MALIPO SEHEMU YA 04

28 3 0
                                    

*Endelea.....*
STORY: *MALIPO*
MWANDISHI: *IRENE SYLIVESTER MBUYA*

               *SEHEMU YA 04*
      Basi niliondoka ili kumuwahi mdogo wangu kwani muda ulikwisha enda sana na si kawaida mpaka mda ule kufika hatujaonana. Niliona kama mlango wangu wa bahati umefunguka siku io nlienda nunua chakula kizuri nilimnunulia na mdogo wangu na soda kwani ni kwangu ilikua bahati ya mtende kuota jangwani. Ilipofika Jumamosi nilienda pale hospitali baada ya kuonana na daktari nilikutana na Dada Jacky namwita dada kwani Jacky alinisaidia sana japo ilifika mahali mambo yakabadilika,basi Jacky alinambia nimsubiri mpaka atoke kazini alafu atanipeleka anakoishi nikapajue. Alininunulia chakula hakika kwa upendo ule kuna vitu nilianza sahau furaha ilianza rejea tena,dakika chache baadae Jacky alikuja pale aliponiacha nikila alinikuta palepale kwani alinambia nimsubiri mpaka atakaporudi. Tuliongozana na Jacky hadi nyumbani kwake njian alinambia anaishi na rafiki ake wa kiume(mpenzi) hivyo akanisihi sana nisiogope hana shida hivyo niwe na amani. Tulipofika nyumbani tulimkuta huyo mpenzi wake akiangalia filamu ya kizungu ya kutisha tisha,alinitambulisha kwa mpenzi wake huyo aliefahamika kwa jina la George. Nilikaribishwa katika nyumba ile kwa furaha na wote walinipenda nilikaa nikajisahau nikasahau kuwa muda ushasogea sana nipokuja kushtuka ilikua sa mbili usiku,niliaga na kutaka kuondoka
"Getrude ni usiku sana mdogo wangu huogopi?"aliniuliza Jacky
"Hapana siogopi kwani kuna shida gani?"nami niliuliza
"Hapana shida wala ila tunahofia hali yako hivyo si salama sana kwa wewe kutembea huko nje mda huu"alikazia mpenzi wa Jacky
"Tatizo ni mdogo wangu atalia sana kwani hajazoea kulala bila kuniona mimi ingawa huwa hatulali sehemu moja"
"Usijali kesho asubui utaenda kumwangalia sawa Getrude"alisema tena Jacky
     Niliwaskiza wao na nilibaki kwao kwa mara ya kwanza tangu wazazi wangu wafariki nililala kitandani yaani nilihisi kama ndoto kupata fadhila namna ile. Nilisahau mateso yote niliyopitia kwa muda mfupi tuu ila maumivu yalikua palepale tuu mbaya zaidi nilipomkumbuka Julian jinsi alivyokuwa akiteseka niliwaza *'hivi nina raha gani wakati wadogo zangu sijui hata wamekula nini wala sijui wana hali gani Eeh Mungu naomba uwaangalie wadogo zangu huko waliko'*  nililala mpaka asubui kutoka sebleni Jacky alikuwa keshapika chai, tulikaa mezani tukanywa chai kwa pamoja. Baada ya kumsaidia Jacky kusuuza vyombo nilimuaga George kwani Jacky alishakwenda kazini. Hata George alikuwa akifanya kazi ila kipindi hicho alikuwa likizo. Niliondoka na kwenda hadi dampo sikuwa kama kapurwa tena nilikuwa nmevaa vizuri kana kwamba Mike alinipita bila kunitambua. Na Mike alikuwa kiburi ukimuita haji labda akujue na wakati mwingine hata aliowajua hakuwaitikia. Nilimfata na kumshika mkono ndipo aliposimama
"Heeee Dada Getrude ni wewe au macho yangu jamani?!!!"alishangaa sana
"Ni mimi Mike"
    Nilimshika kiganja chake kwa mikono yangu miwili nilimwelezea juu ya msaada nilioupata hivyo nilimueleza kila kitu hata hali ambayo nilikuwa nayo. Ilikuwa ngumu kuona machozi ya Mike ila alivyojua mimi nilikuwa mjamzito alilia sana alipata hofu juu ya maisha yangu. Baada ya kuongea na Mike nilimpa hela kidogo za kutumia,niliondoka na kwenda hadi kule alikokuwa akiishi Julian. Kwa bahati nzuri nilimkuta Julian akiwa anatoka ndani,alikuwa amedhohofu sana roho iliniuma sana nilimvutia pembeni na kuanza kuongea nae alilia sana alinielezea jinsi yule mama alivyokuwa akimtesa alinionyesha makovu aliyonayo mwilini nilijikuta nalia tuu nilimuahidi kurudi kumchukua
"Julian nisamehe mdogo wangu kwani mimi ndio chanzo cha mateso yako ningejua nisingekukabidhi kwenye hio familia, ila nipe muda kidogo tuu mdogo wangu nitafanya kazi nikipata tuu hela nitapanga chumba alafu utaishi na kaka yako Mike"
       Julian alikuwa hana cha kuniambia nilimwambia tuu akimbie dukan kabla yule mama hajatoka . Ila kabla hajaondoka yule mama alitoka ndani alianza kuturushia maneno makali huku akinitukana kuwa nilikuwa nikijiuza sasa hivyo nilikuwa nikitaka kumchukua mdogo wangu ili nikamuuze na yeye nipate hela. Alimuita mdogo wangu na kumpiga mbele yangu sikuweza kumtetea hata nilibaki nikilia tuu.

*Usikose MALIPO SEHEMU YA 05 kujua yatakayojiri*

MALIPOOù les histoires vivent. Découvrez maintenant