Sehemu ya Tatu(03)

3 0 0
                                    

Bwana Kefah aliwapenda sana wavyele wake kuliko kitu chochote kile kwani walijinyima mengi ili kuwapania yeye na ndugu zake.
Ni wazazi waliokosa elimu za shuleni lakini walikuwa walimu wazuri wa mafunzo ya kimaisha. Kefah na ndugu zake hawakulelewa katika maisha ya ukwasi kwani wazazi wao hawakuwa wakwasi.Walilelewa kijijini na maisha ya kijijini unayaelewa tu jinsi yalivyo.
Kina Kefah kiamsha kinywa chao lilikuwa jembe au kazi ya aina yeyote ile.
Kwani kwao methali ya asiyefanya kazi na asile ndio iliyopewa nafasi ya kwanza. Ungelishinda njaa kama usingelifanya kazi. Maisha haya enzi hizo yangeunwa ni unyanyasaji wa watoto lakini mzazi angemnyanyasaje mwanawe.
Kwa wengine wangeliona kama kosa na unyanyasaji ila kwa Bi Juhudi ilikuwa kuwapa wanewe elimu ya msingi itakayowasaidia kukuwa wakijua hali ya nyumbani kwao jinsi ilivyo.
Kadri siku ziliposonga na kupita ndipo akili za Kefah zilizidi kuchua,ndivyo alizidi kupevuka na kujua maisha ni nini na yanafaa kukabiliwa vipi.Akawa anaelewa mbona wavyele wake hawakuwa wakwasi na mbona Mungu akamruhusu kuzaliwa kwenye familia ila.
Kwa kweli familia ya Bi na Bwana Mwamba licha ya uchochole walichokiridhi ni utu,upole,bidii na amani. Vitu hivi vilikuwa nguzo muhimu ya aila hii kusimama pasipo talaka wala malumbano na matusi. Bi Juhudi aliwalea wanawe kwa msingi bora.Licha ya changamoto zote alihakikisha wanawe wamekula na wamevaa. Ungewaona kina Kefah wakitembea barabarani ungedhani ni wana wa mfalme. Mama yao aliwalea vyema kipindi Bwana mwamba alikuwa kazini akipambania familia yake pia.
Wazazi hawa walipambana kwa udhi na uvumba kuwapa wanao malezi bora ambayo wao walikosa kuyapata kutoka kwa wazazi wao.
Hawakutaka pia wanao wapitie kwa mkondo waliopitishwa ndani.
Walitamani masomo ila nafasi walizikiosa na hawakutaka pia wanao wakose masomo kama wao walivyokosa. Kupata wazazi kama hawa ni adimu sana. Wengine huchoka na kukwepa majukumu.Wanaanza ulevi na kusahau majukumu yao. Ila kwa Bi na Bwana Mwamba ilikuwa tofauti. Wao walisaidiana sana kama kidole na kucha kupambania maisha yao na ya wana wao.
Kefah alikuwa akielewa wazazi wake na hungempata akizozana nao wala kuwatukana kama watoto wengine watukutu wafanyavyo.
Alikua kwa heshima kwani alikunjwa angali mbichi. Hakugusa kitu cha mtu,aliwaheshimu watu na mali zao. Na si Kefah tu bali wana wa Bwana Samson hawakuwa na tabia ya udokozi wala unyang'anyi.Wote walikuwa na heshima walifundishwa kuridhika na chao wasikitamani cha mtu,wakaelewa mafunzo na kuyashika hadi wa leo Kefah amekuwa mtu mzima hawai patikana akifanya maovu.
Ni mtu anayetii na kuliheshimu jasho la wengine jinsi angependa na lake liheshimike.
Juhudi za wazazi wake ndizo alizozirithi kwa asilimia mia moja.

Tabasamu la Baba ndilo Urithi wanguDonde viven las historias. Descúbrelo ahora