"Baba huyoo.." Mama yangu alinipokea kwa furaha kubwa pale uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Nilienda Italia kwa ajili ya kuongeza maarifa katika elimu yangu ya dini Theology na Philosophy..
"Mama huyoo.." Niliitikia kwa furaha pia maana ni miaka takribani mitatu tangu niondoke nyumbani
Alinisaidia begi tukaanza kutembea kuelekea kwenye gari letu
"Karibu mwanangu, nilikumiss sana ulivyoondoka.. nikatamani hata ungeniachia mjukuu wa kuniliwaza hahahah" alinitania utani ulionigusa
"Aaah mama usihofu kuhusu hilo suala la mjukuu.. nimekuja na wazo la kuoa.." Niliongea uongo bila aibu
"Weeeeh..! Yani katika vitu umewahi kunifurahisha ni hilo suala la kuoa mwanangu.. nimefurahi sana, umekua baba angu.." alifurahi kutoka moyoni nami nilifurahi kumuona mama yangu akifurahi
Safari iliendelea vizuri sana, nikamsimulia mama mambo mengi niliyoona Italia hadi tukafika nyumbani.
Kwenye uwanja wa nyumbani nilimkuta baba na wafanyakazi wote wakinisubiri kama mfalme, hakika ilikua furaha sana kwangu..
"Karibu jembe langu, kidume wangu.. sasa hivi mlango wa mbinguni mweupeee ukifika unaingia fasta tu. Hongera sana mwanangu..!"
"Hahahah ahsante baba.. nashukuru uliniombea sana..!" Nilifurahi kuwakuta wote wazima kabisa
Tuliingia ndani, nilikuta meza iliyoandaliwa kwa ustadi mkubwa sana. Mishumaa iliing'arisha meza nzima, vyombo vyenye rangi ya dhahabu viliandaliwa kwa ajili ya chakula pamoja na vijiko vizuri sana
"Wow.. mama! Hii ni babkubwa.. umejua kunifurahisha asee.." Nilimkumbatia mama na kuendelea kushangaa urembo mbalimbali uliowekwa kwenye nyumba yetu
"All of this is for you son..!" Alisema baba, machozi ya furaha yalinilenga
"I don't deserve this dad.." Nilimkumbatia baba yangu
"You do baby.. haya uje kula, sitaki machozi kwenye nyumba yangu wakati ni siku ya furaha.." Alisema mama
Nilimsikiliza nikaenda mezani kula
"Oh..! Rodrick unamkumbuka Agness?" Mama aliniuliza swali lililonishtua kidogo
"Ndio, kafanyaje.."
"Alikua anakuulizia mara kwa mara na akaomba ukirudi umtafute.."
"Oh..! Kumbe.." Niliongea bila kujua niseme nini
Moyo wangu ulishtuka sana. Agness nilikua nikimpenda sana tangu sijaenda masomoni, imekuaje anitafute kwa bidii wakati hakutamani hata kuniona kipindi cha zamani..!
Sikutaka kujiuliza maswali mengi bali nilitamani kumuona na kusikiliza nini alikua alitaka kunambia
Baada ya kula nilipumzika kidogo hadi jioni ilipofika, nikavaa t-shirt yangu pendwa nyeusi na jeans nyeusi pamoja na raba nyeupe. Sijui kwanini nilitaka kupendeza sana japokua sikujua Agness alitaka kuniambia kitu gani..
Nichukua gari moja wapo kati ya magari yaliyokua kwenye parking lot yetu na kwenda kwao Agness. Imepita miaka mitatu lakini bado nilikua napakumbuka kama nilitoka jana.
Nilipofika nilimuona mama yake Agness yuko nje anachambua matembele, nikashuka kwenye gari kwa heshima na kumsogelea
"Shkamoo mama.."
"Marahaba mwanangu.. za masiku?" Aliweka matembele pembeni akainuka kunisalimu
"Nzuri mama, vipi nyie.."
"Tupo wazima sana.. Agness alikua anakuongelea hapa muda si mrefu.." Alisema
Moyo wangu ukazidi kujawa na shahuku ya kujua nini kinaendelea..
![](https://img.wattpad.com/cover/256199791-288-k75779.jpg)