The witness.

26 1 0
                                    

"Shhittt!!, Go after her."

"Usije ukampoteza its either her or us. I'll finish this up." Jumoz alimwambia kwa sauti Benny aliyekuwa akikimbia kumkamata msichana aliyekuwa akiwarecord.

Ni katikati ya msitu wa Nruki wenye milima yenye view nzuri lakini pia ni sehemu ambayo sio watu wengi hutembelea kutokana na umbali uliopo kati ya makazi ya watu na sehemu hiyo. Naki ni msichana anaependa sana adventures and exploring. Ni msichana mwenye creativity, passion na asiye na uwoga wa kujaribu chochote na anaependa sana social networks   Kwasababu ya hivyo vitu tarehe, 4,july maisha yake yalibadilika na kuchukua njia mpya baada ya kushuhudia mauaji ya kikatili katika msitu huo.

Alihema kwa tabu baada pumzi kukata kutokana kukumbia umbali mrefu bila kupumzika kwa kuoga wa kupoteza maisha yake kwenye mikono ya wauwaji wawili.
"Mungu wangu, njia ni ipi tena ya kurudi nilipotoka?!" Naki aliwaza akiwa amejificha nyuma ya mti mkubwa huku akiwa na uwoga usioelezeka. "Ni kina nani wale? Na yule waliomuua ni nani?! Amewafanyaje mpaka wamuue kikatili kiasi kile?! Wakinikamata ni lazma nitaniuawa" Aliendelea kuwaza.
Ghafla alikatizwa na hatua za kishindo ambazo zilikuwa zinaenda alipo.
Aliganda akiwa amefunga macho na kuzuia pumzi ili kuepusha kusikika lakini katika hali ya uwoga wake usiozuilika, hatua zilivyozidi kusogea alipo, alitoa mguno kitu ambacho kilimfanya atoke mbio akiwa tayari ameshajua kaonekana. Naki alikimbia huku akihema kwa nguvu.
"Naitaka hiyo kamera tu. Nipatie in return I'll spare your life." Benny alishout kumwambia Naki huku anamkimbiza.

Akiwa katika hali mbaya Naki aliendelea kwenda bila kutambua hata anapoelekea. Begi alilokuwa amebeba lenye jina 'Vent' ambalo hakulifunga vizuri lilikuwa linadondosha vitu vyake huku akikimbia.
Aligeuka baada ya kusikia kama hakimbizwi tena, ndipo alipoona Benny akiokota kipochi chake ya IDs, alitazama begi lake na kugundua lipo wazi akaligeuzia mbele na kuendelea kukimbia.

Giza limeanza kutanda msitu unazidi kutisha na kumuongezea uwoga msihana Naki. Kwa bahati nzuri alifanikiwa kuona barabara inayopita magari. Nguvu ilimjia upya akaanza kukimbia kuelekea ilipo barabara hiyo. Alikimbia huku akiomba msaada kwa kila gari iliyopita, in her suprise aliona kijiji mbele yake kitu ambacho kilizidi kumpa nguvu ya kuendelea kwenda.

"Mzee samahani, Nipeleke kituo chochote cha polisi unachokijua nitakulipa ukitaka" Naki alimwambia mzee aliyekuwa anakokota baiskeli yake.
"Hapa kikijini hatuna kituo chochote cha polisi labda kwa mwenyekiti." Alijibu kijana huyo huku akimshangaa Naki alivyokuwa rough na alielowana jasho.
"Nataka polisi!!!" Naki alifoka ghafla akaanza kulia. "Samahani, Naomba niambie napata wapi japo usafiri unaoenda mjini?!" Aliuliza Naki kwa sauti yenye mawimbi ya kilio.
"Binti unatatizo gani?" Mzee yule aliuliza
"Nahitaji usafiri wa mjini" Naki alisisitiza.
"Usafiri hapa mpaka kesho muda umekwishaenda sana mwanangu. Umepatwa na nini?!" Mzee aliuliza.
"Maisha yangu yapo hatarini" Naki alijibu akiwa anaanza kutembea huku akiwa kama kachangayikiwa.
"Binti nini shida?" Mzee aliendelea kuuliza huku akiwa hajui hafanye nini.

"Nitaenda wapi usiku huu ambapo hawataweza kunipata?! Au Niombe malazi kwenye nyumba yoyote?! Kijiji kilivyo kidogo hivi wakipita nyumba hadi nyumba Naki si nimeisha mimi jamani?" Aliwaza Naki akiwa analia huku akiendelea kupanic na kushindwa kujua afanye nini.

"Gari.., Mungu wangu asante!" Naki alihamaki kuona gari mbele yake aina ya suzuki ikiwa imepaki kwenye nyumba moja hapo kijijini.
"Hodi, Hodi"  Naki aliita hodi katika nyumba ile.
Alitoka kijana marika yake kumsikiliza.
"Karibu", yule kijana alijibu.
"Asante, nashida naomba kuongea na mtu mzima au zaidi mwenye hii gari na shida ya kuenda mjini sasa hivi, tafadhali sana" alijielezea Naki.
"Ni nani? Akaribie ndani." Sauti ya mwanamke ilisikika kutoka ndani.
Wakati huu Naki alianza kupata matumaini na amani kidogo akajisikia yupo sehemu salama.

Aliketi akaomba maji ya kunywa akiwa tayari kuomba msaada anaouhitaji, simu ya mmoja ya aliowakuta ndani iliita.

Akiwa anakunywa maji Naki aliulizwa, "Ehe binti, unaitwa nani, umetokea wapi na unahitaji tukusaidie nini?"

Naitwa Naki Benson, ni...... ghafla akasikia mtu aliepokea simu akisema, "Tararibu sijakuelewa, unasema hamkuwa  wenyewe kivipi na kazi nimewapatia wawili tu?
Binti unasema umetokea wapi vile?! Aliuliza mama aliyekuwa akimhoji Naki.
Mimi?.. Naki aliongea kwa kuuliza
Ndio, umesema unashida gani?! Yule mama aliendelea.
Nina...
"Mtoto wa kike anawashinda wanaume wawili??! hii kazi imetoka huko juu, ikiharibika hasara yake hata maisha yenu hayawezi kulipia. Nataka apatikane leo leo huyo aliyoona na ushahidi anaotembea nao." Aliongea kwa ukali na kukata simu.
Kuna nini Jimmy?! Yule mama alimuuliza mwanaume aliyekuwa akiongea na simu.
"Hamna mama ni kazi za watu tu." Alijibu jimmy.

"Oh my God!! Oh my God!! Oh my God!!
Huyu anaongea na wale wauwaji, na yeye anahusika, asije akajua mimi ndio msichana wanaemtafuta, naondokaje hapa??!!"
Naki aliwaza huku akiwa anaonyesha panic.
"Uko sawa dada?!" Jimmy alimuuliza Naki.
"Aahh, ndio, ndio nipo sawa, nipo sawa kabisa,.. asanteni kwa maji" alishukuru huku akiwa anasimama na kuondoka.
Subiri,ulisema unashida gani vile?! Yule mama alimuuliza Naki.
Huku akiwa anajitahidi asionyeshe wasiwasi, Naki aligeuka na kusema "nilikuwa na kiu sana na nyumbani ni mbali kidogo nikaona nipite kuomba maji.

Si ulisema unashida ya kwenda mjini saiv?!!
Yule kijana aliyemkaribisha Naki aliuza.

Mjini sasa hivi?! Jimmy aliuliza huku akimwangalia Naki.

Nini kitatokea?

Je, Jimmy atagundua Naki ni nani?




THE WITNESS Where stories live. Discover now