Je,ataniacha?(Sehemu ya 07)

3 1 1
                                        

Mwezi wa tano mwaka uliofwata Bob Ohm alijiunga na chuo kikuu cha ufundi cha Bumbe.
Bob akajiunga na chuo kile kama mwanafunzi wa somo la Kawi na elektroniki akifanya kitengo cha diploma, Bob akaanza maisha mapya kule chuoni.Baada ya miezi miwili Bob alimpenda mwanadada mmoja mrefu,mwemba na alikuwa mrembo pia.
Bob akamtongoza kwa muda mrefu bila kufua dafu. Mwezi mmoja baadaye wakakubaliana wakawa wapenzi. Cha kuhuzunisha ni kuwa mapenzi yao hayakudumu hata mwezi mmoja.
Je,nini kilifanyika?Ni swali msomaji unaweza kujiuliza sana.
Bob alipomuuliza yule mwanadada mbari yake ikawa kwamba wanatoka kwa mbari moja na yule mwanadada,hapo mahaba yakakufa.Bob akabaki kuchanganyikiwa sana asijue la kufanya.Akayachukia mapenzi kabisa.
Tena rafiki wake wa kiti cha kwanza akamtongoza huyo mwanadada wakapendana jambo lilomuumiza Bob. Hakuumia kwa sababu rafiki yake alimsaliti,la hasha!Bob alihisi vibaya kwa sababu alimpoteza msichana mzuri kwa sababu ya mila na desturi. Na rakiye Bob akamchukua. Cha kuumiza pia ni kuwa hadi washafanya tendo la ndoa pamoja nafasi ambayo ingekuwa yake Bob.
Bob akayachukia mahaba sana akajidharau sana.Bob mara nyingi angeonekana mnyonge sana. Kwani hakuelewe alikuwa na tatizo lipi.
Miezi minne baadaye, Bob akawa amepunguza mawazo mengi,akarudisha fahamu zake hisia 'zikafufuka'.
Bob alipokuwa akipitia mtandao wa Facebook akamkuta msichana mrembo. Msichana huyu sio mara ya kwanza kuonana na Bob.Washawahi kutana Bob akiwa shule ya Upili.
Bob akavutiwa na Uzuri wake akamwomba nafasi ya uchumba.Yule mwanadada hakukataa akamkubalia Bob wakapendana sana.Wakapanga mengi pamoja na mrembo huyu kwa jina la Shally.Hakika mwanadada huyu ni mrembo kupindukia.
Huyu ndio mwanadada ambaye Bob anashinda akitazama picha yake kwenye rununu yake.
Mwanadada alimwahidi Bob kumpenda na kuoana nae.Walikuwa mbali na mwingine.Shally yuko kule mjini Kisumu Kazini naye Bob yupo chuoni.Walikuwa wameahidiana kukutana Kisumu Siku tatu zijazo.
Bob alikaa pale chini ya mwembe kwa muda mrefu.Huku kaonekana mwenye hofu.
Hofu lake liliibua swali zito akilini mwake.
Swali hilo lilikuwa,"JE,ATANICHA?."
Muda wa kuanza masomo ya jioni ulikuwa umefika.Bob Ohm akanyanyuka na kuenda zake darasani.

JE,ATANIACHA?Where stories live. Discover now