MISS TANZANIA|SEHEMU 01

379 7 1
                                    

“Patrick amka basi darl inakaribia saa nne sasa”Alisema Veronika kwa sauti laini ya kubembeleza.

‘Mmmmhhh”Aliguna Patrick ,akajigeuza upande

wa pili na kulivuta zaidi shuka.

“Amka basi bwana uende ukaoge”Alizidi

kubembeleza Veronika

Kwa uchovu mwingi Patrick akaamka na

kunyoosha mikono yake juu huku akijipinda

“Loh !I’m veeery tired”Akasema kwa uchovu.

“lakini ukishaoga uchovu wote utaisha my

darling “Akadakia Vero.

Kwa uvivu Patrick akajiinua kitandani na

kuelekea bafuni .Dakika chache baadae alitoka

akiwa amechangamka.

‘Kweli maji ni dawa nzuri ya uchovu.Sasa

najisikia saafi kabisa.Nadhani itabidi kwa sasa

nipunguze muda wa kufanya kazi .Nimekuwa

nikifanya kazi kwa masaa mengi sana kwa siku

kiasi kwamba nakosa hata muda wa

kupumzika.naogopa tukija kuonana nisije kuwa

nashindwa kutimiza majukumu yangu kama

mume kwa sababu ya uchovu”

Vero akatabasamu halafu akatoa kicheko cha

chini chini na kusema

“Kweli mpenzi jitahidi kwa sasa kujaribu kupata

muda wa kutosha wa kupumzika.”

“Nitajitahidi baby”

Baada ya kuhakikisha sasa yuko safi Vero akamshika mkono Patrick na kumpeleka sebuleni kupata stafstahi.

“Patrick dear nataka unisindikize Supermarket nikafanye manunuzi ya vitu vya ndani .

   Si unajua kesho Andrew na vicktoria wameahidi

kututembelea”Alisema Veronika wakati

wakiendelea kupata chai.

“Mhh Vero we nenda tu mwenyewe mi niache

nipumzike bwana”Patrick akajibu

“jamani dear usifanye hivyo naomba bwana

unisindikize ,mi naona uvivu kwenda peke

yangu”

‘haya mama ,tumalize twende ili tuwahi kurudi”

“Nashukuru dear”

Katika vitu ambavyo Veronika alibarikiwa kuwa

navyo ni uwezo wake mkubwa wa kushawishi.

****************************************

**************************

Veronika Rugi alikuwa ni binti mrembo mwenye

mvuto wa aina yake.Binti huyu licha ya kujaaliwa kichwa kizuri chenye nywele laini ,nyingi na ndefu ,alikuwa na uso mpana wa mviringo ulionakshiwa na macho mapana

yenye kurembua muda wote.

Midomo mizuri ,laini ambayo akikupiga busu

hutatamani abanduke.Mtoto huyu alijaaliwa shingo murua ambayo iliungana na kiwiliwili

You've reached the end of published parts.

⏰ Last updated: Jan 18, 2015 ⏰

Add this story to your Library to get notified about new parts!

MISS TANZANIAWhere stories live. Discover now