part~2~

36 1 0
                                    

Karibu tena katika kipindi kingine cha tarehe yangu.

Nilifanya kazi hii kwa bidii ya duduvule agotaye gogo. Kwa kipindi kifupi nikakiletea kiwanda faida Mara dufu. Baada ya kugundua uwezo wangu mkubwa katika kazi hiyo,  niliamua kuomba uhamisho ili nirudi nchini mwangu kuhudumia viwanda vya huku. Lengo langu lilikua kuhakikisha viwanda vya nchi yangu vinapiga hatua.

Nilikumbana na upinzani mkali baada ya kuomba uhamisho. Nchi yangu ambayo nilidhani nilikua nikiisaidia ndo ikawa ya kwanza kunisaliti kwa kunionyesha udhalimu. Chanzo hasa cha upinzani huo no ufisadi. Serikali ilitaka viwanda viachwe mikononi mwao pasipo kufwatiliwa ili wapore mali ya mwananchi. Mwanzoni sikulichukulia swala la utata sana kwani nilifikiri no kawaida ya majembe yalimapo pamoja hayakosi kugongana.

Nilipingana vikali na serikali hata baada ya kunipa chauchau mara kadhaa. Kumbe ni heri kujikwaa kidole kuliko ulimi. Serikali ikaamua kunipotezea dira ya maisha kwa kunitia gerezani kwa madai ya kashfa. Nikahukumiwa kwa kuiba pesa za umma baada ya kushindwa kipigana na tembo.

Ama kweli chaka la simba halilali nguruwe. Mastakimu yangu na samani zinginezo zikauzwa ili kufidia madai niliyolimbikiziwa.

Ingawaje akili yangu haina tofauti na kichungi, bado haijawa sababu ya kutokuelezea kifungu hiki kifupi kinachofuata. Mke wangu Kaja kunitembelea gerezani kama kawaida yake ila siku hii alionekana kuwa na mushkil kwenye wajihi wake. Machozi yakaanza kumtoka alipoyaoteza macho yake kwangu na kugundua kwamba nilikuwa nimefahamu kuna tatizo.

Nini kilichokua kimemkuta mke wangu? Mwanetu alikua kaaga dunia ama? Sina ufahamu pia. Ungana Nami kwenye ukurasa ufwatao nikujuze. Shukran kwa kusoma ukurasa huu.

KIFO HUKAA KWENYE MSHIPIحيث تعيش القصص. اكتشف الآن