Sura Ya Pili

4 1 0
                                    


Utopeni!

Mbona Utopeni?

Zama za kale nchi hii ilikuwa kisiwa kidogo mno katikati ya bahari ya Utope Mwekundu.

Bahari kubwa inayotumika na vyombo vya majini katika safari zao.

Kisiwa kilichotumika na walanguzi kufichia na kusafirisha bidhaa mbalimbali haramu haramia.

Ili kuwakabili walanguzi hawa,vyombo vya usalama wa kimaitaifa viliafikiana kwa kauli moja,kupindua mkondo wa bahari,ili kuweza kufikia na kuhangamiza kabisa kisiwa hiki.

Baada ya mbinu nyingi na muda mrefu walifanikiwa.

Wakayabeba maji mithili ya joka kuwa la baharini;bega kwa bega;sako kwa bako!

Maji yakasalim amri,ingawa shingo upande na kuelekea kwenye mto mkuu.

Pakabakia eneo kubwa petepevu lililojaa utope.

Utope uliozidi pindi mvua iliponyia.

Kwa kuwa walanguzi hawa walikuwa gugu lililokita mizizi katika nchi jirani,waasi kutokea pande za kaskazini walipigania na kufaulu kujitenga.

Kisiwa kikashikana na nchi kavu na kuundia nchi mpya ya Utopeni.

Utopeni ikawa ndio makao makuu ya Mantra Citi.

Nchi iliyojaa matope na utope si haba.

Usiseme ulanguzi,mauaji,utekaji nyara,mauaji ,ubakaji wa haki za kibinadamu!

Matope yalionatana na kuwachafua wote walioishi katika nchi hii.

Maadili yao yakachanganyika na utope yasitambulike

Matope wakachanganyikana na damu na kuacha uvundo duniani kote.

Matope yakawa nchi yenye rotuba lilikootea gugu la Mantra Citi.

Gugu lililoenea kwa kasi ya virusi vya hewani na kuiacha dunia ikitapatapa kwa kunyimwa hewa ya kupumulia.

Kupindua mkondo wa maji kulileta hasara ya kimazingira isiyogharamikika.

Viumbe wa majini wa kuelea na wa kuzamia waliangamia.

Mbuga za wanyama zilizotegemea maji haya ziliangamia kutokana na mafarakano kati ya wanyama na waja.

Misitu yenye chemichemi zilizochiririka chinichini kuokea baharini ilinyauka huku jangwa likijipanua na kuenea kwa kasi.

Ukame na njaa vikawa viamsha kinywa Utopeni na nchi nyingine jirani.

Kampuni ya Mantra Citi ikapata mwanya wa kuagizia vyakula na kutoa misaada ya kifedha kuzinusuru nchi husika.

Zimwi likazimeza nchi hizi kizimakizima bila kuzitafuna.

Zimwi likazikaba koo asasi zote za utawala.

Kutema mate zisiweze,kutema pia isiwezekane.

Kutokana na umaskini uliozikumba nchi hizi na zingine duniani,kampuni ikaanzisha miradi ya magenge ya vijana.

Magenge ambayo yalikuwa kucha kali za kukwaruzia iwapo mtu yeyote angejaribu kupinga au kuingilia shughuli za kampuni.

Maajenti kama vile Bakari wakapata bidhaa za kusafirishia ughaibuni kwenda kujipatia maisha mubadala na yenye matumaini.

Nyumba za kuwahifadhia watoto mayatima zikawa ndio njia mwafaka ya kulangulia watoto.

Mantra Citi ikawa ndio sheria na sheria ikawa ndiyo Mantra Citi.

***********************************************************************************************

Kichinjio kikubwa cha  nyama ya punda na pundamilia kilifunguliwa Utopeni.

Nyama iliyopakiwa kwa mifuko maalum na kusafirishwa kwenda nchi za Asia ,hasa Uchina.

Mkurugenzi wa kiwanda hiki alijulikana kama Chimantra.

Alikuwa jamaa mfupi wa mviringo asijulikane mgongo u wapi,wala tumbo li wapi?

Kwa umali alionekana kama kipira kikubwa cha soka.

Jamaa mkali kama shubiri .

Wafanyikazi walimuogopa kama radi .

Kwake uaminifu na kuhifadhi siri za uchinjaji wake kilikuwa kipimio cha kupata au kutopata kazi huku.

Kichinjio hiki kilikuwa katikati mwa uwanda mkuwa uliozungukwa na kinamasi chenye utope telezi.

Vijia maalum vya kuingilia na kutokea vilitengenezwa kwa vyuma, vilivyotengeneza daraja za juu kwa juu.

Baadhi ya madaraja haya yalikuwa ni reli za juu kwa juu

Hakukuwa na njia mbadala ya kupenyea ila kuruka kwa kutumia ndege.

Uwanja mdogo wa ndege  ulijitandaza kama mkeka juu ya jumba kuu na pana;chini yake maofisi na magala yasiohesabika.

Ndege zilitumika na wenye kiwanda,viongozi na wageni mashuhuli.

Licha ya kutofikika,ulinzi mkali ulikiangazia kiwanda hiki 24/7.

Wafanyikazi wengi waliishi ndani mwa kiwanda.

Kutangamana na watu ilikuwa nadra kama machozi ya kobe;ama ukipenda mkojo wa jogoo.

Siri za kazi zao walizizika kaurini.

Wengi wao wakiwa barobaro wanachama wa magenge utopeni.

Walilishwa kiapo pamoja na kutishiwa kuchinjwa mithili ya punda pundamilia waliowachinja.

Mamaneja wote huku walikuwa nia wachina huku kazi za kipunda zikiwachiwa wanamatopeni.

Waliokaidi amri au kufa kwa ajari,walichinjwa na  kuzikwa utopeni pamoja na mizoga ya punda pundamilia.

Kilikuwa na kichinjio cha watu ja wanyama.

Nyama zilizofungwa kwa mifuko mieusi zilisafirishwa moja kwa moja hadi Asia kwa ndege,huku zingine zikisafirishwa hadi andarini kwa kutumia gari moshi.

Mabohari maalumu yalitumika kuzibebea nyama zenyewe.

Pindi nyama zikipakiwa hufungwa kabisa na kufunguliwa kwa vifaa maalum yawasilipo.

Maohari yaya haya yalitumika kulangulia wanadamu.

Tuseme mizigo ilitoka ikiwa ya nyama ila kuwasili ikiwa ya bidhaa mbalimbali.

Niamini nikikuambia miujiza ilifanyika njiani.

Mantra walikuwa na uwezo wa kufanya miujiza eti!











You've reached the end of published parts.

⏰ Last updated: Apr 24, 2023 ⏰

Add this story to your Library to get notified about new parts!

MANTRA CITIWhere stories live. Discover now