu ni kijana tu anamiaka 26 tu "
"Namuona kwenye jarida la forbes alikuwa tajiri wa 134 duniani mwaka jana. Wali estmate assets zake zipo more than 8 billions USD "
"Ndio na kikubwa walichovutia ni umri wake ni mdogo sana na kuweza kuwa na utajiri wote huo"
"Ukiwa ndan ya familia tajiri haina haja ya umri kuwa tajiri"
" hahha na kweli, haya maria acha nikuache uamalizie kazi " huku juliana alikuwa akisogelea kompyuta yake
"Haya juliana acha nimalize kabla  ya saa 11 jioni"
Ilikwenda mpka saa 11 jion na maria aliweza kufanikikisha kazi yake na kuwasilisha kwa mrs delmas
Mrs delmas alimsifia na kusema " umeifanya vizuri na kuipanga kwa usahihi, excellent miss kermal excellent"
"Ohh hasante Mrs delmas "
Mrs delmas alipomaliza kuangalia kazi yake na akamruhusu maria kurudi ofisin kwake
Wakat anafika.ofisini andre na ferdnand wakamfuata maria, andre akmuuliza huk ferdnand akikaa kwenye meza  ya maria "vp boss kasemaje"
"Ameipenda kazi amesema ipo sawa"
Ferdanand akadaikia"lazima aipende mana umeifanya kwa ustadi sana na chuo ulichosoma kinatoa ustadi mkubwa sana"
huku maria akishtuka
" mhh umejuaje chuo nilichosomea"
Andre akajibu "fredy anajua file la wafanya kazi wengi hum kwasbab dem wake ni HR"
Maria akiwa kwa mshangao akajibu " ohh okay"
Andre akamuuliza maria huk akisogeza kiti chake karib na maria " inaonekana familia yen ina pesa mana chuo kile sio mchezo"
"Hapana andre nilienda kwa scholarship,mm nafamilia yang tunamaisha ya kawaida sana"
"Ohh ndo mana umefanya kaz kwa ufanisi katika siku yako kwa kwanza tu"
Frednand akadakia "she is very intelligent anaufaulu mkubwa sana"
Maria akaendelea "frednand unaonekan dem wak anakupa vitu vingi"
andre akajib" fred anampa vitu vizuri chumban lazima ampe siri nzito bila kujitambua anafanya makosa"
Jibu la andre liliwafanya wote wacheke na baad ya hapo maria alikuwa amemaliza kufunga kompyuta yake na kuwa tayari kurudi nyumban kwasbab mda wa kazi ulikuwa umeshaisha
Aliwaaga andre na frednand waliokuwa wamebaki pale ofisini.
Alivyofka kweny apartment yak aliyokuwa amepanga akaingia ndan nakuweka mkoba wake na kwenda jikon na kuanza kujityarisha chakula cha usiku maana mchana hakula.
Wakat anajitayarishia chakula sim yake iliingia meseji aliienda kuichukua mana ilikuwa kweny meza ya pemben na kuangalia kukuta meseji imetoka kwa rafiki yake Renata akimuuliza anaendeleaje na kazi kwa siku ya kwanza ilikuaje.
Maria alimjibu na kumwambia "yan imekuwa kama ndoto kwangu baada ya kila kampuni kunikataa kwasabab ya ile scandal.. ile scandal imeniharibia sana CV yang ila namshukuru mungu kwa kupata kaz hapa tena kampuni kubwa sana"
Renata akajib " mungu ashukuriwe , ila maria inabid ufanye kwa ufanisi kwasbab wamekukubal licha ya scandal hiy."
Maria "yan na mpka sasa sijajua imekuaje nikapata kaz licha ya ile scandal ..sijajua bado"
Renata "achana na hayo ..enhee niambie ulikutana na ex wako "
maria huku akizima jiko "hapana yy yupo ngaz ya juu kabisa siwez kuonana nae kirahisi. Speaking of my ex i think he knows kama nik pale au ndo yy aliyefanya manuva"
Renata " yupo ngaz ya juu kuajiri sio kazi yake ila uwez jua may be"
Maria " mhh may be ..okay renata have a nice night acha nile ..nijiandae na kesho"
Renata " ok maria good night"
Baada ya maongez hayo maria akaweka sim juu ya meza  na kujipakulia chakula ..baada ya kula akasafisha nyumba,akatayarisha nguo zake za kesho ..ilikuwa mida yaa saa 3 usiku alipomaliza vishughuli na kuamua kwenda kulala..
Asubuhi mida ya Saa 2 asubuhi Mrs delmas alifika ofisini na kumuita maria alimtaka aende nae kweny kikao since yeye ndo aliyetayarisha ile forecast atakua msaada wakat anaipresent
Alibeba vifaa muhim kwa ajjli ya mkutano wakat anatoka wafanya kaz wenzie walikuwa wanampa good luck na juliana alimwambia"una bahati siku ya pili ofisin umeshalikwa kikao cha bodi ..(una nyota kal ) akimwambia kwa kumnongoneza" maria akajibu "hasante" huku akiendelea kutayarisha files zake.
Wakatoka na mrs delmas mpka ghorofa ya 16 na kwenda mpka sehem ambapo kikao kinafanyika wakat wanakaribia kufika wakakutana na CEO Mr Martin Merio naye akielekea kwney chumba cha kikao. Moyo wa maria ulishtuka baada ya kumuona Martin
Mrs delmas alimsalimia Mr martin "how are you mr merio or young Mr Merio"
Martin akajibu " am fine mrs delmas how is you"
Mrs delmas akimgeukia maria " am good, ahh na huy ni mfanyakaz mpya tupo nae kitengo chetu anaitwa Miss Maria kermal"
Huku Martin akifurahi akampa mkono maria na maria akiwa bado yupo katika mshtuko alimpa mkono Martin na martin akasema "karib katika Merio electronics karib sana "
Maria akajibu " hasante mr CEO hasante " huk joto la mwil wake likizid kiwango

MariaWhere stories live. Discover now