1.Kurudi Nyumbani

763 20 9
                                    

Ni muda mrefu tangu nilivyoondoka Tanzania, nilikuwa nafikiri huku nikiangalia nje ya dirisha la ndege, inaonekana hata nyumbani bado panaendelea, tabasamu dogo lilijichora mdomoni kipindi ndege inatua kiwanja cha ndege cha Mwl j.k Nyerere.

Inawezekana najisikia amani kwa sababu nimerudi Tanzania kwenye nchi walipo rafiki zangu wapendwa au kwa sababu nimefanikiwa kuyakimbia matatizo ya familia,nilijisikia uzito kifuani baada ya kukumbuka hali niliyomwacha nayo baba uingereza.

Nikavuta tu pumzi ya nguvu kipindi nashuka kwenye ngazi za ndege na kujaribu kupotezea mawazo kwa kuangalia huku na kule kama kunakitu kipya cha kuona.

Baada ya ukaguzi, nilichukua begi langu moja nililokuwa nalo na kuliburuza kuelekea nje, sikuwa na mizigo mingi kwa sababu nilipanga vitu kwenye begi dakika za mwisho kabisa ili familia isigundue kwamba nataka kuondoka......au niseme kutoroka.

Nikatabasamu kidogo baada ya kujisikia kama James Bond.

Hapakuwa na mtu wa kunipokea uwanja wa ndege kwa sababu sikumwambia mtu yoyote aje kunipokea, najidanganya mwenyewe kwamba nataka kuwashtua lakini kiukweli sikutaka tu waniulize kwanini nimeamua kurudi ghalfa.

Niliingia kwenye moja ya Taxi zilizokuwa nje ya airport baada ya kuweka mzigo kwenye boot, nilijisahau nikataka nikae kwenye siti za nyuma kwa sababu nimezoea taxi za uingereza.

"Unaelekea wapi?" Dereva taxi alisema.

"Nipelekee...xxxxx" nilimjibu kwa kusita.

Aliweza kukisia kwamba najua kiswahili kwa sababu ngozi yangu ni nyeusi lakini kwa sababu mama yangu alikuwa muingereza, unaweza sema rangi ya ngozi yangu ni brown.

Nilishukuru kugundua kwamba bado kiswahili changu hakijaharibika sana, sio kwamba nilikuwa siongei kiswahili kabisa kipindi niko uingereza na familia yangu lakini ili tuzoee kiingereza, ilikuwa kama sheria kukitumia kwenye maongezi.

Familia yetu haijawahi kuwa na mawasiliano sana na ndugu wa kwenye ukoo, nadhani baba amewahi niambia kuhusu ndoa yake na mama ilivyopingwa na wanaukoo, sikutoa macho yangu dirishani hata mara moja tangu safari ya taxi ianze, jiji halijabadilika sana kama nilovyotegemea lakini kuna mabadiliko kidogo.

Tulisisimama kwenye trafiki, ghafla sauti nzito ikanishtua "Inaonekana umetoka safari ya mbali?" Aliniuliza dereva taxi kwa kupaza sauti utafikiri ameniita mara mia bila mimi kumsikia, Niligeuka upande wangu wa kulia polepole ili nimwangalie vizuri, sura yake ilikuwa na tabasamu dogo, nikageuka mbele huku nikivuta pumzi kwa nguvu.

"...ndiyo!" Nilijibu huku nikiiachia pumzi, Nilisema huku nikigeuka upande wa dirisha nikijaribu kumpotezea kwa sababu sijawahi kuwa mtu wa kuongea sana na watu ntakaowaona kwa muda mfupi.

Nadhani nae alielewa kwamba sijisikii kuongea sana ndio maana akakaa kimya, taxi ikaanza kusogea pole pole, jiji hili halijawahi kutokuwa na tatizo la trafiki barabarani.

Pembeni ya barabara kulikuwa na kiwanja cha mpira, kichwani zikaja kumbukukumbu za siku za sekondari kipindi bado nipo Tanzania, sikukosa kuwa kiwanjani kila nikiwa na nafasi, sio kwamba napenda sana mpira lakini ilikuwa ni moja ya sababu kwanini nilikuwa napatana na rafiki yangu wa karibu Kelvin.

Kelvin huwezi kumwambia chochote kuhusu mpira, tumewahi gombana mara nyingi sana uwanjani kwa sababu nilikuwa sichezi jinsi anavyotaka yeye .

"Haha..." Nilicheka kwa sauti ndogo, sijui itakuwaje nikikutana na Kelvin kwa sababu niliondoka bila kumwambia chochote mbaka dakika za mwisho, nafahamu kwamba amefanikiwa kuingia kwenye moja ya timu kubwa za mpira, alinitumia meseji facebook baada tu ya kukubaliwa kwenye majaribu.

Mapenzi Ya PembetatuTahanan ng mga kuwento. Tumuklas ngayon