Sura ya Tatu

30 0 0
                                    

Mzee Moja aliianza safari yake ya kuwa mumiliki wa daladala kwa kununua gari zee na kulitengeza ili kuwavutia wasafiri.

Alilifufua na kulipa uhai mpya,umbile jipya.

Baada ya muda alichukua mkopo kutoka kwa benki yake na kuyanunulia magari mengine mawili.

Akiwa kituoni alikuwa meneja wa biashara zake zote.

Rebeca alimsaidia katika kuoka keki na kuzisambaza.

Kwa sasa walikuwa wameweza kununua tanuri la kisasa lililotumia stima.

'Mzee Moja Bakers' ilikuwa imezaliwa na kuingilia uokaji wote wa keti,mikate,biskuti na kadhalika.

Kulikuwa na wafanyikazi zaidi ya ishirini,waliojihusisha na uokaji na kusafirisha kwa kutumia pikipiki.

Kwa kuwa 'makao ya mke ni jikoni',Mzee Moja alikitosa zaidi katika biashara ya Magari na kumwachia Rebeca kuendesha kiwanda cha uokaji.

Kinyau alifaidika pakubwa kwa kuhusishwa kama fundi wa  pikipiki.

Ajabu ni kuwa Kinyau hakuwahi kuhudhuria chuo chochote kujifunzia ufundi wa pikiki.

Licha ya kuhitimishia masomo katika shule ya msingi alikuwa na ufahamu mkubwa kuhusus mitambo.

Wakati mwingine alihusishwa katika kuzitengeneza mashine mabalimbali pale kiwandani.

Kilikuwa ni kipawa na majaliwa.

Wakati mwingine aliongezea ufahamu wake kutoka kwa mtandao wa 'youtube'

Alizidi kubobea.

Biashara zilikuwa zimenoga.

Pale kituoni wafanyi biashara walikuwa wamejiunga katika vikundi na kuanzisha vyama vya kuhifadhi na kukopesha pesa.

Vyama vilivyowasaidia mno kugharamia upanusi wa biashara zao.

Vyamba ambavyo pia viliwawezesha kupata mikopo kutoka kwa benki na mashirika mengine ya kifedha.

Ni kupitia kwa njia hii ambapo Mzee Moja aliweza kupata hela za kuinua biashara zake.

Kuna waliomwonea shime na waliomwonea gere  kwa ufanisi wake.

Wamiliki wa kampuni za uokaji,hasa za kitaifa hawakufurahia umaarufu wake uliokuwa ukikolea kila kuchao.

Njama ya kumwangamiza Mzee Moja ilipangwa.

Kokoti alipwewa jukumu la kumwanagazima uokaji wa Mzee Moja.

Keki zake zilinunuliwa na kutiwa mafuta taa na kisha kuuziwa walaji.

Lengo likiwa kuzua gadhabu miongoni mwa wateja wake na kumuweka kwenye njia panda ya sheria.

Njama ilipikwa,kuivishwa na kisha kuandaliwa mezani.

Walipanga wanunuzi ambao wangezila zile keki sumu na kisha kusingizia matatizo ya kuhara na kutapika.

Kipawa cha uigizaji cha Kokoti kilipata mwanya wa kumutumbuiza shateni.

"Muna ninawo wasee?"

"Hizi kei tutazimanga kisha tujifanye tunawahiwa na mwendesho!"

"Munacheki?"

Kokoti aliwaelekeza wanasanaa wenzake.

"Tunawo msee!" ,walijibu kwa pamoja.

"Nyinyi ni mbogi genje! ama niaje wasee?"

"Ni ndoo tu tunasakanya,na wira ni....."

HIMAYA YA MZEE MOJAWhere stories live. Discover now