Chapter 1

8 0 0
                                    


Ding dong...! Kengele ya mlango ililia

"Nani?.." niliuliza bila kupata jibu lolote kabla ya kengele kulia tena mara ya pili

Nikasogea na kufungua mlango kwa tahadhari.. ghafla akaingia mume wangu kwa nguvu sana kiasi cha kuniangusha chini

"Kwanini umechelewa kufungua mlango..?" Aliuliza kwa hasira sana

"Kwani vipi jamani.. mbona hivo?" Nilijikokota nikasimama na kufunga mlango ulioachwa wazi na mume wangu

"Mbona una hasira hivo? Nini kimetokea hadi umerudi mapema nyumbani?" Niliuliza kwa upole bila kupata jibu lolote

"Nisamehe sikujua kama wewe ndo ulikua unagonga mlango.." Nilimsogelea na kumshika begani ili kumtuliza

"Ebu sogea huko bhana.." Alitoa mkono wangu begani kwake

"Ukoje wewe..? Lione..! Kama chizi vile, hivi huoni kama niko na mawazo mengi? Huwezi kukaa kimya? Unanipigia kelele wakati niko na mambo mengi ya kutafakari.." Alinifokea kwa sauti ya ukali sana ambayo sijazoea kabisa

"Jamani.. umekuaje wewe? Yani huongei kitu unafoka tu..! Sasa ulitaka nifanyeje? Nikuache mwenyewe nikalale au nicheke tu wakati unaonekana haupo sawa...?" Nilijikaza nikamjibu

"Huna msaada wowote wewe..! Hujui lolote, kazi yako kukaa tu ndani.. yani uko useless..!" Alizidi kunitukana

"Imetosha...!" Nilishika remote na kuzima tv kisha nikaondoka kwenda chumbani

"Najuta kwanini hata nilioa mwanamke mwenye kelele kama wewe.. Ndo kwanza miezi mitatu ila mikosi imeshaanza kutawala nyumba yangu.." Alizidi kuongea

Niliumia sana roho yangu hasa nilipokumbuka namna mume wangu alivyonilazimisha kuacha kazi ili nisimtawale ndani ya nyumba na leo ananitukana sababu nashinda ndani bila kufanya chochote..!

"LOVELY...!" Mume wangu aliniita kwa sauti sana

"Abeee..!" Nilishtuka na kwenda mbio sebuleni

"Nini baba.." Niliuliza kwa mshangao na hofu

"Unamfahamu Ricardo?" Aliuliza akiwa ameshika simu yangu

"Ricardo yupi?" Nilishangaa lile swali

"Ricardo Morris..!" Alinionesha picha yake kwenye simu yangu

"Yeah..! Ni rafiki yangu sana. Nimesoma nae chuo Canada.." Nilimjibu

"Jamani Lovely.. kwanini hujanambia siku zote hizi?" Aliongea kwa upole usio wa kawaida

"Sorry. sikujua kama ni such a big deal.." Nilimwambia kwa upole

"It's alright babe.. mi wala sikulaumu. Mara ya mwisho kuwasiliana na Ricardo ni lini?" Aliuliza taratibu

"Last week alinipigia kunijulisha kwamba anakuja Tanzania na anaomba tuonane akifika.." Nilisema

"Seriously?" Aliuliza kwa mshangao

"I'm sorry honey.. kweli nilitaka nikwambie leo ukitoka kazini.. I swear.." Nilijibu kwa hofu sana

"Hey.. Babe.. no..! Sijamaanisha hivo.." Alinishika mkono na kunikalisha chini

"I'm just so happy kwamba unamfahamu Ricardo, wewe hujawahi kunitambulisha kwa marafiki zako wengi hadi leo nashangaa unamfahamu mtu muhimu kama Ricardo. Sijutii kukufahamu kipenzi..." Aliongea kwa furaha na upole nami nikafarijika.

Asubuhi na mapema niliamshwa na mlio mkubwa wa simu yangu ila niliipuuzia maana nilikua na usingizi sana..

Baada ya dakika kadhaa simu iliita tena, nikamsikia mume wangu akiamka kuangalia nani anapiga.. Ghafla akakurupuka na kuniamsha

I LOVE YOU BUT I'M MARRIEDTempat cerita menjadi hidup. Temukan sekarang