Mara nyingi alijiita ‘Bazu’
Mkuu wa idara ya mapenzi
Hamna kike mtegoni angeepuka
Mistari malenga ndio washindani
Jiji likamjua na likamtambua
Sifa akabeba na akakolea
Raha ikampanda ‘hepi’ zikanoga
Pakashume akajidai simba marara
Sikia leo bwagu kapata bwaguzi
Mechi mabao katinga tena virahisi
Amekuwa baba wa mabinti na wana
Jukumika hataki mafichoni ameenda
Daktari anasema ako na kisosnono
Yamkini anayo kaswende pia
Daktari ameshauri akapime Ukimwi
Leo si ‘bazu’ si ‘champe’ si bingwa
Leo Bingwa kimemramba pasipo
Simba amezeeka na meno kangooka
Mifupa hawezi tafuna tafuta tena
Amejuta! analia sana
