Nilipofika kwa Mr. Richard niligonga na haikuchukua muda alifungua mlango..
"Ah! Shem.. kuna nini? Ungenipigia simu tu, hata usingehangaika kuja huku.." Alijibu kwa hofu akidhani kuna tatizo
"Hio simu yenyewe unayo?" Nilimuonesha simu yake
"Aah! dah.. aseee ahsante sana shem.." Alinishukuru na kuichukua simu yake
"Unaendeleaje lakini? Haupo sawa kabisa.." Niliuliza
"Bila Martha mimi sio kitu yani.. nampenda sana Martha.." Alijibu na kunikumbusha machungu niliyokua nimesahau kwa muda
"Haha najua, ila jitahidi hata kulala maana Martha kesho atatoka hospitali.. unataka akukute umechoka ovyo..?" Nilijibu kwa kujikaza
"I need to drink some wine.. labda ndo ntaweza kulala.." Alisema na kuelekea chumbani.
Baada ya muda alirudi na chupa ya wine pamoja na glass mbili.. kimoyo moyo nilisema "leo sikuachi salama.."
Tulianza kunywa wine, yeye alikunywa kwa speed sana na kuongeza glass zaidi ya tano.. Mimi hata ile glass ya kwanza sikunywa hadi robo, sikutaka kulewa kabisa.. Baada ya masaa kama mawili hivi, alikua amelewa hoi
"Nenda ukalale.." Nilimuamsha ili niondoke.. "Nataka kuondoka.."
"Usiondoke Martha wangu, tukalale wote.." Alinishika mkono
"Mimi s.." Nilitaka kumwambia sio Martha ila nikasita
"Aya twende.." Nikamnyanyua pale.. mzito balaa, nikamkokota huku nae akijitahidi kutembea hadi tukafika..
Nilijikaza nikavaa roho ya simba.. nikalala na Mr. Richard akidhani mimi ni Martha
Asubuhi aliwahi kuamka kabla yangu..
"Jesus...!" hio kelele ilikua kubwa hadi ikaniamsha
"Agness.. what's happening?" Alionekana kuchanganyikiwa
"I don't know.. I'm as confused as you are.." Nilijibu kinafki
"Did we sleep together? like really sleep together.." Aliuliza swali ambalo lilinichekesha ila nikajikaza
"I guess so.." Nilijibu kwa pozi
"My wife will kill me.." Alisema kwa hofu sana
"I have a husband as well, kwahiyo what happened between us inabidi iwe siri.." Niliongea kijasiri
"Okay leave please.." Aliniharakisha kuondoka
"That's not how you are supposed to treat a woman you slept with the entire night.." Nilijibu kama kahaba
"Excuse me?" Alishangaa jibu langu
"I'll get going babe.." Nilimchokoza
"Babe..?" Alishangaa tena
"Just kidding.. bye shem.." Nilimuaga na kuondoka
Nilipofika hospitali nilimkuta mume wangu anapiga story na Martha wanacheka kweli
"Babe..! umefika saa ngapi?" Niliuliza kiujasiri
"Muda si mrefu, kama dakika kumi zimepita.. ulikua wapi?"
"Nilienda kufata supu ila nimekuta foleni, nimeagiza atuletee huku mimi na mgonjwa hahaha.." Nilijibu
"Hahaha wewe na mgonjwa tuu.." Alikazia
"Ndio.. how was your night?" Niliuliza
"Lonely.." alijibu kiupole
"Don't worry, leo narudi.." Nilijibu na ghafla akaingia Mr. Richard hakutaka kuniangalia usoni
