SURA YA KWANZA

11 1 0
                                    

Mantra citi si mji!

Mantra citi ni himaya ya kihuni.

Mantra citi ni himaya ya genge la walanguzi,waporaji na wauji.

Genge ambalo kama  minyiri ya pweza linashamili katika miji yote,nyanja zote za maisha na nchi zote duniani.

Kauli mbiu ikiwa,"PORA NIKUPORE TUPORANE"

Manta citi limeswahilishwa kutokana na msemo wa kimombo;

Mankind Transport Corridors.

Shughuli kuu za genge ili lililoshamiri na kuayaacha mashirika ya kijasusi yakijikuna vichwa;Ulanguzi wa binadamu kutoka taifa hadi lingine.

Mizigo yao mikuu ikiwa wanawake na wanaume wanaotumika kama watumwa wa kimapenzi.

Watoto wadogo husafirishwa kutumika katika mashamba ya maua na machimbo ya madini.

Wengine hubahatika na kuasiliwa na wakwasi wasiojaliwa watoto.

Kuna wengi ambao  hutumika katika ukahaba wa watoto.

Kuna wengi wanaotumika kama mifugo wanaobebezwa madawa ya kulevya matumboni mwao na kisha kuchinjwa na sehemu kama vile figo na maini kuuzwa katika soko haramu  la viungo vya miili binadamu.

Manta citi ina maajenti ambao ni madaktari tajika na wapasuaji wa maiti ili kufanikisha opereshoni zao.

Sio madaktari tu!

Kuna wahandisi,wanasiasa,wakuu wa vikosi vya usalama na hata viongozi wa mashirika ya kimataifa.

Mantra citi ni zimwi lisilokuwa  na kichwa ila mikono mingi mirefu.

Mithili ya gugu maji katika ziwa Victoria.

Mantra citi ni mji wenye vitongoji vingi duniani.

Kuna vinavyohusika na kusafirisha silaha kwa waasi ili kuviepusha vikosi vya usalama kuweza kuziba njia zao za biashara.

Biashara ya kishetani.

Mantra citi ni gugu maji ambalo vikosi vya kijasusi vimeshindwa kuling'oa.

Jinsi wanavyojitahidi kuliangamiza,ndivyo linavyozidi kuenea kwa kasi.

Waking'olea huku linamelea kule!

Viongozi wa mantra citi hayajulikani.

Wanachama ndio wengi kama mchanga wa bahari Hindi.

Shughuli za kufagia mchanga kabisa kutoka fuo za bahari zinaweza kuchukua takriban miongo mingapi?

***********************************************************************************************

Bakari ni mfanyibiashara tajika katika nchi ya Utope.

Anahusika na biashara ya "general merchandise"

Ni muuzaji wa chochote kinachoweza kuuzika!

Ana biashara katika nyanja zote za kiuchumi.

Sikwambii mohospitali,usafiri,kilimo,elimu,usalama,makaazi,utalii,hoteli,usagaji wa nafaka....

Taja tu nikwambie!

Usisahau ni mumiliki wa chama cha kisiasa na mwakilishi katika bunge la kitaifa.

Bunge kuu la Utope

Bakari ni ajenti mkuu wa mantra citi.

Wanachama wa Mantra citi huingia na kutoka nyumbani kwake,si mchana si usiku.

Na ana nyumba nyingi!

Ana wake wengi pia.

Watoto kuna wake na wengi wa kuasili.

MANTRA CITIWhere stories live. Discover now