IBADA ZA KANISA LA KRISTO

0 0 0
                                    

Jambo mojawapo muhimu sana mara mtu anapookoka ni IBADA,
>>Biblia inahimiza kuwa kila mtu wa Mungu asiache kukusanyika pamoja na wenzake,Ebrania10:25
•Ibada inatakiwa iwe desturi au tabia ya mtu wa Mungu wala siyo kitu cha kulazimishana ,kanisa la kwanza la Mitume lilikua na tabia au moyo wa Ibada.Matendo3:1-3,13:1-3.

Aina ya Ibada ambayo mtu anatakiwa kuwa nayo ni Ibada ya ROHO NA KWELI.

            MAANA YA IBADA
Ibada ni kumpa Mungu heshima inayostahili kwa sababu ya kustahili kwake.
•Ibada ni Heshima
>>>Kuabudu,ni shughuli ya kumwadhimisha Mungu katika Uwepo wake.

            
                 AINA ZA IBADA
Kuna aina mbili za ibada katika  sehemu ya Kanisa kwa ulimwengu huu,
1.IBADA YA LITURUJIA
2.IBADA HURU

1.IBADA YA LITURUJIA/ILIYOTUNGIWA UTARATIBU
-Hizi ni ibada ambazo mtu anaongozwa na kitabu ama sheria iliotungwa na wanadamu.

Na ibada hizi mara nyingi humzuia Roho mtakatifu kufanya kazi ndani ya kanisa kwani anakuwa amewekewa kikomo cha kutenda kazi.

2.IBADA HURU
Hii ni ibada ambayo inaongozwa na Roho mtakatifu kwa kupitia watu amabao hawako chini ya sheria ya kitabu cha dini kama mwongozo wa kufanya Ibada.Na katika ibada hii hakuna kitabu maalumu kwa ajili ya sala.

KANISA LA KRISTO NA MTAZAMO WAKETahanan ng mga kuwento. Tumuklas ngayon