"Kazana tu, endelea kusukuma ana karibia kutoka jitahidi!jitahidi!! Sukuma"
Ili kuwa ni saa nane (8:00) za usiku mwezi ukiwa umeandama angani na kung'aa sana kwa siku hiyo. Sauti za wakunga zilisikika ziki mtia moyo mama mjamzito aliye kuwa akijifungua huku akilia kwa uchungu na maumivu makali yasiyo simulika wala kuelezeka, ila kwamtu aliye kwisha jifungua anajua maumivu hayo. Maumivu yalikuwa makali sana kwa mama huyu kwani ilikuwa ndiyo Mara yake ya kwanza kujifungua.
Baada ya maumivu makali sauti zilisikika za katoto kadogo kakilia kuashiria tayari mama yule kajifungua.
"Hongera Dada"
"Asante sana, oh! Ahsante Mungu, nimejifungua salama"
"Eee! Hongera sana jamani umejifungua katoto kakike, kamwali jamani"
"Asante sana, Mungu awabariki sana"
Wakunga walikuwa wakimpa pongezi mama yule huku wakimpa katoto kake akabebe baada ya kumfanyia hatua zote za usafi pamoja na kumkata kitovu. Mama yule alikabeba katoto kake na kukatazama huku akitokwa na machozi.
"Asante Mungu hatimae mwanangu yu salama sasa" alijisemea mama yule huku akika bembeleza katoto kake.
Ilikuwa ni Vicheji mkoani pwani katika wilaya ya mkuranga.Siku hiyo hiyo masaa hayo hayo aliyo jifungua mama yule, katika hospital ya muhimbili wodi namba kumi na saba (17) jijini Dar es salaam mama mwingine ana jifungua watoto mapacha.
"Hongera sana Dada hatimae umejifungua"
"Asante"
"Jamani mapacha!! Waoo!!"
"Alafu vya kike vyote"
"Hongera sana"
Manesi na madaktari walikuwa wakimpa pongezi mama huyo kwa kajifungua salama, pongezi zilikuwa nyingi sana kwa mama huyo alie jifungua watoto mapacha wakile walio onekana kufanana sana.
"Tayari na sikia kajifungua"
"Haya twendeni tukamuone"
"Sawa twendeni"
Walikuwa ni mama watatu walio kuwa wame kaa nje ya wodi wakisubiri mgonjwa wao ajifungue. Waliingia wodi namba kumi na saba (17) baada ya kusikia mgonjwa wao kesha jifungua.
"Waoo! Jamani shosti hongera sana umejifungua"
"Tena watoto mapacha, jamani na penda watoto mapacha Mimi"
"Eee! Jamani kweli, mimi sinili kwambia watakuwa mapacha mana walivyo kusumbua"
"Mh! Kweli haya ngoja tukupe chakula ili uapate nguvu"
"Nita shukuru kweli mama huko tumboni ninavyo kusikia"
Baada ya mama yule kupewa pongezi nyingi, mama mmoja alitoa chupa iliyo kuwa ndani ya kikapu cha kutungwa na mkono(ukili) alitoa chupa na kikombe kisha akamimima uji ulio cha nganywa na maziwa, bluband pamoja na sukari.
"Uji huu mtamu sana"
"Ndio nime upika hivyo ili ukupe nguvu kwa haraka"
"Ooh! Asante sana mpendwa wangu"
"Usha mwambia mumeo kama umesha jifungua"
"Hapana, bado sijamwambia, sasaivi atakuwa kwenye ndege kutoka ujerumani, tangu Jana aliniambia yupo safarini kurudi nyumbani. Nataka nimfanyie bonge la surprise"
Stori ziliendelea huku wa mama wakiendelea kumpongeza mwenzao kwa kajifungua salama watoto mapacha.
Lakini kwa mama mwingine huko vicheji yeye hakuwa na wakumpongeza usiku ule zaidi ya wakunga na taratibu wakunga walianza kurudi makwao baada ya mama yule kujifungua salama usalimini. Kwani hata hivyo alizalia nyumbani hakuweza kuwahishwa hospitalini.
Wakunga waliondoka wote akabaki mama mmoja ambae walikuwa ni jirani take na walizoeana sana kiufupi walikuwa marafiki wazuri walio patana na kusaidiana kwa kila jambo.
"Sasa Mzazi inabidi upate kakitu ka kuweka tumboni ili upate nguvu, mana lazima utakuwa unanjaa"
"Nikweli lakini humu ndani sina kitu chochote chakula pesa zote nimenunulia vifaa vya kujifungulia"
"Basi Mimi naenda kukuangalizia Kule kwangu"
"Sawa nitashukuru sana"
Dada yule alitoka usiku ule kuelekea nyumbani kwake kuangalia kama ana chochote ambacho kinaweza kumsaidia Mzazi wake. Alibeba unga ili mtengeneze Mzazi uji. Baada ya uji kuiva alimpa ili atulize njaa.
"Umeshampa jina mwanao?" Aliuliza yule Dada
"Bado ila nafikiria kumpa jina la marehemu bibi yake"
"Lipi hilo?"
"SABRINA"
"Eee! Hilo zuri kabisa mpe hilo hilo"
Basi kuanzia sikihiyo mtoto alianza kukua na jina LA Sabrina.
Baada ya kuwasili baba wa watoto mapacha kutoka Ujerumani alishuka uwanja wandege wa kimataifa wa mwalimu Julius Kambarage Nyerere uliopo Dar es salaam. Lakini alisha ngazwa sana kuto muona mkewe pale uwanjani kwani alitarajia kumkuta pale ili ampokee. Lakini hakuliweka sana akilini mwake alianza safari ya kwenda nyumbani kwake Mbezi beach, alipakia usafiri wa tax iliyo mpeleka hadi maeneo ya nyumbani kwake.
Baada ya mwendo mrefu na kukaa sana kwenye gari kutokana na foleni za jiji LA dar es salaam alifika nyumbani kwake. Moja kwa moja alielekea kwenye nyumba take namba 126 alifika getini akabonyeza swichi ya kengele iliyopo ukutani pembeni ya geti.
Alibinyeza kwa muda mrefu lakini hakuna aliye kuja jifungua geti.
"Inamana huyu Anitha hayupo nyumbani au vipi" alikuwa akijisemea mwenyewe huku akibonyeza kwa hasira ile kengele. Lakini bado Anitha hakufungua geti wala mfanya kazi wake wandani. Akachukua simu yake ya mkononi na kumpigia mkewe Anitha.
"Namba ya mteja unayo ipigia haipatikani kwa sasa, tafadhali jaribu tena baadae au acha ujumbe mfupi wa maneno" ni sauti iliyo kuwa ikijibu kutoka kwenye simu.
Kitendo hicho kilizidi kumtia hasira baba hiyo.
"Yani hili mwanamke, uwanja wa ndege hajaja kunipokea na geti hataki jifungua sijui yuko na mwanaume mwingine, haki ya mama tuta toana ngeu, yeye afe niende jela au Mimi nife pumavu kabisa" baba yule alikuwa akijisema mwenyewe kwa hasira sana. Akakaa nje pale kwamuda wa dakika kumi akawaza aruke ukuta.
"Sijui niruke hii fensi lakini hapana juu kuna nyaya za shoti ina wezekana hazija zimwa nitachezea maumivu hapa"
Akajaribu kubonyeza tena kengele lakini bado kimya.
"Sasa kama anoga ndio anoga muda wote huo, hapana hapana naibiwa sasa na vunja geti naolewake nipoteze nguvu zangu hapa alafu nimkute kakumbatiana na lijamaa nitakacho lifanya haijawahi tokea ulimwenguni" lakini akiwa anawaza kufanya hivyo alisikia ndani ya fensi.
lakini akiwa anawaza kufanya hivyo alisikia ndani ya fensi geti likifunguliwa, baada ya geti kufunguliwa alitoka mdada wake wa kazi aliye julikana kwa jina la vumilia. Baba yule alimsalimu vumilia na kofi moja zito sana la shavu huku aking'aka kwa hasira.
"Mshenzi wewe na mama yako hukondani, nimetoka safarini badala mje kunipokea uwanja wa ndege mme kalisha makalio yenu hukondani, sinili waambia saa nane na nusu mchana nita kuwa uwanja wa ndege au siku sema!!!?"
"Ulisema baba"
"kwa hiyo mmefanya kusudi!?"
"Hapana"
"Hapana nini! Shenzi nyie alafu bado mkaona haitoshi mka amua kukaa ndani kimya ili mimi niteseke hapa nje!?"
"hapana baba tuli... Tuli...!"
"Tuli.... Tuli....! Nini nipishe huko niingie shenzi kabisa! Na mkirudia tena huo ushenzi wenu nita piga wote wewe na mama yako, alaa...! Ngoja sasa nimuingilie na huyo mpuuzi huko ndani nayeye akanieleze kwa nini hakuja kunipokea!"
Baba yule alieleka mlangoni huku akiwaka kwa hasira na ghadhabu kama kalishwa pilipili mbuzi au kichaa. Alielekea mpaka mlangoni na kusukuma mlango kwa hasira mpaka ndani baada yakuwa amesha ingia ndani ghafla alijikuta akishangazwa na kile alicho kiona mbele yake.
Watu wengi walijaa sebleni wakiwemo ndugu zake rafiki zake na majirani, walikuwa wameshika vinywaji.
"Anitha mke wangu hii maana yake nini!?" aliuliza baba yule kwa mshangao.
"Hahaa! Huu lazima uwe mshangao kwako baba wewe mwenye hasira na ghadhabu kama mbogo, lakini sasa tuliza hasira zako kwani nina ujumbe maalumi kwako" Anitha alikuwa akimwambia mumewe huku akicheka.
"Aaa!Ume jifungua eeh?" Alisema baba yule huku akishangaa baada ya kuona kitumbo cha mkewe alicho kiacha kimejaa sasa kimepungua ujazo.
"Ndio na kikubwa nime kuzalia..... Au hapana, otea mwenyewe" kutokana na baba huyu kupenda watoto wa kiume alijikuta akibwatuka kwa nguvu.
"MToto wa kiume"
"Nop"(hapana)
"so what"(kwahiyo nini sasa)
"otea tu"
"Umenizalia toi"
Watu wote pale wali angua kicheko na kumwambia.
"WATOTO! MAPACHA!"
baba yule alipiga kelele za furaha na kumkumbatia mkewe kwa furaha huku akimbusu. Baada ya kuonyeshwa watoto furaha ilizidi hasira alizo kuwa nazo mwanzo.
"Jamani hongera mke wangu"
"asante mume wangu"
Watu walifurahi sana sikuhiyo, walikunywa walilewa na waka leweka walio leweka.
Watoto hawa pacha walizaliwa katika familia ya kitajiri yenye uwezo kifedha, mali na kila kitu.
"sasa mke wangu mimi Ninawazo"
"wazo gani tena?"
"kwa nini tusiwape hawa watoto majina ya Jasmine na Asmine"
"oh! Wazo zuri, sawa kabisa mume wangu kulwa tumuite Asmine na doto tumuite Jasmine kutokana na herufi za majina yao au"
"sawa tu mkewangu, pia itakuwa ni rahisi kuwa tofautisha" wazazi hawa wawili walifikia muafaka wawa toto wao kuwaita Asmine na Jasmine.
YOU ARE READING
SABRINA
RomanceSabrina ni hadithi inayo simulia maisha ya binti Sabrina ambae amezaliwa katika familia masiki mkoani pwani wilaya ya mkuranga kijiji cha vicheji, analelewa na mama yake katika mazingira magu mpaka anamaliza kidato cha sita kwa bahati mbaya mama yak...