Huenda kwa kutazama filamu tu yatosha kupata funzo , kutahadharisha au keulimisha ,yote sawa . Huenda ukapendezwa na kuiga hulka za wahusika katika filamu. Mja huenda akafanikiwa kuiga ilhali mengine yakabakia utandawazi , ndoto tu! .
Kuitazama filamu au vipindi hivi humpa mtu msisimko wa kutodhubutu kutoitazama msururu wa maonyesho, hasa filamu za mapenzi kwa kupania kujua moja mbili kuhusu mapenzi. Baadhi ya filamu huiga maisha ya kisasa ya kibinadamu kisha kuongeza chuku na yanapoonyeshwa kwenye vioo vya mtandao na runinga huonekana jambo jipya na tofauti . Iwe na funzo au kukosa ni sinema tu.
Taabu alishabikia vipindi vya mapenzi akitawala rimoti kila jioni kwa vipindi vya saa kumi na mbili na saa mbili.
Jioni moja sebuleni aliitazama filamu hii nisiyoikumbuka vyema ,'Maria... imposter labda'
"Wanaume wa kiafrika wamekosa uzito wa huba wa kisasa , utamdhulumu binti vipi kisha ukose matamu tamu ya kumfariji, kumpaka mafuta kwa ishara ya pole..?" Ilikua kauli yake Taabu . Baadhi ya mijadala yasiokua na mshindi kati yake na mimi . Atakayempiku mwenziwe kwa hoja avishwe taji, lakini mbona nivishwe taji ilhali Taabu kwa miaka zake alifahamu mengi ya kunizidi hata hivyo si bubu huzungumza kwa lugha yake. Halikunikera kwamba Taabu alipenda sana kutilia doa wanaume wa kiafrika kwa kuwadunga mishale , 'eti mavazi ya kitenge na khaki bado yamejaa kwenye wall drop na viatu vizito vya ngozi ya ngombe, Mara nywele ngumu kiasi ya kungarisha sufuria ,kushindwa kuipa ndevu umbo mraba kuvuta utanashati... ' Ni baadhi ya kejeli zake nyepesi katika mijadala za ghafla .
Wakati mwingine huvuta mawazo na kuwaza kuhusu swala la kijinsia na vita ambazo kwa mtazamo wa ndani hazitawai kesha ila kukete . Kwa mfano mwishoni wa karne ya kumi na tisa na mwanzo wa huu wa ishirini , jinsia ya kike haingeshiriki katika majadiliano ya wazee na uongozi , ziliaminika kua za kiume pekee .
Baadaye mashujaa wa kike wakasimama imara kutetea jinsia yao na mda kwa mda wakapata kutambulika na haki zao vile vile , wakapata fursa ya kujitosa katika taaluma za kujichagulia , lakini hata hivyo nafasi zao katika uongozi ni fenye , ntaipigia upato nchi ya Rwanda , wanawake wamechukua asilimia sabini katika uongozi huenda tukawapa fursa nchini wakafanya vyema kama wenzao wa Rwanda , ni wazo tu. Wanawake wakahimizwa wapate elimu ya vitabu huku alama za kufuzu zikipunguzwa ikilinganishwa na ya wavulana iliyosalie mle juu kwa mwenye nguvu mpishe, mwenye akili apite, .
Asilimia thelathini ya viti vya uongozi vikapewa wanawake , Benki ya wanawake ikazinduliwa , sheria Kali thidi ya dhulma ya jinsia ya kike yakakazwa kamba na haki zao zikatambulika barabara.
Hivi sasa takwimu katika utafiti waonyesha idadi ya wanawake imeongezeka hadi takriban asilimia sitini zaidi ya wanaume ya thelathini na tisa nukta. Cha kushangaza ikiwa mama kampigania
bitiye na kumsahau mwanawe wa kiume . Hivi sasa mawimbi yamegeuza wimbo kutoka mtoto wa kike kuelekea wa kiume ingawaje hafifu , uliopewa mada "boy child" .
Mie si mtafiti au mtabiri ila huenda mkondo ukabadilika na mtoto wa kiume akitetewa kutopewa fursa sawa na wa kike katika maswala yanayohusu wanawake na vijana . Mtoto wa kike atanufaika kuwili ;katika kitengo cha wanawake na ile ya vijana , ilhali wa kiume akifaidika ujanani pekee , wakizama majini na kukosa nguvu ya kurejea ufuoni huku wa kike ukipewa kipaumbele...
Ningezidi kujitosa katika lindi la kijinsia na kukumbuka waliopuuzwa kabisa ambayo ni jinsia ya tatu ilipewa anwani "The third gender" lakini ya Taabu yangenirejesha hapa alipo. Uga wa mapenzi. Sikua mtaalamu katika sekta ya uchumba lakini kwa kusoma na kusikiliza kulinifanya kujikunjua kutokana na mitego yake Taabu, Mara angedokeza " Biblia yampa mume mamlaka ya uongozi katika familia , jinsi mfalme anajukumu na kuitumikia watu wa ufalme wake , vivyo hivyo ndivyo anatarajiwa kumhudumia mkewe, kumpa kila kitu anachohitaji, kazi ya mkewe ibaki kushughulikia nyumba na kumpikia mumewe bas! Kwisha. Au vipi?" Kwa madaha Taabu angeniuliza kwa kuchora alama kubwa ya Z hewani na duara kwa vidole, alivyodokeza mke wa taswira yake alijichora kama mnyonge na mtegemea nundu ila kwa kuchagua kutolipua bomu kutoka kinywani mwake nilijibu kwa upole " kweli Biblia imeeleza wazi vilevile Kurani, na kumpa mke majukumu yake ila sikutegemea kidole kimoja kuvunja chawa , hivyo basi afaa kuwa msaidizi , si kucharazwa kwa kila wajibu, japo kufifia ,amshike mkono,ni mime wake aise.. " " Kwa hivyo mwanamume asiwajibike ,ategemee usaidizi wa mwenziwe ?ooh kisha anone kingurue kwa kutegemea nundu ? Mke akimshinda mume kuwajibika mume hugeuka kuwa mzigo kisha kutapatapa ......"