Buriani mwafaka

109 11 12
                                    

                       Sauti na nafsi ya waridi

Katu si ajabu, kunipalilia ua, kuninyunyuzia , kunilisha kwa mbolea nikakua na kupendeza kwa macho na harufu kuvutia.

Ajabu ni kuwa sikuchagua kutupwa katika lindi la mauti au kutumika kwa madhumuni ya kuboresha mapenzi. Mchumba kumzawadia mwenziwe kwa ua. Pengine hakikisho ni iwepo ningepata fursa kujizungumzia ningechagua kuwa nyekundu tu, si nyeupe ,buluu au  rangi mnazonipaka kwa kutumia mbinu za kisasa ,ningeweza tu ningewakashifu wote walionitumia vibaya . Waliinitumia kusaliti mapenzi , waliowakatisha roho wapendwa wao kisha kupumzisha nafsi zao kwa kuniweka juu ya chumba chao cha kusafiri mbinguni, kuuzwa ughaibuni na kufaidi walionyakua cheo za juu na kumsahau mkulima aliyejitahidi kunawiri kwangu . Ningechana mbuga na kuotea msituni ili walio na kiu wapitie midomoni chatu.

Sina kashfa kwa waliopoteza wapendwa . ila ningependa kuwepo na kutumika kama njia mwafaka wa buriani .

Mie hushangazwa  na wanadamu, wapo ambao hawanihitaji hadi wakati wenzao  watakapo aga dunia,Na je, madhumuni yangu kuu ni kutumika kama pambo katika maisha au njia mwafaka ya buriani ,

Buriani mwafaka

-----------------**------------**---------**--------**------**--

Tukienzi kiswahili ,si katika mazungumzo pekee bali pia maandishi, haswaa kukisoma na kuwaalika waandishi chipukizi wanaojitosa katika uga wa uandishi .

Asante kwa kukisoma kifungu hiki cha kwanza , dokeza maoni yako hapa chini nitafurahia kupata kutoka kwako.

Lucky maingi

Kitanda Cha MautiWhere stories live. Discover now