Sehemu ya Kwanza(01)

7 1 1
                                    

     Ni saa tatu asubuhi,siku ya Jumamosi Bwana Kefah Mpevu kaonekana amekaa kwanye kiti  cha plastiki nje ya Nyumba yake yenye vyumba vitano.Huku akitazama eneo lake alilolinadhifisha kwa miti ya kila aina aliyoipanga kwa utaratibu uletao mvuto mzuri sana ukiitazama. Eneo lenyewe lilizungukwa kwa ua wa mimbooni iliyochanganyikana na mimea mingine.Ua wenyewe ulichongeka kwa ufundi wa hali ya juu ukiutazama lazima uchukue muda kuuchambua ukose kuumaliza.
Kazi hii kafanyika na mwana wa jirani yake kwa jina la Bi.Hilda,aliyetambulika kama "Mama Kidoh."
Kidoh alibarikiwa sana kwa kipawa cha sanaa ya uchoraji na Uchongaji.
Kidoh mwenyewe alikuwa kijana mpole,mwembamba na mrefu. Miaka yake yapata ishirini na mitatu. Ni kijana ambaye hakupata elimu bora kama wana wengine wapatayo. Babaye mzazi kafariki angali mdogo sana kawacha jamaa yake kwa mikono michochole kilichompelekea Kidoh kukosa malezi bora. Bi. Hilda nae alikuwa mchapakazi sana ila kipato hakikuweza kukidhi mahitaji kwani juhudi za mkono mmoja tena wa kike hazingeweza kutafuta chakula,mavazi,elimu na vitu vingine vya kimsingi. Bi. Hilda alikuwa katambulika sana kama 'Mkulima bora'. Lakini mkulima mbona asiweze kumsomesha mwanae. Bi.Hilda ndiyo alikuwa mkulima ila wa kukodishwa kwa malipo duni. Bi.Hilda angeifanya kazi hiyo kwa ustadi.Angekuwa na shamba angelima vya kwake vimsaidie ila shemeji wake walimnyang'anya shamba aliliachiwa na mmewe marehemu.Kasalia tu na nafasi ya kunyumba na msala tu pamoja na eneo dogo umbali wa kutema mate.
Kando na ukulima wa kukodishwa angepasa kila aina ya kazi ingekuja usoni mwake.
Kikubwa zaidi Bi.Hilda alimiliki tabia ya upole na unyenyevu,hakuwa mtu wa kuzua vurugu na malumbano, la hasha! Alikuwa mfano bora kwa wanawake wote wa kijiji cha  Jitahidi.
Mama mtu aliambukiza tabia zake za upole kwa mwanae Kidoh. Na si tabia tu bali na jitihada.
Bi.Hilda aliweza kumsomesha Kidoh shule ya msingi tu.Maana mkono hukuna ufikapo.Shule ya upili hangemudu gharama ya karo ya shule ya upili. Mungu nae ana mpango na kila mja,alimjalia hekima na uelewa kwa sanaa za kutumia mikono kama uchoraji wa picha,maandishi,kupanga rangi,kuchonga nyua na maua kwa umbo lolote ulitakalo.
Kwa kazi hizo Kidoh huwa anamsaidia mamaye kwa kutimiza baadhi ya majukumu,kitu ambacho humfanya moyo wa mamaye kufurahia,kutabasamu na kumbariki mwanae.
Hata Mola mwenyewe kwa sheria zake kumi kaamrisha wana kuwapenda na kuwaheshimu wazazi wao wapete kuishi maisha marefu. Lakini si marefu tu bali na yenye baraka tele.
Huu ndio urithi mwana aupatao kutoka mwa mzazi.
Kidoh alimuenzi mamaye jinsi mtu huienzi mboni yake.Kwa kidogo apatacho angempa mama sehemu fulani. Jambo hili lilimba Kidoh kibali na kuwa maarufu sana kwani watu walimtambua sana kwa kazi yake nzuri na wakawa wanamuitia kazi mara kwa mara.
Kidoh hata kwa kazi zake ndogondogo hangeweza kununua ardhi sehemu nyingine,licha ya kuwa ni azimio na ndoto ya moyo wake.Alikifinya kijumba chake cha nyasi palepale kwao kwa lile eneo dogo waliloachiwa na Amu zake. Kidoh aliishi kutamani kulipa kisasi na kunyakuwa shamba lililokuwa lao,ila Amu zake 'wanajuana' na wakuu wa serikali.Maana Kidoh amejaribu kuwapa ripoti ila hajapata msaada wowote.Jambo ambalo humpa Kidoh mawazo mengi sana.Kwani yeye ni mwanaume,akipata familia yake itaishi wapi? Kidoh mara nyingi husumbiwa na hilo swali ambalo humfanya kutamani apate pesa anunue shamba kwingine waende na mama yake.Lakini pesa za kununua zitatoka wapi wakati kazi yake ni ya malipo duni na mahitaji ni mengi?Ila matumaini hayakwishi kwa mja aliyehai,ndicho kitu alichojiambia.Na kikubwa sana anachokienzi ni 'tabasamu'la mamaye mzazi.Hapendi kumuona akidhalilika wala kuumia ila tu amwone akifurahi siku zote.
Eneo la Bw.Kefah pia lilipandwa nyasi zikapandika na zimefyekwa zikafwekeka
Madhari yale yalikuwa ni ya kuvutia sana.
Kazi hii yote Kidoh kahusika ndani.
Bwana Kefah alimpenda sana Kidoh kutokana na kazi yake nzuri yenye utadi mkuu.
Kidoh kijana aliekosa elimu ya shuleni akabarikiwa na uwezo mkuu wa kufanya kazi za jasho na mikono kwa utadi mkuu sana.

Tabasamu la Baba ndilo Urithi wanguWhere stories live. Discover now