Power of Bravery.

20 1 0
                                    

Usiku ule Benny na Jumoz walikuwa wameshakutana na wote wakiwa kijijini pale wakichanganua namna ya kumpata msichana Naki.

"Anaitwa Naki Nelson Sebastian, miaka 26." Benny alimsomea Jumoz moja kati ya IDs alizokuta kwenye kile kipochi.
"Sasa hizo info zitatusaidia nini jamaa? Umeshindwaje kumkamata?! Atakuja kutuletea shida huyu, Jimmy amewaka moto huko alipo inabidi tumpate huyo msichana leo hii kabla hapajakucha." Aliongea Jumoz huku akilaumu
"Hivi vitambulisho vinaonyesha wazi kwamba huyu sio mtu hichi kijiji na, . . . . ingekuwa ni rahisi kumkamata, saiv angekuwa futi sita chini." Alisema Benny
"Mimi ndiye nitakae muadabisha kabla ya kumnyamazisha pindi tutakapo mkamata." Benny aliendelea kwa hasira.
"Tunaanzia wapi sasa?!" Benny alimuuliza Jumoz.
"Kama si mkazi wa hapa its not too late itabidi kila gari inayokwenda mjini tuiangalie kwanzia kesho mapema sana. Ngoja nipige simu kumtaarifu Jimmy kuhusu hii plan." Alisema Jumoz.

(Tulipoishia kwa Naki) . . . .

"Unataka kwenda mjini kufanyaje saiv?!" Yule mama alimuuliza Naki.

"Hapana mama sio kwenda mjini saiv. Nilitaka kujua kama mtaenda mjini kesho niweze kuomba lyft." Naki alijielezea huku akiwa anatabasamu kuwaondolea any doubts.
"Ahaa. . . Lyyft." Alisema yule mama

"Huyo kijana ndio amekuja na hio gari kutoka mjini ongea nae." Yule mama aliongea huku akimnyooshea Jimmy kidole.

"Mungu wangu, najikomboaje hapa mimi."
Naki aliwaza.
"Mjini unataka kwenda kwenda sa ngapi?"
Jimmy aliuliza

"Ngoja nionyeshe kama sina uhitaji wala haraka ya kwenda sana mjini."Naki alijiambia kichwani.
"Unaulizwa," yule mama alimwambia Naki
Naki akashtuka,

Naam. . . ., Mimi muda wowote tu utakaotaka kuondoka ni sawa kwangu. Alijibu Naki.

"Ahaa sawa kuna vitu vichache nakamilisha. Vikiisha tu, kesho utapata lyft." Jimmy alijibu akiwa anaonekana yupo distracted na simu

"Sawa nitashukuru. Asanteni sana mimi nakwenda." Naki alishukuru na kuaga haraka.
"Binti, subiri saiv ni usiku,
Hebu mtoe mgeni." yule mama alimsubirisha Naki na kumwambia kijana aliemkaribisha Naki wakati alivyobisha hodi

"Usijali mama, Natoka kwenda kuonana na watu ngoja nitoke nae." Alisema Jimmy

Hapana hapana, hamna shida, nipo na wenzangu wananisubiri nimewaacha dukani tu hapo. Kweherini. Alijibu Naki na kutoka nje haraka.

"Oh my God!!!
Sasa hivi ninawakimbia watu wa tatu, wawili kati ya hao wananifahamu kwa sura
My chances for survival are thin. Nitaenda wapi mimi.? Simu yangu imezima. Think Naki, think." Naki alijisemesha mwenyewe huku akiwa nakazana sana.

"Nilisema mbali, porini kabisa na ndio mana tumekuja huku kijijini. Sasa mmefanya nini?
Yuko wapi?" Jimmy aliwasemesha Jumoz na Ben kwa ukali.
Bado hatujampata mkuu. Alijibu Jumoz
Sasa umeniitia nini?! Mtafuteni mumpate. Alifoka Jimmy.
Nilivyokuwa namkimbiza alidondosha kipochi chake, hichi hapa mkuu. Ben alimwambia Jimmy huku akimpa kipochi cha Naki alichookota.

Jimmy alitoa moja ya IDs za Naki na kuanza kusoma jina kwenye kile kitambulisho na kuangalia picha iliopo.

"Huyu. . . , ndio mtu tunaemsaka?!!" Aliuliza Jimmy kwa mshangao.
"Ndio mkuu." Alijibu Ben
Anabegi la mgongoni jeusi?!! Vimeandikwa Vent?!! Jimmy aliuliza tena
Ndio huyo, umemuona wapi?! Aliuliza Ben kwa shauku

"God damn it!!!!!" Jimmy alishout
"Umemuonea wapi?!" Jumoz alimuuliza tena Jimmy.
"Sijumuona tu,..." then akasita,
"Oh c'mon, why didnt I figure it out earlier??!!..shit. . , shit. . , shhittt!!!!!" Alishout Jimmy na kushusha pumzi kwa nguvu kisha akaendelea,

"Nilikuwepo nae muda si mwingi kwenye ile nyumba niliofikia mimi baada ya kuwaacha nyie katika lile eneo."
"Yuko wapi. . . , umemuacha katika hiyo nyumba??!" Aliuliza Ben kwa shauku.

"Hapana aliondoka akiwa ana haraka sana," then Jimmy akakaa kimya sekunde kadhaa . . . Kisha akasema,
"Haraka lets go, lets go, huyu msichana anatafuta usafiri wa mjini, bado yupo ndani ya hichi kijiji ni lazima awe mikononi mwetu usiku huu. Jimmy aliwaambia wenzake huku akianza kutembea kwa haraka.

"Dad, I need help. . .Nataka kuja nyumbani, naogopa sana." Naki alikuwa anaongea mwenyewe huku analia akiwa yupo ndani ya nyumba ambayo haimalizika ujenz.

Akakumbuka alichowahi ambiwa na baba ake. "Ukijua upo na mwizi karibu, weka mali zako kwake, siku zote zitakuwa salama."

" Yes,. . .Inabidi nirudi kwenye ile nyumba, niwe japo karibu na pale, watanitafuta kila sehemu lakini sio walipo wao." Alijiongelesha Naki kisha akaanza kutembea kwa wasiwasi akiogopa asije akakutana na wauwaji wanaomsaka kuelekea kwenye ile nyumba aliyoikimbia mwanzo.
Naki alirudi katika ile nyumba na moja kwa moja akaingia chini ya gari(suzuki) iliyokuwa imepark nje na kulala sehemu ambayo surface ya gari ilizibwa na maua yaliopandwa katika nyumba hio.

"Mungu najitoa kwako unilinde." Naki alisema kimoyomoyo.

Kutonakana na purukushani alizopitia Naki, she was exhausted, na licha ya mazingira aliyokuwepo, alikuwa akipitiwa na usingizi wa mang'amung'amu.(kushtukashtuka)
Majira ya sa tisa usiku Naki alishtushwa na hatua za watu waliokuwa wakitembea kulifata gari lilipo.
Alikuwa ni Jimmy na wenzake.

"Itabidi nipige simu kabla hili swali halijawa out of hand." Jimmy aliwaambia wenzake kisha akafungua mlango wa gari na kutoa simu iliyokuwa imefichwa chini ya siti. Akaiwasha na kuanza kuadial namba, iliita na kupokelewa.

"Samahani sana mheshimiwa, . . nimekutafuta kwasababu kuna tatizo limetokea." Alisema Jimmy kwa heshima kisha akaendelea,

"Ndio, ndio mheshimiwa, nii. . . . .," akakatizwa kisha akasema,
"hapana ile imeenda as planned lakini wakati tunafanya hivyo kuna mtu alituona, akarecord kila kitu na mpaka sasa hatunae." Alisema Jimmy
Simu iliendelea kwa muda Jimmy akiwa anasikiliza bila kujibu chochote.
Baada ya muda Jimmy alianza kuongea tena

"Kuna kipochi aliangusha wakati tunamkimbiza kina information zake ndani . . .
Sawa, nitakutumia"

Kisha Jimmy akaendelea kukaa kimya.

Kule chini ya gari Naki alikuwa akitetemeka kwa uwoga
"Mungu wangu, huyu anaejiita Jimmy anaongea na nani? Nani atahitaji information zangu,? Na za nini?. Huyo muheshimiwa ndio nani?! Na ndio aliowapa hawa watu kazi ya mauaji." Naki alijiuliza maswali mengi huku akiwa ni mwenye uwoga sana.

Ghafla akasikia simu imewekwa loudspeaker. Sauti ya mwanamke ikawa inasikika.

"Oohh my God!!!, Oh my God!!!, Oh my God!!!", Naki alisema kichwani kwake.

Naki amesikia nini?!

Je, Watagundua Naki yupo walipo wao?!

Fuatilia!









THE WITNESS Where stories live. Discover now