Sehemu ya 4

2 1 0
                                    

Baada ya miezi miwili...

Tulikua tumekaa na mume wangu ambae kwa kiasi kikubwa alikua amebadilika na amempenda mtoto japokua anajua sio wake.. Nami nilikua nimebadilika sana. Tulimpa jina la Martha

"Hodi.." Ilisikika sauti mlangoni

Mume wangu akaenda kufungua mlango ni Mr. Richard na mwanamke mwingine aliyefanana naye sana, nikajua tu atakua mama yake

"Karibuni sana jamani.." Mume wangu akawachangamkia wakaingia ndani

"Mr. Rodrick, mimi na wewe tumekuwa marafiki wa kipindi kirefu sana japo kuna mambo nahisi hayako sawa.." Aliongea huku moyo wangu ukienda mbio sana

"Ndio.. japo sijui ni kitu gani unaongelea ambacho hakipo sawa.." Alionekana kutoelewa

"Nimemfata mtoto wangu Martha.." Nilitamani ardhi ipasuke niingie, nilifumba macho huku machozi yakinitoka

"Nani? Martha?" Alisimama kwa mshtuko.. alikua anajua Martha sio mtoto wake ila hakujua baba ni nani

"Martha ni mwanangu, kama huamini muulize mke wako.." Sikua tayari kwa hii vita siku hii

"Mke wangu ni wangu, kama mtoto ni wako pole sana maana mtoto kazaliwa na mke wa mtu.. ni mtoto wangu huyu.." Alijibu kijasiri

"Nayajua yote hayo, na nimejiandaa kikamilifu Rodrick.. Kiongozi wa kanisa nimemuita yuko njiani kusuluhisha hili.." Aliongea Richard kwa kuijiamini

"Siwezi kukubali mjukuu wangu alelewe na gaidi kama wewe.. mwanamke kahaba usie na aibu.." Mama Richard aliongeza

Moyo wangu ulihisi kutoka nje.. nikainamisha kichwa chini nikiwa sina la kusema

"Huwezi kumtukana mke wangu kahaba halafu nikakaa kimya.. Huyo kahaba ni mke wangu na nampenda sana, chunga kauli zako mama.." Alinitetea huku majuto yakiniandama sana kwa yote niliyomkosea na bado ananiita mke wake kipenzi

"Hodi.."

Mr. Richard akakimbilia mlangoni kufungua, akaingia kiongozi wa kanisa.. nilikua bado siamini

"Rodrick kijana wangu, unaendeleje na hali?" Aliuliza kistaarabu

"Naendelea vizuri baba.."

"Bila kupoteza muda, Mr. Richard amenielezea kila kitu kuhusu mahusiano yake na mke wako. Kihalali inabidi mtoto aliyezaliwa na mwanandoa nje ya ndoa alelewe ndani ya hio ndoa. Ila kiubinadamu, rafiki yako amepoteza mke wake na anaishi kwa upweke sana. Wewe tayari una watoto wawili na mke, tunaomba kama kanisa mtupatie huyo mtoto ambae mke wako amezaa nje ya ndoa ili ampatie faraja Mr. Richard.." Alisema

"Siko tayari.." Alisema mume wangu

"Kama miongoni mwa viongozi wa kanisa, unatakiwa kuonesha mfano mzuri kwa kutoa sadaka na kuwaonea huruma wengine.. usipofanya hivo basi hustahili kujiita mkristo.." Aliongeza

"Fine.. fine fanyeni mtakavyo.. kama mnataka kunitenga nitengeni, kama mnataka kunifukuza kabisa sawa ila mke wangu na mimi tutamlea mtoto wetu na tumeshaandaa tarehe ya ubatizo wake.." Alijibu kwa kujiamini

"Basi sawa Mr. Rodrick, nasikitika kwamba kuanzia leo wewe sio mwenzetu tena, sio kiongozi wa kanisa na muumini wa kanisani kwetu. Tunasitisha huduma zote za kiroho na kimwili juu yako, tunakutakia maisha mema.." Akaongea na wakaondoka wote

"Mungu wangu, ni nini hiki jamani... ni balaa gani hili? Mume wangu hawezi kukaa mbali na kanisa kabisa, mimi hapa mimi ndo shetani.." Niliwaza

.......................

Niliingia chumbani huku nikiwa nimeumia sana, machozi yakinitoka, nikiona kabisa Mungu ameniacha.. hadi nimetengwa na kanisa. Nilipiga magoti chini na kulia kwa Mungu..

"Ee Mungu wangu, nilikuomba mke mzuri ukanipatia, daima nimekua nikimuombea aende katika njia njema. Imekuaje leo hii amenikosea kiasi hiki? Nimekosea wapi Mungu wangu? Nilimpenda sana, nikamjali na kumthamini, sikutaka aaibike mbele za watu hata baada ya kujua amebeba mimba nje ya ndoa..! Leo nimetengwa na kanisa na nimepoteza kila kitu hata elimu yangu haina maana tena. Nifanye nini Mungu wangu? Nifanye nini? Siwezi kuishi tena, sina furaha ya kuishi nje ya kanisa..."

Kipindi nikisali nikaona hamna haja ya kuendelea kuishi.. Nikanyanyuka nikafunga mlango kwa ufunguo, nikafungua droo ya kabati tunakoweka vidonge nikamimina vingi sana na kumeza kwa maji kidogo sana ya bafuni..

"Ee Mungu nakuomba unipokee mikononi mwako, naomba unisamehe kwa kujiua.. naomba unisamehe na unipokee kwako. Mlinde mke wangu na umpe ujasiri wa kuwalea watoto katika njia njema, mimi siwezi kuendelea tena.." Nilisali kimoyo moyo na hatimaye nikakata roho

.......

Nilikaa muda mrefu sana sebuleni nikilia bila kusikia sauti ya mume wangu, ikabidi nikaongee nae nimuombe msamaha maana nimemkosea sana na kumharibia maisha yake

Nilipofika kwenye mlango wa chumbani nikakuta umefungwa..

"Mume wangu.. nifungulie basi.. naomba unisamehe mume wangu, nakuomba ufungue mlango basi tuongee.." Niliongea lakini sikupata jibu lolote

Nililia na kubembeleza sana bila mafanikio yoyote hadi nikakaa chini mlangoni pale

"Kiukweli bora nisingeolewa na wewe, nimekuharibia maisha yako yote. Nilitamani kuolewa na mwanaume tajiri na wewe ndo ulikuja akilini kwangu, sikukupenda wewe.. nilipenda pesa zako ndio maana alipokuja Mr. Richard, nikaona ana pesa zaidi yako.. nikaanza kukuona huna lolote... Ila, baada ya mimi kupata matatizo ndio nimegundua kwamba ulinipenda sana na ulikua tayari kupoteza kila kitu kwa ajili yangu. Nimekukosea sana mume wangu na sasa ninakupenda kweli kabisa.. sihitaji chochote duniani hapa, nakuhitaji wewe unisamehe.. tusahau yote na tuanze upya.." Niliongea hadi nikapitiwa usingizi

Baada ya muda nikakurupuka usingizini..

"Mume wangu.. nifungulie basi.." Nililia sana

"Rodrick.. mi navunja mlango.." Nilisema na kumaanisha

Nilitafuta namna ya kuvunja mlango na kufanikiwa.. nilimkuta Rodrick amelala chini amepoa sana.. nilishtuka mno

"Rodrick jamani.. amka tulale, usilale chini hapo.." Nilianza kumuamsha

"Rodrick.." Nikamshika mkono ila alikua amelegea sana.. "Mungu wangu.. amka jamani Rodrick.. usinifanyie hivi mimi jamani... amkaaa.. Ee Mungu nakuomba umuamshe mume wangu jamani, ntaishije mimi bila Rodrick, hata sijakuomba msamaha baba yangu.. Amka hata dakika moja baba angu, nakuomba.." Nililia lakini alibaki kimya.. Alikua amefariki tayari, nililia sana kwa maumivu na majuto maana amejiua kwa ajili yangu..

Baada ya mazishi nilikaa chini, nikiwa na maumivu makubwa mno.. Nikiomba msamaha kila baada ya dakika.. Nilikuta madhabahu iko safi nikaitia doa lisilofutika.. Kila nikikumbuka hivi nilikua nikitubu..

"Ee Mungu, usinihukumu kwa wingi wa dhambi zangu.. bali huruma yako iniponye.. Nilikuta madhabahu iko safi, nikaitia doa lisilofutika... Unisamehe mimi mkosefu na usiniache..."

MWISHO

Bạn đã đọc hết các phần đã được đăng tải.

⏰ Cập nhật Lần cuối: Feb 23, 2021 ⏰

Thêm truyện này vào Thư viện của bạn để nhận thông báo chương mới!

THE STAINED ALTARNơi câu chuyện tồn tại. Hãy khám phá bây giờ