Tangu siku hiyo,aliamua yeyote aliyehusika kwa njia yoyote katika kuharibu maisha yake atalipa kwa kifo.Alikuwa tayari ameua maajenti waliowatimua na kunadi vitu vyao vya nyumba,akamtafuta kijana yule aliyekejeli aila yake na kufanya afutwe kazi na kumtupa kisimani.Aliyekuwa amesalia ni Jane….
Ulikuwa unasema nini kuhusu hali ya kinyumbani na kikazi?”Jane alipiga funda la kileo cha Fighter,mkono wake wa kushoto pajani mwa Kazembe.
“Nilifutwa kazi katika kampuni niliyokuwa nikifanya kazi na sikulipwa hata senti.”Kazembe alisema na kumkazia Jane macho.
“Lini?”Jane aliuliza.Tayari kumbukumbu za mwaka wa 2008 zilikuwa zimeanza kumnyemelea na kumkaa akilini sawasawa lakini picha na tukio halisi haijamwigia kabisa.
“Kitambo kidogo.”
“Unaitwa nani kwanza?”
“Kazembe.”Jane aliwaza kwa muda na kung'amua kuwa halijui wala hajawahi kulisikia jina kama hilo.Asilojua ni kuwa Kazembe alipoenda kuchukua kitambulisho alitumia kitambulisho cha ajenti mmoja aliyemtoa roho kisha akaenda na kuhongana apewe kitambulisho pasi na kutoa cheti chake cha kuzaliwa.Aliwaongopea waliokuwa wakifanya shughuli hiyo na kusema kuwa anajua kila kitu kuhusu wazazi na mbari yake.Jina Kazembe alitumia la ajenti yule na kutupilia mbali jina lake halisi.
“Usijali.Mimi nitakupa kazi na donge nono la pesa.Lakini Lazima ufanye kitu fulani.Sahau yaliyopita.”
“Ninafahamu kitu chenyewe ni kipi.”
“Kitu gani vile?”“Kutimiza mahitaji yako ya kimwili.”
Jane aliingiwa na furaha manake
alikuwa tayari amependezwa na Kazembe.Kronometa yake ilisoma saa tano kasorobo.“Twende nyumbani kwangu.”
Wawili hawa waliondoka wakiwa wamezungushiana mikono viunoni.Mmoja anadhani usiku wa leo atakula raha huku mwingine akihisi kuridhika na kuwaza jinsi atakayotumia kumtesa mwenzake vizuri mpaka aage dunia.
Dereva wake alikuwa tayari ameshafika.Waliingja na kuketi kwenye viti vya nyuma na kubanana pamoja kana kwamba nafasi ilikuwa finyu.Walipiga soga na kupiga vikwakwa,wakabugia vileo na kuvuta sigara mpaka wakafika nyumbani kwa Jane……..
Itaendelea..
Mwandishi :Erick Ndungu/Matuko Weye
Follow me on Twitter @WeyeMatuko.
YOU ARE READING
KISASI
General Fiction......Alikuwa tayari ameua maajenti waliowatimua na kunadi vitu vyao vya nyumba,akamtafuta kijana yule aliyekejeli aila yake na kufanya afutwe kazi na kumtupa kisimani.Aliyekuwa amesalia ni Jane.... Anasa/Kisasi/Upendo