NADHANI YEYE NDO ANAPANGA

26 3 1
                                    

                Utangulizi
"Nadhani yeye ndo anapanga" Ni wazo ambalo mara nyingi sana lilikua likimsumbua kijana Erick Marwa Maganya ambae kila alichokuwa akikipanga kwa namna moja au nyingind kilikuwa hakiende vile alivyotaka yeye. Ilifika hatua akataka kukata tamaa akiamini kuwa kama MUNGU ndie anapanga ni maisha gani waja wake waishi basi ni bora akae asubiri ikifika zamu yake atapewa fungu lake. Lakini akifikiria atakula nini aligundua aliwaza upumbavu.

Hi n hadithi ya kusisimua iliyojumuisha maisha yote anayoyapitia mwanadamu. Mitihani kama vile kusengenywa, kudharauliwa, mauaji, tamaa, na mambo mengne kama hayo. Pia vipindi vya furaha kama vile mafanikio, mapenzi, kujirusha havikuachwa mbali.
Nina uhakika kabisa utafurahi na hutajutia kupoteza muda wako kusoma hadithi hii ya kusisimua

Mwandishi Sunteh Marwa Machugu

SEHEMU YA KWANZA: SAFARI YA DAR ES SALAAM(Erick)

'Sikati tamaa' wimbo wa msanii Darassa wa Tanzania ndio ulikuwa unaimba kwenye simu ya abiria aliyekuwa amekaa siti ya nyuma yangu. Nikiwa nimekaa nikitafakari hali ya maisha nyumbani nilipokimbia na kutafakari nitaishije ugenini nakoelekea kulisababisha nisisikie sauti ya abiria mwenzangu akinisalimia. Kama mtu niliekuwa ndotoni nilikurupuka. "Eh eh"
"Nakusalimia kaka mambo?".
"Safi tu' huku nikipepesa macho kumtambua anaenisalimia.
Akaniuliza swali ambalo nilichelewa kujibu kwa kuduwaa kumtazama mtoto wa kike mnene mlefu ambae hata kwenye basi alitembea ameinama. Akiwa amevaa suruali ya jeans ya blue iliyomshka kisawasawa kwenye paja zake zlizojaa pande zote na kutengeneza umbile la mtungi. Huku juu amevaa shati nyeusi iliyokaa bomba. Kwa kweli nilivutiwa kumtazama. Sura yake ya mviringo yenye mashavu ya kuteleza na kichwani alinyoa kipara kitu ambacho kwetu Mara sikuwahi kuona. "Vipi kaka mbona uko katika hii hali". Nisijue cha kujibu kwa haraka nilijikuta namjibu "ni maisha tu dada yangu". Akakaa kwenye siti yake kisha akaniuliza. "Maisha yamefanyaje" nakumbuka nilichmjibu ni kwamba ni stori ndefu ambayo inahitaji utulivu na muda wa kutosha. Akaniahidi kwa kuwa wote tunaelekea Dar basi atatafuta muda nimsimulie kwani anashauku ya kujua ni nini hasa kilichoniweka katika ile hali. Kwa kijana wa miaka 22 kama mimi kuonekana kama mtu niliyekata tamaa na maisha ni dhahili kuwa nina mengi ya kusimulia. Gari ilianza safari ya kutoka katika kituo cha nyegezi ambacho hata hilo jina niliambiwa na makonda niliyowakuta kituo cha kwanza kiitwacho 'buzuruga' niliposhukia nikitoka Tarime Mara. Tulipotoka kituoni hapo mazugumzo yetu yakaanza. Aliniambia yeye anaitwa Janeth ni mkazi wa Dar anaishi na mama yake tu baba yake alifariki tangu akiwa na miaka kumi. Nikampa pole ya kumpoteza baba yake. Akaendelea kwa kusema.

"Mama yangu ni mjasilia mali anaemiliki saluni kadhaa jijini dar es salaam".
"Mimi ni mwanafunzi katika chuo kikuu cha dar es salaam kozi ya biashara".
Nikapata swali hapo hapo na kumuulza kama anaishi dar na anasoma Dar Mwanza anafanya nini?.
Akatabasamu kisha akanijibu kuwa Mwanza alikwenda kumtembelea shangazi yake ambae alimuomba kipindi chote cha likizo yake aimalizie nyumbani kwake mwanza.

Tuliendelea kufahamiana mpka tulipofika Singida ambapo gar ilisimama na tangazo likasikika likisema abilia wanaotaka kwenda maliwato na kupata chakula wafanye hivyo ndani ya nusu saa gar itaanza safari ten.
Janeth alinitaka twende pamoja tukapate chochote kwani tangua tometoka Mwanza, singida ilikuwa kituo cha kwanza kusimama kwa hiyo alidai njaa ilimuuma.
Nilitabasamu kwa aibu kwani tofauti na nauli nilotoka nayo kijijini sikuwa na akiba hata Tsh 100 kwenye mfuko. Tangu jana usiku nimeingia Mwanza nililala na walinzi buzuruga kituo cha mabasi mpaka asubuhi nikibana pesa ya nauli hata nishinde njaa.
Nilimueleza hayo yote akaniomba niongozane nae ataghalamia. Tukaongozana nae mpaka kwenye mgahawa mmoja amba kutokana na njaa sikukumbuka hata kusoma jina lake.

Tulipo maliza tulirudi kwenye basi safari ikaanza.
Nilikurupuka toka usingizini baada ya kusikia sauti ikiita kwa mbali "Erick Erick" nikiwa sijielewi nilibaki najifuta futa usoni kujiweka sawa.
"Tumefika ubungo kituo cha mabasi na huu ndo utakuwa mwisho wa safari yetu.

Tulishuka akaniomba nimsaidie kutoa mizigo kwenye 'boot'. Ilikua mishale ya saa 4 : 15 usiku ambapo niliendelea kushangaa taa kubwa zikitoa mwanga wa kutosha toka pande zote za kituo. Tulipanda daradara na safari ikaanza huku Janeth akinishawishi nifikie kwao nilimkatalia kwani niliamini mama yake asinge kubali kufikia kwake. Sifa ya mkoa wetu wa Mara kwa matukio ya kinyama ilisababisha nizidi kumkatalia aliniachia namba yake japo sikuwa hata na simt nilimuahidi nitaikariri. Alinipatia kiasi kidogo cha pesa kisha alipofika anapokwendj alishuka. Akiwa ananitazama kwa huruma huku akitabasamu daradara iliondoka tukamuacha akiwa anapanda bajaji. Msongo wa mawazo ulianza tena baada ya kuachana na binti yule mkarimu, mcheshi na muongeaji aliyeifanya safari yangu ya faraja mbali na matatizo nilokumbana nayo nilikotoka.

Idadi ya abiria ilizidi pungua kutuo hadi kituo mpaka ilipofikia hatua daradara ikasimma abiria wawili wa mwisho walishuka nikabaki mwenyewe nashangaa huku nimekikumbatia kibegi changu kidogo kama mkoba wa kutunzia hela alichokuja nacho baba toka Musoma mjini alipokuwa anafanya biashara ya kuuza mahindi aliyokuwa anayachukua toka vijiji mbali mbali. Kondakta aliniomba kushuka kwani kile kilikua kituo cha mwisho. Nilipepesa macho kulia na kushoto na kuamua kusonga mbele. Nikiwa natembea peke yangu barabarani huku simuoni mtu yeyote isipokuwa majumba marefu na mafupi pamoja na magari na pikipiki vikipishana huku na kule.

Mwendo wa mita miatatu(300m) kwa mbele kidogo niliwaona wanawake wakiwa wamesimama kando kando ya barabara wengi wao wakiwa wamevaa nguo fupi na za ajabu sikujali  Nilitabasamu kidogo nikiamini nitapata msaada kwani imani yangu ilinituma kuwa wanawake ndo watu wenye huruma.

Kabla sijawakarbia vizuri alinikimbilia mwanmke mmoja kabla hata sijamwambia shida zangu alianza kujithaminisha kwangu

"Mimi ndie Nay gwiji wa hii kazi nitazame juu mpaka chini hutaona kasoro". Nikiwa namtazama mtoto wa kike kweli kaumbika juu mpaka chini mweupe hana doa, miguu mizuri ikionekana ya kuteleza, nyuma kama kabeba kichuguu ama kweli alikuwa mzuri

"Sema tu kwa bei yoyote utapata huduma".

Nikatambua kuwa walikua pale wakifanya bishara ya kuuza miili yao huku nikishangaa! Kwa uzuri ule walikosa waume wa kuwaoa. Potelea mbali nikaona nimueleze shida yangu

"Nisikilize dada yangu, mimi hapa nimetoka kijijini mko wa Mara nimekuja Dar kutafuta maisha nimefika usiku huu sina pa kulala naomba kama unaweza nisaidia japo kwa usikuu mmoja tu nikiamka asubuhi nitajua cha kufanya

Yule dada alianza kupayuka
"We mjinga me nakuona mtu wa maana kumbe mkimbizi huna lolote. Kwanza nitolee hapa sura mbaya we unadhani Dar wanadumu omba omba kama wewe. Hebu nitokee huko usinichefue kwanza ushanitia mkosi mapema"
Vikasikika vicheko vya wenzake vilivyoniumiza. Kwa ile hali ilipelekea nikaanza kujuta kumkatalia Janeth kwenda nae kwao. Niliondoka kinyonge huku nikifikiria nitakavyoumaliza usiku...

Itaendelea jumanne ijayo

Has llegado al final de las partes publicadas.

⏰ Última actualización: Mar 26, 2018 ⏰

¡Añade esta historia a tu biblioteca para recibir notificaciones sobre nuevas partes!

NADHANI YEYE NDO ANAPANGADonde viven las historias. Descúbrelo ahora