part~4~

46 2 0
                                    

Karibu tena chukua kiti utulie hii part ni Kali mtuwangu.

~~~~~••♪•••~•••••~~~~~•••~~~~~~~~

Nilifanikiwa kuwajeruhi maafisa wa ulinzi kabla ya kufanikiwa kutoroka. Nilipowasili chengoni, nilimkuta mke wangu tayari ashadondoka chini. Damu zilikuwa zinamtoka mdomoni. Alionekana kubishana na muda hata nisingeweza kumsaidia. Tuliambiana buriani kisha akanikabidhi barua aliyokuwa nayo mkononi na kukata roho baada ya kushindwa kumalizia neno "I love yoo..."

Niliifungua barua na kuyapepesa macho yangu pasi kuamini. Hadi sasa ningali namtafuta daktari gwiji wa macho ili niwe na uhakika wa ninachokisoma. Ungana nami unisaidie kupata uhakika kuwa ninachokisomandicho kilichoandikwa

~~~~~~•~~~~~~~~~~•••••~~~~~~~~

Huzuni yote naielekeza kwako lazizi. Nafahamu fika kuwa itakua vigumu sana kuifuta taswira ya maisha yetu. Kifo changu kisiwe chanzo cha kuuzima mshumaa wako wa maisha. Niwie radhi mpenzi kwa kukuficha siri nyingi za maisha yangu. Lengo la barua hii si kukushawishi kunisamehe ila ningependa kukujuza nilichokifanya. Nimeamua kumpa mwanetu sumu ili angalau nimlinde katika ulimwengu huu wa wafu. Nafahamu wazo hili limekuvunja moyo kabisa ila utakaporudi jela mwanao hatakuwa na mtu wa kumsitiri....
~~~~~~•~~~~~•~~~~~

Nilikomea hapo na kukimbilia chumbani ili kuhakikisha kilichoandikwa. Nilimkuta mwanangu tayari kashaaga dunia. Taabu zilikua zimeniganda kama Lupe agandaavyo kwenye ngozi ya ng'ombe. Ama kweli adhaniaye kasimama aangalie asianguke. Simanzi zilinikaba za kwao nazo zikanipanda ila sikua na jinsi. Mara tu nilipokuwa nimejilaza chini machozi yananitoka kama maji bombani, kikosi cha mapolisi kikajitoma ndani kwa vishindo na kunitia pingu.

Nilifikishwa mahakamani na kufunguliwa mashtaka upya. Sikuruhusiwa kuhudhuria mazishi ya familia yangu. Akutendaye mtende usimche akutendaye. Hivyo basi napiga staghafiru kwa yale nitakayoyatenda. Naapa kutoisamehe serikali iwe hapa duniani au hata huko ahera. Natazamia kuwekwa huru siku mosi na iwapo nitawekwa huru, basi nitasababisha maafa makubwa katika dunia hii.

Huu ndo mwisho wa sinema. Huuuuuuu... Finaly am releasing you to the world of reality. Vote~vote my people if you enjoyed my story. Thanks for your   participation in my story.
✋✋✋✋✋✋bye~bye

You've reached the end of published parts.

⏰ Last updated: Feb 24, 2017 ⏰

Add this story to your Library to get notified about new parts!

KIFO HUKAA KWENYE MSHIPIWhere stories live. Discover now