Sehemu ya Nne(04)

2 0 0
                                    

Bwana Kefah alingia subuleni mwake akaketi kwenye kochi huku macho kayatunga kwenye picha ya aliyoipiga na babaye mzazi aliyokuwa kaiweka ukutani.Picha hii ilikuwa na kumbukumbu nyingi kwake Bwana Kefah. Ni picha ambayo humfanya Kefah kumheshimu sana baba yake na kumuenzi zaidi. Picha ambayo humfanya Kefah asitamani kumuona Mzazi wake akiwa amekasirika au kukasirishwa.Picha inayompelekea kusaidia babaye awezapo.Picha hii inaonekana yenye thamani kubwa na siri nzito kwake Bwana Kefah

Je,Picha hii ina siri gani? Kumbe ni picha walioweza kupigwa kwenye lango la hospital moja Kuu kwa jina la Central Kule Bikini Kericho.Bwana Kefah hiyo picha ni ya kumbukumbu kuwa sana kwani alikuwa kabakisha sekunde chache tu kupoteza babaye mzazi asimuone tena.
Je nini kilitokea? Ni swami ambalo msomaji ana we za jiuliza sana.
Hivi ndivyo ilivyokuwa. Wakati huo Bwana Kefah alikuwa shuleni akiwa kidato cha nne.
Jioni akishatoka shuleni na rafikiye Bakari,alifika nyumbani walikokuwa Wanaishi.
Kefah hakumkuta babaye nyumbani walla kuona mavazi yake ya kazini. Muda ukasonga ikawadia Saa mbili masaa ya jioni baba MTU haonekani wala dalili zake hazikuwepo. Jambo hili halikuwa la kawaida tangu Kefah alipomjuwa babaye.
Kefah alianza kuulizia kwa wafinyikazi wengine waliokuwa wakifanya pamoja na Babaye asipate habari na hata wengine hawakumuona siku hiyo kazini. Kiwewe chungu nzima kilimja Kefah mwilini huku akili zake na dhamiri zikimhakikishia kuweko kwa hatari. Akiwa kwenye harakati za tafuta-tafuta hapa na pale mmoja kati ya rafikize kwa jina Evans akaja. "Baba yako anaendelea vipi? Naskia kaokotwa barabarani akiwa hali mbaya." Alimuuliza Kefah. "Eti wasemaje!"Kefah alimaka huku kapigwa na bumbuwazi. Akili zikamtoka,kichwa kikazunguka asikose kuamini aliyoyaskia.
"Tafadhali nieleze Evanso,umezipata wapi hizo habari wakati mwenyewe nimeuliza hadi kwa rafiki same baba hawana habari zake?"Kefah alimsihi.
"Pole ndugu yangu,nilipofika nyumbani niliambiwa na mama yangu kwamba asubuhi akitoka ofisini alikutana na bwana Mwamba akiwa amelala kando barabara kwa njia kuu ya kuelekea ofisini. Akamuuliza kama anaumwa asijibiwe polite kwani Baba yako alionekana mwenye machungu makali. Bahati nzuri Lori mojawapo ya malori ya kampuni likapita mama yangu akalisimamisha huku akipayuka 'msaaada! jameni Saidia!' Ndipo dereva akasimamisha Lori wakambeba wakamkimbiza zahanatini akamwacha huko akishughulikiwa. Hivo ndivyo nilivyoambiwa na mama."Evans alimweleza.
Hapo Kefah alizidi kuchanganyikiwa zaidi. "Ni sawa Evanso asante kwa taarifa yako" Alisema hayo akatoka mbio za mguu niponye kuelekea zahanatini jioni hiyo akamuwacha Evans. Akakuta kumefungwa.Akabisha lango kwa nguvu huku akihema kwa sauti kuu. Bawabu akatokea.Kefah akamwelezea."Ama ni yule mzee aliyechukuliwa hapa na ambulesi akiwa amezidiwa sana?"Bawabu alisema kwa kubahatisha. Kefah alichanganyikiwa akailaani siku aliyozaliwa kwani alikosa matumaini kabisa na wakati ulikuwa umeenda sana,hangeweza kufika mjini kumtafuta babaye. Na simu yake akipiga haikuwa inafanikiwa kuingia. Akarudi kwa nyumba yao huku amedhoofika na kunyong'onyea sana.Asikose kujua lakufanya. Maswali yalimjaa akilini mwake,ni nini kamtendekea maskini babaye,alimuaga vyema tu akienda shuleni.iweje akazidiwa?
Wakati wa Saa tatu usiku akaona simu ikikiriza,Kefah kaiparamia kwa hofu kuu kwani namba ilikuwa ngeni awake.
Akaishika kaielekeza sikioni. Akasikia ni sauti ya babaye ila ila aliongea kwa unyonge sana na kwa maumivu makali.
Babaye akamweleza kuwa alizidiwa na ugonjwa asubuhi akienda kazini,akachukuliwa Zahanatini ikahudumiwa ikashindikana akapelekwa Central Hospital akafanyiwa oparesheni, amepasuliwa tumbo wakakata utumbo uliokuwa umekunjana ambao ungemletea kifo asingeshughulikiwa kwa wakati, wakamshona na atakaa siku kadhaa ndipo atoke kitandani.
Bwana Kefah alikosa kuamini ila ikawa ishatokea.

Tabasamu la Baba ndilo Urithi wanguDonde viven las historias. Descúbrelo ahora