MALIPO SEHEMU YA 06

19 1 0
                                    

*Endelea......*
STORY: *MALIPO*
MWANDISHI: *IRENE SYILIVESTER MBUYA*

              *SEHEMU YA 06*
        Nilishtuka alifajiri sana nikiwa bado nakumbuka maneno ya yule mama jirani sikuamini kabisa mara swali likaijia 'Getrude umekaa hapo ukisubiri nini? Amka nenda kamtafute Mike' ni nafsi yangu ilikua ikiniambia hivyo nilijitizama kwenye kioo na kuongea na kioo kama naongea na mtu,nilikua nikijilaumu na kujilalamikia sana mara hapohapo wazo jingine likanijia kwamba nikamtafute yule mama anieleze ilikuwaje mdogo wangu akala sumu ndani kwake,yeye alikuwa wapi io sumu alieka wapi wakati alikua anajua kabisa ile nyumba ina watoto na kwanini asile mwanae akala Julian huu ni mchezo kabisa wamemuuwa Julian hawa mashetani kwanza hapa napoteza muda ngoja niwafate. Nilisimama mara moja kama askari jeshi aliefuzu mafunzo yote nilichukua mswaki na maji baada ya kufanyia kinywa changu usafi nilivuta mzula wangu (kwa jina lingine boshori) nikavaa kwani sikuwa na mpango wa kuchana nywele muda ule. Nilishika malapa(alimaarufu kama kandambili) yangu nikitembea kwa kunyata mpaka nilipoufikia mlango taratibu nilifungua makomeo na kutoka nje. Hapakuwa na mlinzi katika nyumba ya Jacky,hivyo nilifanikiwa kutoka bila kuonekana na George wala Jacky,nilitembea kwa miguu mpaka kwa yule mama japo kuna umbali ila nilifika niligonga geti na alifungua dada mmoja 
"Za asubuhi?"
"Nzuri tuu nikusaidie nini?"
"Nina shida na mama wa nyumba hii"
"Wewe ni nani ili nimuambie?"
"Nimekwambia nina shida na mama wa nyumba hii sasa hayo maswali yote ya nini?
      Tukiwa bado tunazozana yule mama alikuja na kuuliza
"Kelele za nini asubuhi asubuhi?" Ila hakuwa ameniona aliponiona alishtuka sana
"Aaaa unashtuka kwasababu unajua  ulichokifanya sasa leo utajua kuwa maisha ya mtu hayachezewi kamari"
"Sabrina hebu nenda ndani" alimwambia yule dada alienifungulia geti kisha akaniangalia akiwa hajui aniambie nini
"Naomba uniambie mama kwanini mmeniulia mdogo wangu?"niliuliza nikiwa nalia
"Sisi sio wauwaji ilikuwa tuu bahati mbaya"aliongea kwa sauti ya chini tuu
"Bahati mbaya?!! Kwanini hiyo bahati mbaya imkute yeye na sio mwanao? Dawa zenyewe zimeandikwa weka mbali na watoto sasa wewe ilikuaje sumu ukaeka karibu na mtoto kisa sio mwanao si ndio?" Nilikua na hasira sana nilitamani hata nimpige mawe
"Getrude mwanangu..."kabla hajamalizia kuongea nilimkatisha
"Umuuwe mdogo wangu ndio uniite mwanao mama yangu hakuwa kama wewe,mara ya mwisho kuja hapa unakumbuka uliniambia nini? Unakumbuka uliniita majina gani? Unakumbuka uliongea vitu gani? Ila sikujia hayo, mimi namtaka mdogo wangu  nimesema namtaka mdogo wangu,kwanza mmemzika nyie kama nani ndugu zake hatupo mbona msitutafute,mwende tuu mkamzike mdogo wetu mliambiwa na sisi tumekufa? We mama wewe hukujua kama nina kichaa si ndio? Au ulijua nitanyamaza tuu kama ulivyokuwa unampiga siku zile kama wewe si muuwaji kwanini mumzike nyie na wakati mnafahamu fika kaka yake hayuko mbali kwani dampo ampajui ninyi mngemtafuta Mike angewaleta nilipo mlishindwa nini? Kama hamkuwa tayari kumlea mngenipa siku ile ile niondoke nae nilikua nikikusikia sana ulivyokua ukimtesa hata ile siku uliyomtolea nguo afue si kwamba sikuona nilinyamaza tuu kukuheshimu,mimi nimelala hapo kwako muda sana pasipo wewe kujua mateso aliyopitia mdogo wangu wakati mwingine nilikuwa  nikiyashuhudia kwa macho yangu,sasa kabla sijaenda mbali niambie kwanini mmemuuwa mdogo wangu?"
       Nilichachamaa huku nikimtisha kuwa akumbuke kuna sheria na nilimchanganya zaidi baada ya kumwambia kuwa nilikuwa nikimuona vile alikuwa akimtendea mdogo wangu. Hakuna mtu asieogopa kufungwa,kitendo cha kufungwa kwanza nikitendo cha kukosa uhuru wako mwenyewe huwezi fanya chochote unaishi kwa muda mara lima,mara,cheza,mara lala,mara kula,mara oga na wakati mwingne muda ukipita hujala utajuwa mwenyewe si kazi ya bwana jela,huwezi amua kuwa naenda kula saivi au nitalima badae,hivyo lazima angeogopa tuu. Niliendelea kumgomea pale getini akiniomba niingie ndani lakini nilikataa katakata mpaka mume wake nae akatoka ndani kusikiliza mke wake anazozana na nani getini.

*Usikose MALIPO sehemu ya 07*

Has llegado al final de las partes publicadas.

⏰ Última actualización: May 05, 2019 ⏰

¡Añade esta historia a tu biblioteca para recibir notificaciones sobre nuevas partes!

MALIPODonde viven las historias. Descúbrelo ahora